Thursday, June 22, 2017

Siri ya Herufi ya Mwanzo ya Jina Lako


HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.

HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.

HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.

HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.

HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.

HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.

HERUFI G 
mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.

HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.

HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.

HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.

HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.

HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.

HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.

HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.

HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.

HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.

HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.

HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.

HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.

HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.

HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.

HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.

HERUFI Y 
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha.

HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo,
je na jina lako lina maana gani? Jibu usione aibu!Sambazaaa hii

Saturday, June 17, 2017

Umaskini Wako Chanzo Chake Hiki Hapa!!!!



Kuna wakati umekuwa ukujiuliza sana kwa nini wewe ni maskini na kwa nini wengine ni matajiri, labda nikwambie tu hivi, usiendelee kujiuliza swali kama hili ngoja tu ni kupe jibu la moja kwamba, umaskini au utajiri unaanzia kwenye akili yako.

Kile unachokifikiria sana kwa muda mrefu bila kujali unafikiria umaskini au utajiri hicho ndicho utakachokipata. Hauzuiliwi kufikiria na kutenda kitajiri hata kama pato lako ni dogo au hata kama unajiona ni maskini, lakini tambua chanzo cha umaskini au utajiri ni akili yako.

Kwa hiyo kwa mfano unajiona umepigika, huna pesa mfukoni na umejikuta umekuwa ni mtu wa kukopa huku mara kule, hiyo ni dalili tosha kwamba pia  ni matokeo ya akili yako iliyopigika ama akili ya kimaskini ambayo umewekeza kwa muda mrefu.

Kama upo katika hali hii, haina haja ya kujichukia au kujiona hovyo hovyo kubali kujirekebisha na kuchukua hatua zitakazokuwezesha kusonga mbele kimafanikio. Ukiwa mbishi, nikupe uhakika huu utaendelea kuteseka na umaskini.

Kwa hiyo unatakiwa uangalie na kujua kwamba kinachokufanya uendelee kuwa maskini sio kwa sababu huna pesa au huna mtaji, bali ni kwa sababu ya matokeo ya mfumo wa mawazo yako ulionao na umeujenga kwa muda mrefu.

Dawa pekee ya kuweza kukata mizizi ya umaskini ni kwa wewe kuamua kubadili mfumo wa mawazo ambayo unayo ya kimaskni na kujenga mfumo mzuri chanya utakao kuwezesha kukusaidia kufanikiwa.

Chanzo cha utajiri na umaskini wowote ule ni matokeo ya mawazo yako. Matokeo ya mawazo yako yanakuja na kile unachojifunza na kukiweka mara kwa mara akilini mwako,

hicho ndicho kinachoonekana kwa nje.

Ni wapi unatakiwa kuanzia ile ufutilie mbali historia ya umaskini?
1. Jifunze kila siku kuhusu mafanikio kwa kutafuta kanuni na mbinu mbalimbali zitakazokuwezesha kufanikiwa kupitia vitabu au semina.

2. Kaa na watu wenye mafanikio kwa pamoja. Jifunze kwao. Acha kung’ang’ania kuwa na watu ambao hata wewe hawana uwezo wa kukusaidia chochote.

Njia sahihi ya kukufanya wewe ukafanikiwa na kuwa na mawazo sahihi. Yatafute mawazo hayo sahihi kila siku ya maisha yako na uwe miongoni mwa watu wenye mafaniko makubwa

Wednesday, June 14, 2017

Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na Kuwatumia Nyoka Badala ya Kuwa




Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo yenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana.Sumu ya nyoka inatumika kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi hivyo thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake.

Gram moja ya "snake venom " kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25,000

*Kama unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka

1.zingatia hali ya joto na hewa .

Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29 degrees Celsius nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku,

2.mabanda na nyumba za nyoka zinahitaji kusafishwa mara kwa Mara

Hali hiyo itasaidia kukuza uzalishaji wa nyoka kwa wingi.Nyoka wanahitaji kuwekwa mahali salama kuzuia matatizo yeyote ile ya kiafya kuwapata.

3.Nyoka kwa kawaida hula panya 3-4 na hulishwa kwa wiki 3-4 .Nyoka hula panya walio hai lakini wanaweza kula waliokufa pia ,Nyoka hupenda kucheza na panya mwanzo kabla ya kuwala hivyo ni vema kuwapatia walio hai.


Faida 3 za ufugaji wa nyoka

1.uzalishaji wa venom ambayo ukiuza unapata kiasi kikubwa cha pesa.

2.hupunguza na kutokomeza wadudu waharibifu kama panya nk.Nyoka chakula chao kikuu ni panya hivyo husaidia kutusafishia shamba au nyumba kwa kuwamaliza wadudu hawa.

Dawa ya kuua sumu ya nyoka itengenezwayo kutoka kwa sumu ya nyoka, yaani anti-venom, ndiyo tiba bora pekee ya kuumwa na nyoka.

Mwisho sio kila tukiwaona nyoka tunawaua ,nyoka ni rafiki zetu na sio maadui.Tuwatumie ipasavyo watatusaidia sana

Hatua 10 Muhimi za Kumchagua Mchumba Mtakae Funga Ndoa









Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.

Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.

Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.

Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.

Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.

Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.

Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi

Sunday, March 26, 2017

Kama Unaogopa Kufanya Kitu Hiki, Sahau Kuhusu Mafanikio Katika Maisha Yako Yote...!!!

Image may contain: 3 people, people sitting and closeup


Fikiria kila unachokijua na kukikumbuka kuhusu mabadiliko unayotaka yawe katika maisha yako, halafu  uone ukweli huu  kama kweli nawe ni mmoja kati ya watu wanaotaka mafanikio au uko nje ya mstari wa mafanikio na pengine tu wewe hujijui. Kama kweli unataka mafanikio, ni kwanini  mara kwa mara umekuwa ukisita au kuogopa kufanya jambo ambalo lingeweza kubadili maisha yako na kukuletea mafanikio mkubwa? Hili ndilo tatizo walilonalo watu wengi wanahofia sana kufanya mabadiliko kwa namna moja au nyingine hata kwenye yale malengo waliojiwekea wao wenyewe kuna wakati huwa wanaogopa pia.

Kimaumbile, kila binadamiu anahofia mabadiliko, lakini hofu ya mabadiliko inapozidi kuwa kubwa na kukuzuia kufanya mambo ya maana kwako, hofu hii  sasa hugeuka kuwa ni maradhi yanayokuzuia wewe kufanikiwa. Hebu fikiria tena, ni mara ngapi umekuwa ukitaka kufanya mabadiliko Fulani  katika maisha yako, lakini umekuwa ukijikuta ukishindwa kufanya hivyo kutokana na kuogopa kufanya vitu Fulani? Ni mara ngapi umekuwa ukitaka kuingia kwenye biashara lakini umekuwa na hofu nyingi zinakuzuia? Hivi ndivyo ilivyo mabadiliko huogopwa, wakati mwingine bila sababu ya msingi.

Wengi wetu kutokana na kuogopa mabadiliko, hujikuta ni watu wa kutoa sababu ambazo hata hazina mashiko zinazosababisha wao washindwe kutekeleza malengo na mipango waliojiwekea. Utakuta mtu anakwambia  hawezi kufanya biashara ni kwa sababu hana mtaji, ukija kuchunguza kidogo utagundua kuwa hiyo ni sababu ambayo amekuwa akiitoa kwa muda mrefu, iweje kila siku mtu huyohuyo awe hana mtaji tu. Kama uko hivi una hofu tu hata kwa vitu vidogo ambavyo ungeweza kuvifanyana , tambua kuwa kuanzia sasa unaye adui mkubwa ndani mwako anayekuzuia kufanikiwa. Na unapoogopa kufanya mabadiliko ambayo unaahitaji sasa ili ufanikiwe, sahau kuhusu mafanikio katika maisha yako yote.

Tatizo kubwa utakalokuwa nalo linalosababishwa na hofu hii ya kuogopa kufanya mabadiliko ni lazima utakuwa mtu wa kutaka mafanikio ya harakaharaka. Watu wengi wenye mawazo ya kutaka kufanikiwa leoleo hata kama wameanza biashara leo, wengi wao huwa wana hofu hii kubwa ya mabadiliko ndani mwao, unaweza  kufanya utafiti mdogo utagundua ukweli huu ulio wazi. Hawa ni watu ambao kiuhalisia hawaijui wala kuiamini subira ndani mwao, bali ni watu wakutaka mfumo wa maisha uwe ambao unaanza leo biashara na wiki ijayo uwe tajiri ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.

Hivi ndivyo walivyo watanzania wengi wanaogopa mabadiliko na kuamini katika miujiza, sio katika wao wenyewe kutenda na kuona matokeo.  Hebu jaribu kukagua maisha ya walio wengi utakuja kugundua ukweli huu ni watu wanaofikiria sana leo, sasa hivi, siyo baadaye. Hata malengo yao ni ya karibu sana na hawataki shida, wanataka wafanye leo, wamudu leo na kila kitu kimalizike leo. Sijui kesho watafanya kitu gani? Ukimwambia mtanzania aanzishe mradi ili aje faidi baada ya miaka 10 kutoka sasa kwanza atakushangaa, kisha atakucheka we hadi mbavu zimuume. Anataka leo hata kama ni kwa miujiza.

Ndiyo maana wengi kati ya Watanzania hawana malengo, wanaishi tu na kutawaliwa na hofu za mabadiliko. Kuweka malengo siyo sehemu ya maisha yao, kwani malengo yanataka mtu mwenye subira, mtu anayeamini kwamba maisha ni kuanguka na kusimama. Wanachojua kikubwa ni kulalamika na kulaumu, kuponda na kukejeli, kwa sababu wao wamekata tamaa bila kujijua. Ndiyo maana ni watanzania wanne tu kati ya kumi ambao wanafanya kazi, wanatoka jasho na wanaweza kusubiri bila kukata tamaa, wengine waliobaki wanasubiri ujanja ujanja tu ilimradi wafanikiwe hata kama ni kwa kufanya uhalifu wa aina yoyote.

Ni watu ambao wanataka kuishi kihadithi, wawe na pete ambayo wanaweza kuiamuru iwape wakitakacho na wakipate. Maisha ni ya kibunuasi- abunuasi tu, watu hawa kwao mabadiliko ni kitu kigumu sana kwao na kinaogopwa kweli. Kama unataka mafanikio ya kweli yawe kwako, unatakiwa kubadilisha fikra za zako na kuamua kukubali kuwa mafanikio yanahitaji mabadiliko makubwa sana ambayo wewe mwenyewe unatakiwa uyafanye kwa kujitoa hasa. Acha kuwa na hofu zisizo na maana zinazokuzuia wewe usifanikiwe, chukua hatua katika maisha yako, kuyafikia maisha unayoyataka

Fahamu Mambo Matano ya Kushangaza Kuhusu Tangawizi

Image may contain: 3 people, people sitting and closeup




TANGAWIZI ni kati ya viungo mahili vinavyochochea ladha nzuri katika vyakula vya aina mbalimbali na hivyo kuwavutia walaji kula chakula husika.

Tangawizi pia inapowekwa kwenye vyakula vigumu kama nyama huifanya ilainike na hivyo kuweza kuiva kwa haraka zaidi. Hivyo kwa point hiyo tu kwanza utagundua kiungo hiki pia kinaweza kurahisisha umeng'enyaji wa chakula tumboni pia

Wakati tangawizi ikiwa inafahamika zaidi kama kiungo, kwa upande mwingine kiungo hicho huweza kupunguza athari za matatizo mbalimbali ya kiafya pia kama ifuatavyo kwenye orodha hii hapa chini:-

1. Hupunguza maumivu kwa wanawake wakati wa kipindi cha hedhi (Period)

2. Huppunguza maumivu ya mifupa pamoja na misuli kwa ujumla.

3.Inaelezwa kusaidia kuimarisha uwezo wa utunzaji wa kumbukumbu kwa binadamu.

4. Husaidia kutuliza maumivu ya tumbo pia

5. Husifika kwa kuimarisha kinga za mwili na kuufanya mwili kupambana vizuri dhidi ya magonjwa

Tuesday, March 21, 2017

Eheee..Askofu Gwajima Kutimba Clouds Kesho,Atoa Ujumbe Huu Mzito Kwenye Instagram...!!



Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema kuwa Jumatano hii atatembelea Clouds Media Group kwajili ya kuwapa pole kwa yaliyotokea hivi karibuni.

Ijumaa iliyopita kituo hicho kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu kitendo kilichopingwa na wadau mbalimbali wa habari.

“Kesho Tarehe 22/03/2017 saa nne kamili asubuhi, nitatembelea Ofisi za Clouds Media ili kuwapa pole kwa yaliyotokea.” aliandika mchungaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.


Yanga Fungu la Kukosa ,Yapangwa na Waarabu Kombe la Caf...!!!




Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetoa ratiba ya mechi za kombe la shirikisho. Katika ratiba hiyo klabu ya soka ya Yanga imepangiwa kucheza na MC Alger kutoka Algeria.

Yanga imeingia katika hatua hiyo baada ya kutolewa katika kombe la klabu bingwa barani Afrika na Zanaco kutoka Zambia Jumamosi hii.

Timu 32 zimeingia katika hatua hiyo ambapo mechi zake zinatarajiwa kuchezwa kati ya April 7-9 na marudiano April 14-16. Vilabu 16 ndio vinahitajika ambavyo vitaingia katika hatua ya makundi ya kombe hilo

Rais wa Zambia Apigiwa Magoti na Waziri Wake...!!!


Rais wa Zambia Edgar Lungu akinyenyekewa na waziri wake wa Mifugo na uvuvi,

Powered by Blogger.