Saturday, March 18, 2017

Arsenal Yahitaji Maombi ya Gwajima...Yachapwa 3-1



Craig Dawson akiwa hewani juu ya Nahodha wa Arsenal, Laurent Koscielny kuifungia West Bromwich Albion bao la kwanza dakika ya 12 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya timu ya kocha Mfaransa, Arsene Wenger katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa The Hawthorns. Dawson alifunga mabao mawili na la tatu dakika ya 75, huku la pili la West Bromwich likifungwa na Hal Robson-Kanu dakika ya 55 na la kufutia machozi la Washika Bunduki wa London, likifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 15

Thursday, March 16, 2017

Meya wa Ubungo Kufungua Kesi Dhidi ya Vyeti Feki..!!!



Mayor wa Ubungo Mh. Borniface Jacob anakusudia kufungua shauri mahakamani la kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuonesha vyeti vyake ili kuondoa utata uliojitokeza hivi karibuni dhidi ya kiongozi huyo wa mkoa. Kesi hiyo inatarajiwa kufunguliwa jumatato ijayo ya tar 20/03/2017.

Ahukumiwa Kuchapwa Kiboko Kimoja kwa Kumpa Mwanafunzi Mimba...!!!



Mahakama ya Wilaya ya Hai  Mkoani Kilimanjaro  imetoa hukumu ya kuchwapwa kiboko kimoja mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Longoi wilaya hapo baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo

Akisoma hukumu hiyo  Hakimu  mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Agnes Muhina  mbele ya mwendesha mashtaka wa polisi , Valeria Banda, alisema kuwa anatoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushaidi uliotolewa mahakamani  hapo usioacha shaka yoyote.

Kesi hiyo pia ilikuwa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka akiwemo daktari wa hospitali ya Hai,dawati la jinsia na watoto na mama mzazi wa binti huyo, mwalimu na binti mwenyewe.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka wa polisi  kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo   Oktoba 10, 2015 saa 8.00  mchana katika kijiji cha Mkalama Wilayani humo ambapo alimbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa kidato cha tatu mwenye umri (16).

Kimenukaaa...Magufuli Aanza Tumbua Tumbua Tena..Amtumbua Katibu Mkuu wa Wizara...!!!!!



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Bw. Uledi Abbas Mussa.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kutenguliwa kwa uteuzi na kusimamishwa kazi kwa Bw. Uledi Abbas Mussa kunaanzia leo tarehe 15 Machi, 2017.

Hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi zaidi dhidi ya Bw. Uledi Abbas Mussa kufuatia kutozingatiwa kwa taratibu zinazotakiwa katika kushughulikia masuala ya uwekezaji.

Breaking News..Tundu Lissu Akamatwa na Polisi Asubuhi Hii Akiwa Nyumbani Kwake..!!



Mbunge Tundu Lissu akamatwa na polisi asubuhi hii nyumbani kwake na kupelekwa ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma.

Taarifa Zaidi Zitakujia Hivi Punde..!!!

Thursday, February 23, 2017

Utawala Wako Binafsi Unavyoweza Kukufanya Tajiri au Maskin




Utawala binafsi ni vile mtu anaweza kuishi katika maagano na malengo yake kwa kuzingatia muda,mahitaji na nguvu aliyonayo katika kukamilisha jambo hilo. Kwa tafsiri yangu mtu akiweza kuishi katika hayo anakuwa ameweza kujitawala vizuri.

Katika uongozi wa nchi huu ni utawala wa tano kuwepo tangia Tanzania imepata uhuru,ukianzia kwa mwalimu Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete na hatimaye Rais Magufuli. Katika awamu zote hizo zilizopita watu walihusisha matatizo yao ya kiuchumi na mfumo wa maisha kwa ujumla na utawala uliokuwepo!

Mfano wakati wa Mkapa kuna kipindi umaskini au ukosefu wa pesa uliitwa ukapa,kipindi cha Jakaya Kikwete vivyo hiyvo watu walihusisha umaskini na ukosefu wa pesa na utawala wa Kikwete. Muda huu tukiwa chini ya Rais wa awamu ya tano Dkt JPM, utawala wake bado unalaumiwa kwa kuwa chanzo cha watu kukosa pesa. Natabiri hata utawala wa awamu ya sita hali itakua hivyo hivyo.

Lengo langu sio kukataa kuwa kama serikali na viongozi wake hawana la kulaumiwa katika haya la hasha! Lengo langu ni kusema kumbe inaonekana pengine ndiyo hali halisi ya viongozi wetu kushindwa kukidhi mahitaji yetu tunayodhani wanaweza kututatulia. Kumbe hili ni tatizo sugu kwa Afrika na pengine lisije kuisha mpaka pumzi yako ya mwisho itakapokata! Kwahiyo utaendelea kuishi ukilaumu tawala zote zimepita kuwa ndo sababu ya wewe kutofanikiwa?

Vipi kuhusu utawala wako wewe binafsi? Ni kweli unaishi katika malengo uliojiwekea? Ni kweli matumizi ya rasimali zako unazomiliki unazitumia sawa sawa na inavyotakiwa?

Vipi muda unaotumia katika kufanikisha ndoto na malengo ulojiwekea maishani? Au unasubiri rais na utawala wa awamu ya sita ndo uje kua suluhisho la matatizo yako?

Katika kipindi ambacho wewe unalalamikia utawala kuna wenzio wanaingiza pesa,katika awamu ulizoishi za uongozi kuna wengine wamepata utajiri na huku wakiishi katika tawala hizo hizo unazolalamikia wewe kuwa hazisaidii wananchi kufanikiwa kuishi maisha yaliyo bora.

Amini utawala wako. Ni kichwa chako ukiweza kuishi katika mipango,nidhamu,ubunifu na kufanya kazi kwa bidii hata ikulu kukiwa kuna jiwe utatusua. Wakati tukiendelea kupigania misingi iliyo imara na yenye kumwezesha mwananchi kufanya shughuli zake katika ustawi mzuri kwa maana ya kuhakikisha utawala wa nchi unawanufaisha wananchi lazima uhakikishe utawala wako mwenyewe unafanya kazi kwa kadri na kiwango kinachotakikana.

Tuesday, February 21, 2017

Taarifa Kuhusu Mchezaji Emmanuel Adebayor Kuja Kucheza Yanga ya Tanzania Hii Hapa



Jana January 25 2017 moja kati ya taarifa zilizokuwa zimeenea katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Togo aliyewahi kucheza Arsenal, Man City, Tottenham Hotspurs na Crystal Palace  Emmanuel Adebayor kuripotiwa kujiunga na  timu ya Yanga.

Habari kutoka soka25east.com na mitandao mingine mitatu ya Kenya zilisema kuwa staa huyo atajiunga na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga ambayo pia inachezewa na Vincent Bossou anayechezea timu moja ya taifa na Adebayor na walikuwa pamoja AFCON juzi.

Saa 24 baada ya taarifa hizo kupita mitandao ya Skysports na BBC SPORTS imeripoti na kumnukuu Adebayor kuhusu mpango wake wa sasa katika soka akiwa mchezaji huru, anasema bado ana mpango wa kurejea ligi kuu England na hajaizungumzia Yanga hata tone, hiyo imedhihirisha kuwa tetesi za kujiunga na Yanga sio za kweli.

Nimepokea ofa chache kutoka timu za ligi kuu England na wote mnajua napenda kucheza England, licha ya kuwa mimi sio moja kati ya wachezaji wanaopendwa England nimecheza England kwa miaka kumi, ieleweke pia sikuja AFCON kucheza ili nipate timu nilikuja kuwakilisha taifa langu

Hizi Ndizo klabu Tajiri Zaidi Afrika,Simba ,Yanga na Azam Hazisomeki....!!!




KATIKA miaka ya hivi karibuni mchezo wa soka umekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa nchi zilizopiga hatua zikiwamo zile za barani Ulaya.

Kwa Afrika ambako nchi nyingi ni masikini, soka limekuwa kimbilio la vijana wengi ambao kwao ndicho chanzo kikubwa cha ajira.

Wachezaji, makocha, wauguzi na wafanyakazi wengine wa klabu wamekuwa wakifaidika na utajiri mkubwa unaozalishwa kupitia mchezo huo.

Lakini pia, Serikali kupitia mamlaka za mapato, imekuwa ikinufaika na fedha za kodi zitokanazo na mchezo wa soka.

Pia, klabu zimekuwa zikiingiza fedha nyingi kutokana na mapato ya uwanjani, mauzo ya wachezaji wakiwamo makinda wanaozalishwa katika ‘academy’ zao na hata dili za matangazo.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka jana ya Jarida la Forbes la Marekani, zifuatazo ni klabu ambazo mpaka sasa zimeshavuna fedha nyingi kutokana na biashara ya soka.

Al Ahly (Misri)

Ndiyo timu tajiri zaidi barani Afrika kwa sasa ikiwa na thamani ya euro milioni 19,25. Klabu hiyo ndiyo inayoongoza kwa kuwa na mataji mengi barani Afrika (132).

Lakini pia, inaongoza kwa kutwaa mara nyingi lile Kombe la Klabu Bingwa Afrika ikiwa imefanya hivyo mara nane.

Miaka miwili iliyopita, thamani ya Al Ahly ilikuwa mara mbili ya ile ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Esperance (Tunisia)

Utajiri wao unafikia euro milioni 12,75 na wanamiliki mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hiyo iliyoanzishwa miaka 98 iliyopita, ina heshima kubwa Tunisia ambapo imeshinda makombe 26 ya ligi kuu nchini humo.

Club Africain (Tunisia)

Huenda si mara nyingi umekuwa ukiisikia kwenye mazungumzo ya kila siku, lakini ni moja ya klabu zenye heshima kubwa Tunisia na barani Afrika kwa ujumla.

Wakali hao wanamiliki mataji 13 ya Ligi Kuu Tunisia na utajiri wao unatajwa kuwa ni euro milioni 11, 80.

Mbali na soka, ‘vibopa’ hao wa jijini Tunis, wanamiliki timu za michezo mbalimbali ikiwamo ya mpira wa kikapu.

Uwanja wao wa nyumbani unaoitwa Stade Olympique de Rades, una uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000.

Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)

Mamelodi ndiyo mabingwa watetezi wa mbio za kufukuzia taji la ya Mabingwa Afrika mwaka huu.

Walipochukua mwaka jana, ulikuwa ubingwa wao wa kwanza katika historia ya klabu na michuano hiyo.

Mwaka 2001 walikaribia kulitoa mkononi lakini walipochapwa mabao 4–1 na Al Ahly katika mchezo wa fainali. Mamelodi inaongoza kwa kuwa na makombe mengi katika historia ya soka la Afrika Kusini.

Forbes linaitambua klabu hiyo kuwa na utajiri wa euro milioni 10.35.

Kaizer Chiefs (Afrika Kusini)

Kama ilivyo Mamelodi, Chiefs nayo ni miongoni mwa klabu zinazoogelea kwenye dimbwi la utajiri kutokana na biashara ya soka.

Takwimu za kiuchumi za Forbes linaitaja timu hiyo kumiliki utajiri wa euro milioni 10, 48.

Ujenzi wa Uwanja wa Amakhosi unaoingiza mashabiki 55,000 unaomilikiwa na klabu hiyo uligharimu pauni milioni 105.

Mchezo ambao Chiefs huutolea macho zaidi ni ule unaowakutanisha na mahasimu wao wakubwa Orlando Pirates.

Zamalek SC (Misri)

Ilipoanzishwa mwaka 1911, ilifahamika kwa jina la Qasr El-Neel na haikuwa na utajiri iliyonao leo wa euro milioni 10,30.

Mbali na mataji mengine, imeshinda mara tano lile la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Miongoni mwa mastaa wakubwa waliowahi kutamba na timu hiyo ni pamoja na Hassan Shehata, Hossam Hassan, Junior Agogo na Amr Zaki.

Klabu nyingine tajiri

USM Alger (euro milioni 9.65), E.S Setif (euro milioni 8.6), Raja Casablanca (euro milioni 8.13), na T.P. Mazembe (euro milion

Hana Hamu ya Kufanya Mapenzi na Mimi..Naomba Ushauri




Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30, nina mpenzi wangu wa muda mrefu toka 2014 japo mapenzi yetu yamekuwa hayana muendelezo muzuri kutokana na tabia za huyu mwenzangu. Tulianza mahusiano yetu vizuri sana baadae mwenzangu alibadilika ghafla, nikaja kugundua alikuwa na mahusiano na wanaume wengine (zaidi ya mmoja) tukawa tumepotezana kwa mda kidogo coz alikuwa hapokei simu wala kujib text zangu alafu akawa ni mtu wa kusafiri sana kumbe alikuwa anasafiri na hao mabwana zake, siku nimekutana nae nilimuona na dalili za mimba roho iliniuma sana, mwanzoni alidanganya baadae akakubali akawa ametoa hiyo mimba akaomaba nimsamehe kwa sababu nampenda sana tena sana nikawa nmemsamehe. 

Tukawa pamoja kwa mda mfupi baadae alianza tabia yake ya kuruka ruka na starehe kwa sana, niliamua kumuacha japo roho ilikuwa inaniuma alafu yeye hata hajali kila kitu kwake poa tu. Baadae alirudi akaanza kunitafuta akaomba msamaha kama kawaida yake, kupenda ni hatari sana jamani nilimsamehe tukaanza kuwa pamoja, alikaa kwangu kwa muda wa week, nikaanza michakato kwenda kutoa posa na mahari kwao.

Sasa alivyorudi nyumbani kwao akaanza tena unaweza mpgia simu anakuambia sipo nyumbani nipo kwa dada angu fulani, au kwa bibi nitarudi kesho, au nipo hospitali bibi anaumwa baadae simu inapotea hewani hata siku mbili akipatika anakuambia huku kijijini simu ilizima charge. Sasa kilichonichosha zaidi sasahivi hana hata hamu ya mapenzi kabisa tofauti na navyomjua mimi, huyu mpenzi wangu hapo awali alikuwa akiniona tu hutumii nguvu nyingi kumuandaa, lakini sasa hivi hata ukifanyeje hawezi kuwa tiyari hadi umpake mafuta kidogo. na unaweza kumuomba hata mwezi nzima anakuambia sijisikii, sina hamu.

Naomba ushauri wadau, nifanje ili aweze thamini hisia zangu, au hata kama nikimuacha nifanyeje coz nampenda sana huyu dada natamani awe mke wangu wa ndoa, kuna vitu huwa vinanifanya nimpende sana ni rafiki, mnataniana na kucheka, mpole ila sasa ndo hayo mambo yake, nilishajaribu kumuacha nashindwa nafuta namba kila kitu ila akinipigia tu au nikumuona tu nabadilisha mawazo

Fahamu Mambo Yanayowachizisha Wanawake...!


HAKUNA aliyeaibika wakati akijaribu kufanya jambo kwa faida yake. Siku zote kufanya jaribio ni mwanzo wa kuelekea kwenye ufanisi mzuri wa jambo husika.

Rafiki zangu, ni vema nawe ukajiwekea utaratibu wa kujaribu kufanya mambo ambayo unadhani huyawezi, lakini yakileta matokeo chanya yatakuwa na faida kubwa kwako.

Kujaribu kupo katika mambo mengine mengi ya kawaida – ya kibinadamu. Katika mambo mbalimbali ya kila siku. Ukianza na kupata matokeo mazuri, unakuwa mshindi na bila shaka unakuwa umefanikiwa.

Hali ni tofauti katika suala la mapenzi, huku hakuna kujaribu – ni kuamua tu! Hata hivyo, wakati unaamua mambo yako yanayohusu mapenzi ni lazima kichwani mwako utambue kuwa unafanya kitu kwa ajili yako na mtu mwingine (mpenzi wako).

Hapo ndipo kazi inapokuja. Kwa maneno mengine, wakati ukijifikiria wewe katika ulimwengu wa mapenzi, unatakiwa pia kumfikiria mpenzi wako.

Kwa bahati mbaya, katika eneo hili, wanaume wengi huwa hawafikirii sana namna ya kuwafurahisha wenzi wao. Wanahisi ni suala linalowahusu wanawake pekee. Ni kosa.

Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hapa katika Love Moment, nimekuandalia mambo ambayo wanawake wengi wanavutiwa zaidi kutoka kwa wanaume.

Je, wewe ukoje? Una sifa hizo? Hebu twende pamoja katika mada hii ambayo bila shaka itakutoa matongotongo.

USAFI BINAFSI

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au ua la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.

Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.

Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

KUJIAMINI

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika.

Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya. Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.

Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.

Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!

KUJITETEA

Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.

Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.

Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!

Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.

Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.

KUJALI

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.

Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

UKARIBU

Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.

Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.

Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa

Powered by Blogger.