Monday, January 18, 2016

Matokeo Ya Kidato Cha Pili Yaingia Dosari......Wamiliki Wa Shule na Vyuo Wataka Mfumo wa GPA Ufutwe


WAMILIKI wa Shule na Vyuo Visivyo vya Serikali wameiomba Serikali kufuta mfumo wa GPA unaotumiwa na Baraza la Mitihani (Necta) kupanga madaraja ya mitihani ya sekondari, kwa maelezo kuwa haufai kwa kuwa unahalalisha watahiniwa waliofeli waonekane wamefaulu.
Akizungumza jana Dar es Salaam kuhusu matokeo ya kidato cha pili ambayo yametangazwa na Necta hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (TAMONGSCO), Benjamin Nkonya alisema matokeo hayo hayaeleweki kwani wameshuhudia baadhi ya wanafunzi wanaoonekana kufanya vizuri chini ya mfumo wa GPA wakati katika mfumo wa madaraja (division) wanaonekana wamefanya vibaya.
Kwa hali hiyo, Nkonya amemwomba Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kufuta mfumo huo hadi pale Necta itakapokuwa tayari kujibu maswali kadhaa ya wadau wa elimu ambao wanaona mfumo huo hauna tija katika kuboresha elimu.
Baadhi ya hoja ambazo zilihojiwa na Nkonya ni kwamba kulikuwa na kasoro gani katika mfumo wa madaraja mpaka ukaja huo wa GPA na akataka kujua ni nani alilalamikia mfumo wa division mpaka ukaondolewa? Alihoji kabla ya mfumo huo kuletwa, ni wadau wapi walishirikishwa?
Alisema TAMONGSCO ilipata taarifa za kuwepo kwa mfumo huo wa GPA kupitia vyombo vya habari na hawakushiriki katika ngazi yoyote ya mijadala ya kisera kama sheria inavyoelekeza. 
Katibu Mkuu huyo wa TAMONGSCO alihoji, “Je, alama za chini za gredi D, C,B na A zilibaki kama zilivyokuwa wakati wa mfumo wa division au kuongeza gredi E na B+ ilikuwa mbinu ya kushusha alama za ufaulu na matumizi ya GPA yakaanzishwa kwa lengo la kuficha ukweli kuwa viwango vimeshushwa kwa kiasi kikubwa??
Nkonya pia alihoji mfumo huo una faida zipi na unasaidiaje katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaomaliza wanakuwa na ujuzi stahiki utakaowawezesha kuhimili changamoto za soko la ajira na utandawazi?
“Kwa hali hii bado tunaishauri Serikali isitishe matumizi ya mfumo wa GPA hadi pale hoja zetu zitakapopatiwa ufumbuzi,”alisema Nkonya.

Thursday, January 14, 2016

Raia wa Kigeni 15 katika mgodi wa Tanzanite One wafukuzwa nchin

Kaimu Katibu Mkuu mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto (aliyesimama) akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha ambazo zinashirikiana na Wizara ya Nishati na Madini katika kudhibiti utoroshaji madini ya Tanzanite nje ya nchi. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hizo, Amos Makala. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa pili kulia)na wa Tatu kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje



Mwenyekiti wa Kikosi kazi kinachoshughulikia udhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi, Muliro Muliro (aliyesimama) ambaye pia ni Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, akitoa taarifa ya Kikosi Kazi hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, Amos Makala (wa kwanza kulia) wakati wa kikao cha Kamati hizo kilichofanyika jijini Arusha.Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa pili kulia) na wa Tatu kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha wakiwa katika kikao cha Kamati hizo kilichofanyika katika kituo cha Jimolojia mkoani Arusha. Kamati hizo zinashirikiana na Wizara ya Nishati na Madini katika kudhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi na ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni zinazoshughulika na biashara ya madini nchini.


Thursday, January 7, 2016

WAZIRI MKUU ATOA ONYO KALI KWA MADAKTARI WANAO TOA MIMBA WANAWAKE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Josephine John* ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Januari5, 2016.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa ya Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake na wanafunzi kuacha tabia mara moja,lasivyo* atawafukuza kazi na kuwafunga jela.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.

Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.



Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama.

"Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua kali.

Pia, alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akimsalimia mtoto Flora Mapunda (1) ambaye amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo* Waziri Mkuu aliitembelea na* kuzungumza na watumishi* akiwa ktika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.

Rais Magufuli Akutana Na Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa na Waziri mkuu mstaafu warioba



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam January 7,2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa, Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam January 7,2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzo January 7,2016



Monday, January 4, 2016

CUF: Hatutoshiriki sherehe za Mapinduzi


VIONGOZI wakuu wa Chama cha Wananchi (CUF) hawatashiriki shughuli za kiserikali zilizopangwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kutokana na serikali iliyopo kutokuwa na ridhaa ya Wazanzibari. aarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano na Umma ya chama hicho imesema hatua hiyo inatekelezwa katika kuzuia raslimali za wananchi kutumika vibaya ikiwemo kuendekeza uongozi wa serikali usiohalalika kisheria na kikatiba.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari, hata Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF na mwanasiasa aliyegombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, ambao ulihujumiwa kwa makusudi, hatahudhuria sherehe hizo zitakazofikia kilele Januari 12, kwenye Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.

Taarifa imesema chama hicho kimekuwa kikishiriki sherehe za Mapinduzi tangu kilipoanzishwa kwa kuwa kinatambua umuhimu wa siku hiyo ambayo ilikuwa ndio imeipatia Zanzibar jamhuri chini ya kiongozi wake wa kwanza, Mzee Abeid Amani Karume.

Lakini, taarifa imeeleza, malengo ya Mapinduzi hayo yalikuwa ni pamoja na Zanzibar kupata uongozi wenye ridhaa ya wananchi, na sio kama ilivyo sasa serikali kuwa iliyojiweka baada ya maamuzi ya wananchi kuhujumiwa.

Kuhusu asili ya Mapinduzi, imeelezwa kuwa CUF inatambua Mapinduzi ya 12 Januari, 1964 yanahusu Wazanzibari wote na malengo yake makuu kuelezwa na kufafanuliwa vyema kupitia Dikrii Na. 6 ya mwaka 1964 iliyopitishwa na Baraza la Mapinduzi.

Katika Dikrii hiyo, malengo yanatajwa kwamba ni kuleta usawa, umoja na maridhiano baina ya Wazanzibari wote na kupiga vita aina zote za ubaguzi.

Taarifa imesema kwa kuwa tayari umma wa Wazanzibari umetangaziwa kwamba kuanzia Januari 2 kutakuwa na s hughuli mbalimbali zinazolenga maadhimishio ya Mapinduzi na hatimaye kama ilivyo desturi, kilele chake kufikiwa Januari 12, 2016 kwenye Uwanja wa Amaan, “viongozi wa CUF hawatoshiriki ratiba walizopangiwa mpaka pale chaguo la wananchi wa Zanzibar walilolifanya tarehe 25 Oktoba, 2015 litakapoheshimiwa.”

CUF inasikitisha sherehe za mara hii zinafanyika wakati nchi na watu wake wema wapo katika mtihani mkubwa kufuatia kitendo cha mtu mmoja, Jecha Salim Jecha, kuamua kwa utashi wake na waliomtuma, kuiingiza nchi katika msukosuko na taharuki kwa kudai eti ameufuta uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake.

“… Amevunja Katiba, amevunja Sheria ya Uchaguzi na amevunja hata maadili ya kazi yake, (hivyo) mara hii nchi yetu itaadhimisha Mapinduzi huku Serikali ikiwa inaongozwa na viongozi wasiokuwa na uhalali na ridhaa ya wananchi,” imesema taarifa ya CUF iliyosainiwa na Mansour Yussuf Himid, Mshauri wa Katibu Mkuu wa chama.

Taarifa imesema kwamba ni msimamo wa CUF tangu hapo kuwa hakikubaliani na uamuzi huo wa mtu mmoja kujinyakulia mamlaka ya wananchi wa Zanzibar yaliyowekwa kikatiba, na kwa msingi huohuo, “tunapenda kutumia fursa hii kuwaeleza wananchi wa Zanzibar kwamba viongozi wetu hawatoshiriki katika shughuli walizopangiwa katika ratiba ya sherehe hizi.”

Chama kimetoa sababu nne za kufikia uamuzi huo wa viongozi wake kutoshiriki sherehe za mwaka 2016. Sababu hizo ni zifuatazo:

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 (Toleo la 2010), Ibara ya 28, Ibara ya 42(2), Ibara ya 48(b), Ibara ya 90(1) na Ibara ya 92(1) Serikali iliyokuwepo madarakani na Baraza la Wawakilishi lililokuwepo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 – 2015) vilimaliza muda wake wa uongozi tarehe 2 Novemba, 2015 kwa upande wa Serikali na tarehe 12 Novemba, 2015 kwa upande wa Baraza la Wawakilishi. Kwa sasa, hatuna viongozi wenye uhalali wa kikatiba kuweza kutekeleza majukumu ya kiserikali. Kwa hivyo, kushiriki katika ratiba hizo kwa kutumia nafasi ambazo hazina uhalali tena wa kikatiba ni kwenda kinyume na dhamira ya waasisi wa Mapinduzi, jambo ambalo hatuko tayari kulifanya.

Kiutaratibu, kilele cha sherehe huongozwa na Rais ambaye yupo kikatiba. Kwa mara ya kwanza tokea tarehe 12 Januari 1964, sherehe za miaka 52 zitaongozwa na Rais ambaye ameshamaliza muda wake wa uongozi kikatiba na ambaye hana uhalali na ridhaa ya wananchi wa Zanzibar. Kushiriki katika sherehe hizo ni kuhalalisha kipindi cha uongozi ambacho hakipo tena kikatiba. Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wenziwe ndani ya Chama waliokuweko Serikalini hadi tarehe 2 Novemba, 2015 hawako tayari kuhalalisha uvunjaji wa Katiba ya Zanzibar ambayo ndiyo sheria kuu ya nchi.

Viongozi wa CUF wakiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad wanaamini katika msingi mkuu wa Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964 chini ya uongozi wa Baba wa Taifa la Zanzibar, Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, ambao ni kuleta utawala wenye ridhaa ya wananchi walio wengi. Msingi huo umewekwa wazi na kutiliwa nguvu na Katiba ya Zanzibar ya 1984 (Toleo la 2010) kupitia Ibara ya 9(2)(a) ambapo inaelezwa kwamba, “Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa wananchi wenyewe.” Mamlaka hayo ya wananchi yalitekelezwa tarehe 25 Oktoba, 2015 kwa kuwachagua viongozi watakaoongoza Serikali yao kwa miaka mitano ijayo. Kitendo chochote cha kupindua mamlaka hayo ya wananchi ni kwenda kinyume na misingi ya Mapinduzi na misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa la Zanzibar, Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume. CUF hatuko tayari kushiriki katika kuisaliti misingi hiyo na kuisaliti dhamira ya Mzee Karume.

Sherehe za kuadhimisha Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964 zina lengo la kukumbuka malengo ya Mapinduzi hayo na dhamira ya waasisi wake wakiongozwa na Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika kusimamia utawala wenye ridhaa ya wananchi walio wengi. Kuzitumia sherehe za Mapinduzi kuhalalisha utawala usio na ridhaa ya wananchi wa Zanzibar na ambao haupo kikatiba ni usaliti mkubwa wa dhamira ya kuwepo kumbukumbu hiyo. CUF hatuko tayari kuwa sehemu ya usaliti huo.

CUF inafanya uamuzi huo wakati mgombea wake anayepigania haki ya kukabidhiwa mamlaka kutokana na ushindi alioupata, Maalim Seif, amekuwa akikutana kwa faragha na viongozi wa kitaifa wa Zanzibar akiwemo Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye anashikilia uongozi wa serikali inayopingwa uhalali wake.

Viongozi wengine wanaokutana ni marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour Juma na Dk. Amani Abeid Karume, pamoja na Balozi Seif Ali Iddi.

Pamoja na vikao hivyo vilivyofikia tisa, hakuna taarifa inayotolewa kwa umma na haijulikani ni lini vitakwisha. Hivi karibuni, Dk. Shein alipokuwa akieleza mazungumzo yake na Rais Dk. John Magufuli wa Tanzania, alisema mazungumzo yatakapomalizika umma utajulishwa matokeo.

Oktoba 28, Jecha alitangaza kufuta uchaguzi mzima kwa madai ya kuwepo matatizo yaliyoutia doa, wakati huo akiwa ameshatangaza zaidi ya asilimia 70 ya kura za urais ikiwa ni majimbo 33 kati ya 54.

Viongozi wa CCM wamekuwa wakishikilia kuwa kutafanyika uchaguzi wa marudio, wakirejea tamko la Jecha alipotangaza kufuta uchaguzi. Tume ya Uchaguzi Zanzibar haijatangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio huku kipindi cha siku 90 kilichotajwa kikiwa kinamalizika.

CCM yamjia juu Lowassa

Lowassa alikaririwa na vyombo vya habari kutoka Monduli akisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa maelekezo ya Serikali imekuwa ikiwatoza kodi kubwa wafanyabiashara kwa sababu waliifadhili Chadema kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.

CCM imesema kauli ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa wafadhili wa Chadema wananyanyaswa, ina lengo la kuichonganisha Serikali na walipa kodi na kumtaka ataje waliofanyiwa vitendo hivyo.




Juzi, Lowassa alikaririwa na vyombo vya habari kutoka Monduli akisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa maelekezo ya Serikali imekuwa ikiwatoza kodi kubwa wafanyabiashara kwa sababu waliifadhili Chadema kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.

Lowassa aliwahi kutoa kauli kama hiyo jijini Mwanza akiwa kwenye msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema wa mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo aliyeuawa kwa kushambuliwa kwa mapanga.Pia wakati wa harambee ya Chadema iliyofanywa Septemba 22 mwaka jana, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema kulikuwa na matajiri watano wenye uwezo kiuchumi ambao walikuwa tayari kukisaidia kwenye shughuli zake za kampeni, lakini hawataki kutajwa majina yao kwa hofu ya kufuatiliwa na vyombo vya dola.

Jana, akizungumza na waandishi wa habari jijini, Abdallah Bulembo, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, alisema kauli ya Lowassa haina ukweli wowote na kwamba ina lengo la kuigombanisha Serikali na walipakodi ambao wanahitajika sana kipindi hiki.

“Kama kweli Lowassa anawafahamu wafanyabiashara au kampuni ambazo zinatozwa kodi kubwa kwa sababu walikuwa wamekifadhili chama hicho, basi ni vizuri awataje ili wajulikane na waseme wao wenyewe,” alisema Bulembo ambaye wakati wa kampeni alikuwa bega kwa bega na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.

Akijibu suala hilo, Lowassa alisema kuna wafanyabiashara wengi waliokuwa wakikifadhili chama ambao wanalalamika kutozwa kodi kubwa.“Kuna watu wengi wanalia kutozwa kodi kubwa,” alisema Lowassa ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema baada ya kuihama CCM Julai mwaka jana.

“Suala hapa si kuwataja majina, mkihitaji majina yao fanyeni research (utafiti) mtawapata. Lakini mfahamu kwamba kuna tatizo hilo.”Alisema ana uhakika vyombo vya habari vitawapata watu hao na kwa kuwa ni wengi watatoa malalamiko yao.

Akifafanua zaidi, Bulembo alisema kauli ya Lowassa inadhoofisha nguvu ya Rais Magufuli ambaye ameongeza makusanyo ya kodi kutoka Sh850 alipoingia madarakani hadi Sh1.3 trilioni kwa mwezi.“Tunawahitaji walipakodi wengi wakati huu kwani tunahitaji kupata fedha zaidi ili kutekeleza ahadi tulizowaahidi wananchi. Kauli ya Lowassa inatugombanisha na walipakodi,” alisema.

Alisema anachofahamu ni kwamba kodi inatozwa bila kumpendelea mfadhili wa CCM au kumwonea mfadhili wa Chadema.“Masuala ya vyama ya siasa yameshapita, sasa hivi ni kujenga nchi na kodi inatozwa bila kuangalia vyama vya siasa,” alisema Bulembo.Alimwomba Lowassa kumsaidia Magufuli katika kazi ya kutafuta mapato ili kuwaletea wananchi maisha mazuri

“Namwomba Lowassa tujenge nchi yetu, huu si wakati wa kufanya siasa, asubiri mwaka 2020 kama atagombea tena urais tutakutana kwenye majukwaa,” alisema.Alisema kuendelea kupigana vijembe kipindi hiki ni kurudisha nyuma maendeleo ambayo yanahitaji zaidi walipakodi.

“Kodi zina vipimo vyake kama kuna watu wameonewa ukweli utajulikana,” alisema Bulembo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alisema Serikali ya CCM itaendelea kutenda haki kwa wananchi wake ili kukiwezesha chama hicho kushinda uchaguzi kwa kishindo mwaka 2020.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo, mkurugenzi wa idara ya elimu na huduma kwa walipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo haijapata malalamiko yoyote.Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na haifanyi kazi kwa kufuata maagizo ya vyama vya siasa.

“Sisi hatuko kwenye siasa tunafanya kazi zetu kwa kuongozwa na sheria na kanuni. Hatumwonei mtu wala kupendelea,” alisema.Kauli kama ya Lowassa ilitolewa pia na mkuu wa idara ya habari ya Chadema, Tumaini Makene aliyesema hoja ni kueleza kuwapo kwa tatizo ambalo halitaishia kwenye ubaguzi wa kiitikadi.

“Ukianza kubagua watu kivyama, huwezi kuishia hapo. Utaanza kuwabagua kikabila, kikanda na hata kidini. Hii ni kinyume na ahadi ya Rais Magufuli kuwa atakuwa Rais wa watu wote,” alisema Makene.Makene alitoa mfano wa kukataliwa kwa misaada ya vifaatiba katika zahanati za Serikali mkoani Kagera uliotolewa na mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare.

Mara baada ya kuingia Ikulu, Rais Magufuli alikutana na watumishi wa Hazina na kuwaelekeza kukusanya kodi bila ya kuangalia sura, huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifanya ziara za mara kwa mara bandarini ambako ameibua kashfa za ukwepaji kodi na upitishaji makontena kifisadi

TANESCO WAWAOMBA RADHI WATEJA WA KANDA YA KASKAZINI MASHARIK

KUOMBA RADHI WATEJA WA KANDA YA KASKAZINI MASHARIKI WANAOPITIWA NA GRIDI YA TAIFA.


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawaomba radhi wateja wake wanaopitiwa na Gridiya Taifa wa maeneo ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma, Iringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Geita, Simiyu na Mara kwa kukosa umeme leo Januari 04, 2016 majiraya 10:54 alfajiri.

Kukosekana huku kwa Umeme kunatokana na hitilafu ya ghafla kwenye njia ya msongo mkubwa wa Kilovoti 32 kutoka Same hadi Hale ambayo ilisababisha njia ya Kaskazini – Mashariki Kutoka kwenye gridi yaTaifa.

Mafundi wapo eneo la tukio toka alfajiri wanaendelea kutatua tatizo hili. Tutawajulisha mara matengenezo yatakapokamilika na Umeme kureje akatika hali ya kawaida.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.


Imetolewana:
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.

Sunday, January 3, 2016

BALOZI SEFUE AONGOZA SEMINA ELEKEZI YA SIKU MOJA KWA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU



Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo January 2, 2015




Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam




mada katika semina elekezi hiyo wakiwa ni pamoja na (toka kulia) Makatibu Wakuu Kiongozi wastaafu Balozi Dkt. Marten Lumbanga, Balozi Charles SangaKatibu Mkuu Mstaafu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad na wengineo

Mchungaji Rwakatare Aivimbia Serekali

Baada ya nyumba yake kuwekewa alama ya kutakiwa kubomolewa muda wowote kuanzia Januari 6, Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God, Dk Getrude Rwakatare ameitaka Serikali itii uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuzuia ubomoaji.

Mwishoni mwa mwaka jana, Serikali ilianza ubomoaji wa nyumba zote zilizojengwa mabondeni, kama Bonde la Mto Msimbazi, kingo za mito, fukwe za bahari, pia maeneo ya wazi na hifadhi za barabara, kabla haijasitisha mchakato huo Desemba 22 na kutoa siku 14 zitakazoisha Januari 5 kwa wamiliki wenyewe kuzibomoa ili kuokoa mali na baadhi ya vifaa muhimu.
Powered by Blogger.