Thursday, January 7, 2016

WAZIRI MKUU ATOA ONYO KALI KWA MADAKTARI WANAO TOA MIMBA WANAWAKE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Josephine John* ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Januari5, 2016.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa ya Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake na wanafunzi kuacha tabia mara moja,lasivyo* atawafukuza kazi na kuwafunga jela.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.

Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.



Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama.

"Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua kali.

Pia, alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akimsalimia mtoto Flora Mapunda (1) ambaye amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo* Waziri Mkuu aliitembelea na* kuzungumza na watumishi* akiwa ktika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.