Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha amemvua wadhifa wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sinamila, Mashaka Lusotola na kumrudisha kuwa mwalimu wa kawaida.
Hatua hiyo ilikuja baada Mwenegoha kubaini kuwa walimu wa shule hiyo wamekuwa na tabia ya kuwaagiza kuku, wazazi wanaowaandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza.
Mwenegoha alichukua maamuzi hayo, baada ya kuthibitisha kuwa mwalimu huyo mkuu, ameshindwa kudhiti tabia hiyo ya walimu walio chini yake.
Akizungumzia kusimamishwa kwake, Mwalimu Lusotola alisema amefurahi na kufananisha adhabu hiyo na kumpiga teke chura.
Tayari mwalimu huyo amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamaba na Rushwa (Takukuru), leo anatarajia kwenda kuandikisha maelezo, huku akisisitiza kuwa hajaomba kitu chochote kwa wazazi.
Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment