Thursday, February 18, 2016

Uteuzi wa Kamanda Maalumu wa Polisi Kikosi cha Bandari waja kukomesha majipu Bandari

Jeshi la Polisi Tanzania wakati wowote kuanzia sasa linaweza kumteua Kamanda Maalumu wa Polisi Kikosi cha Bandari, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kulitaka Jeshi la Polisi nchini kulinda Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).Mapema wiki hii, Rais 


John Magufuli aliagiza Jeshi la Polisi kurejesha huduma za ulinzi katika bandari hiyo ambayo ilikuwa ikilindwa na Polisi Maalumu wa Bandari.
Akizungumza jana , Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu alisema tayari askari wake wapo bandarini wanalinda maeneo yote muhiumu.Kuhusu hatma ya askari waliokuwa wakilinda bandari hiyo ambao ni Polisi Maalum wa TPA, IGP Mangu alisema watafanya nao kazi kwa pamoja kwani hata sheria iliyounda Jeshi la Polisi linawatambua ‘Auxiliary Police’ kuwa ni sehemu ya Jeshi hilo.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.