Saturday, December 5, 2015

SIKU 30 ZA RAIS MAGUFULI KUWA MADARAKANI ZAOKOA TRILION 1 !!!!!



Rais John Magufuli leo ametimiza mwezi mmoja tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo huku akiweka rekodi ya kuokoa kiasi cha Sh997.4 bilioni (karibu Sh 1trilioni) ambazo zilikuwa zitumike kwa matumuzi yasiyo ya lazima, na ukwepaji kodi.
Sh997.4 bilioni zilizookolewa zitaweza kutumika kununua magari ya wagonjwa, kujenga zahanati, kujenga barabara za lami, kununua madawati, kujenga vyumba vya madarasa, kuchimba visima, kununua mashine za uchunguzi wa magonjwa, magari ya wanafunzi, pikipiki kwa maofisa kilimo, mikopo ya elimu ya juu au kujenga viwanja vya michezo kadri Serikali itakavyoelekeza.
Dk Magufuli aliapishwa Novemba 5 katika hafla iliyofana na alianza kazi ya kutafuta na kuziba mianya ya upotevu wa fedha Novemba 6 alipotembelea Hazina. Katika mazungumzo ya watendaji wa wizara hiyo Rais Magufuli alipiga marufuku safari zote za nje na kwamba zitakuwa zinaruhusiwa kwa kibali maalumu.
Novemba 7 alitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako aliagiza mashine za MRI na CT-Scan zitengenezwe na aliagiza Sh3 bilioni zitolewe kugharimia matengenezo kati ya Sh7 bilioni zilizokuwa zinahitajika.
Novemba 19, Dk Magufuli aliwasilisha bungeni jina la Kassim Majaliwa, mbunge wa Ruangwa kwamba ndiye alimpendekeza kuwa Waziri Mkuu. Baada ya jina kupitishwa na Bunge, Novemba 20 Kassim Majaliwa aliapishwa.
Jioni alilihutubia Bunge akionyesha mwelekeo wa Serikali yake ya awamu ya tano. Katika hotuba hiyo iliyowasisimua wabunge na hata wananchi waliosikiliza kupitia televisheni na redio, Dk Magufuli aliahidi kupambana na mafisadi, kubana matumizi, kuhimiza utendaji kazi, kuinua uchumi na kulinda amani na utulivu.
Baada ya hapo Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa wamekuwa wakitembelea maeneo muhimu kwa uchumi wa nchi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bandari na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
Utendaji huo wa Serikali wa Magufuli ndani ya mwezi moja na kipindi kabla hajaunda baraza la mawaziri, umetazamwa na jamii kuwa ni mbinu ya kusafisha nchi na kutengeneza mazira safi ili mawaziri watakaoteuliwa wafuate kasi hiyo.
Fedha zilizookolewa
Kwa kuzingatia ripoti ya matumizi ya fedha za safari zilizolipwa kama nauli na posho kwa kipindi cha kati ya mwaka 2013 na 2015 kiasi hicho ni pamoja na Sh356.3 ambazo zingeweza kutumika kwa safari hizo. Dk Magufuli aliagiza kwamba baadhi ya shughuli zitafanywa na mabalozi wa Tanzania walioko nje.
Novemba 19 alipozindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma, Dk Magufuli aliagiza Sh225 milioni zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili ya hafla ya wabunge, zipelekwe kununua vitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Fedha hizo zilinunua vitanda 300, magodoro 300, mablanketi 1675, na viti vya magurudumu 30.
Pia, katika hotuba yake bungeni, Dk Magufuli alirejea uamuzi wake wa kufuta safari za nje kwa watendaji wa Serikali na kueleza safari hizo zimeigharimu Serikali Sh356.3bilioni ambazo zingeweza kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 400.
Novemba 23, Dk Magufuli alitangaza kufutwa kwa maadhimisho ya Siku ya Uhuru Desemba 9 na akaagiza Sh4 bilioni ambazo zingetumika zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Morocco kwenda Mwenge. Kazi hiyo imeanza.
Novemba 25, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitangaza kufutwa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani na akaelekeza kwamba fedha zilizopangwa kwa ajili ya sherehe hizo zitumike kununua dawa za kufubaza makali ya ukimwi (ARVs).
Novemba 27, Waziri Mkuu Majaliwa alitembelea bandarini na kubaini makontena 349 ambayo yalitolewa bandarini bila kulipiwa ushuru na kuifanya Serikali kukosa mapato ya Sh80 bilioni.
Tayari wenye makontena hayo wameanza kulipia na jana  TRA ilitangaza kukusanya Sh6.3 bilioni kati ya hizo Sh80 bilioni. Katika ziara yake nyingine ya kushtukiza Desemba 3 Majaliwa alibaini makontena 2,431 yalitolewa bila kulipiwa kodi. Ikiwa makontena hayo yangelipiwa kodi viwango sawa na yale 349 Serikali ingepata Sh557.2 bilioni.
Desemba 3, Dk Magufuli alifanya mazungumzo na jumuiya ya wafanyabiashara nchini na akawataka wote ambao waliondoa mizigo yao bandarini bila kulipa kodi, wajitahidi kulipa katika kipindi cha siku saba kuanzia juzi vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Makontena ni shida
Desemba 1, makontena mengine tisa yalikamatwa na TRA eneo la Mbezi, Tangibovu yakiwa yametoroshwa bila kulipuiwa ushuru wa Sh58 milioni. Jumla ya Sh637.2 zimeokolewa kutokana na mkakati wa kukusanya fedha kutoka kwenye makontena 2,431 pamoja na 349 na hayo tisa.
Matumizi ya Sh 997.4 bilioni
Kwa muda mrefu, Serikali imekuwa ikikwama kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kutokana na kukosa fedha. Dk Magufuli alikiri juzi kuwa hakuna fedha za maendeleo zilizokuwa zimetolewa kwa wizara zote katika mwaka huu wa fedha wa 2015/16, lakini baada ya miezi sita juzi ndiyo zimetolewa Sh120 bilioni.
Dk Magufuli hakusema Serikali imepata wapi fedha hizo, lakini huenda ni sehemu ya fedha ambazo ameokoa katika kipindi cha mwezi mmoja.
Kama fedha hizo zingeelekewa katika ujenzi wa barabara, na kwa kuzingatia kilomita moja inajengwa kwa Sh1 bilioni, fedha hizo zitaweza kujenga karibu au zaidi ya kilomita 1,000, ambao ni umbali kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma au Dar es Salaam mpaka Tunduma.
Aidha, Sh997.4 bilioni zingeweza kununua magari 3,325 ya kubebea wagonjwa kwa gharama ya Sh300 milioni kwa kila moja na kuwezesha kila mkoa kupata magari 133 ya aina hiyo.
Pia, zahanati moja yenye vifaa vyote muhimu ujenzi wake unagharimu kati ya Sh600 milioni na Sh700 milioni. Hivyo, fedha hizo zingeweza kujenga zahanati 1,425 yaani kila mkoa ungepata zahanati 57.
Vilevile, wakati maelfu ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wanasoma kwa kukaa chini kutokana na kukosa madawati, Sh997.4 bilioni zitaweza kutengeneza madawati yenye miguu ya chuma 33,249,142 kwa gharama ya Sh30,000 kwa kila moja na kuwezesha kila mkoa kupata madawati 1,329,966.
Pengine, fedha hizo zinaweza kujenga vyumba vya madarasa 132,996 kwa bei ya Sh7.5 milioni kwa darasa moja, hatua ambayo itawezesha kujengwa kwa vyumba vya madarasa 5,319 kila mkoa nchini.
Kipimo maarufu cha CT-Scan ambacho ufanyaji wake wa kazi unasuasa Muhimbili kwa muda mrefu, kinauzwa kwa wastani wa Sh900 milioni, hivyo, Sh997.4 bilioni zitaweza kununua mashine 1,108 ambazo zingesambazwa na kila mkoa ukapata mashine 44.
Gharama za kuchimba kisima kifupi ni kati Sh1 milioni na Sh3 milioni kulingana na jiografia ya eneo husika, hivyo Sh997.4 bilioni zitaweza kuchimba visima 332,491; kila mkoa ukapata visima 13,299.
Pia, kwa kuwa Serikali inahimiza uboreshaji wa sekta ya kilimo, Sh997.4 bilioni zitaweza kununua pikipiki 332,491 na kugawiwa kwa maofisa kilimo kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa kilimo vijijini na kila mkoa ungepata pikipiki 13,299.
Kama fedha hizo zitaelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu, zitaweza kugharamia wanafunzi 249,368 wa mwaka wa kwanza kwa asilimia 100 kwa wastani wa Sh4 milioni kwa kila moja kwa ajili ya chakula, malazi na ada.
Imeandikwa na Fidelis Butahe, Joyce Mmasi na Peter Saramb

ALBINO KUWANIA TAJI LA UREMBO TANZANIA

Watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania wamepata fursa ya kushindania taji la kipekee la urembo, na pia kuhimiza jamii kuthamini utu wao.

MAGUFULI ATUA TFF


KASI ya utendaji ya Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli imehamia katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuzua tafrani.

Wakitekeleza moja ya maagizo mapya ya Magufuli kukusanya kodi kwa ufasaha na kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Ilala wamezuia akaunti ya TFF ili ilipwe kodi za nyuma.

TRA imezuia akaunti zote za TFF ikitaka ilipwe jumla ya shilingi 1,637,334,000 (Sh bilioni 1.6) ikiwa ni kodi kwa kipindi cha mwaka 2010-13, sehemu kubwa ikiwa ni makato kwenye mishahara (PAYE) ya makocha Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Michelsen.

Pia imeelezwa, TRA inataka ilipwe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Brazil uliofanyika mwaka 2010.

Hata hivyo, TFF imesema makocha hao wa timu za taifa wamekuwa wakilipwa mishahara na serikali, hivyo wao hawakuwajibika kuwakata kodi.

Pia shirikisho hilo, limesema katika taarifa yake kwamba, mchezo kati ya Tanzania na Brazil ulisimamiwa na kamati maalum ya serikali na fedha zake hazikuingizwa katika akaunti za TFF.

Kutokana na hali hiyo, TFF imesema ziara ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (U-15) kwenda Rwanda, Uganda na Kenya imekufa na badala yake timu hiyo itacheza mechi za kirafiki Mwanza na Kigoma.







Itacheza na Burundi mjini Kigoma kwani haina fedha za kwenda nje ya nchi kutokana na TRA kuzuia akaunti hizo za TFF. Shughuli nyingine za soka zitakazohathirika ni;

Kulipwa kwa madeni ya usafiri, chakula na posho za wachezaji wa timu za taifa zilizoshiriki mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018 na Kombe la Chalenji, pia program za soka la wanawake na vijana zitasimama.

Ile michuano ya Kombe la FA nayo haitaweza kufanyika katika hatua ya raundi ya pili, Ligi Daraja la Pili nayo itasimama. Imeelezwa kuwa, TFF haitaweza kulipia vifaa vya michezo ikiwemo mipira kwa ajili ya shule za msingi na vituo vya maendeleo vinatarajiwa kuwasili nchini muda wowote.

Pia kuna hatari kutolipwa kwa mishahara ya wafanyakazi wa TFF, kutolipwa kwa gharama za kambi na karo kwa ajili ya vijana wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 13 walioko Shule ya Alliance Academy ya jijini Mwanza.

Oktoba 2012 na TRA ilichukua Sh 157,407,968 iliyokuwa mgawo wa klabu lakini yalipofanyika mazungumzo na Serikali iliamuriwa zirudishwe TFF lakini mpaka sasa shirikisho hilo linazifuatilia.

Tangu alipoingia madarakani mwezi mmoja sasa, Magufuli amekuwa akisisitiza kwamba, ni lazima TRA ikusanye kodi ipasavyo na mamlaka nyingine kama bandari kufanya kazi ipasavyo ili kutoruhusu serikali kukosa mapato yake.

Source;Global

YANGA YASHUSHA STRAIKA MTOGO


MAMBO sasa kimyakimya tu kwani Yanga ipo mbioni kumleta straika hatari kutoka Togo ambaye ataingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza akiwa maalum kwa mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Straika huyo anatarajiwa kutua nchini siku yoyote kuanzia sasa kabla ya dirisha la usajili kufungwa, Desemba 15, mwaka huu ili kumalizana na uongozi wa timu hiyo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa, uamuzi wa kumleta mchezaji huyo umefikiwa hivi karibuni na benchi la ufundi linalotaka kuwa na kikosi hatari kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika.

“Uongozi unafanya siri kubwa, yaani hautaki kabisa watu wajue juu ya hili kwani unahofia dili hilo linaweza kuingiliwa kati na wapinzani wao.







“Lakini ukweli ni kwamba, straika huyo atatua hapa nchini siku yoyote kabla ya dirisha la usajili kufungwa ili aweze kumalizana na uongozi na jinsi inavyoonekana wanataka kufanya mambo kimyakimya.

“Endapo straika huyo atamalizana na uongozi, kuna uwezekano mkubwa Vincent Bossou akafungashiwa virago kwa sababu kiwango chake ni cha kawaida sana na tayari mipango ya kumalizana naye imeshaanza,” kilisema chanzo hicho.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alipotafutwa ili kuzungumzia taarifa hizo, hakuweza kupatikana kwani simu yake iliita bila kupokelewa.

Akiwa katika mipango ya usajili hivi karibuni, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, aliliambia gazeti hili kuwa, watafanya usajili wa siri kwa mchezaji aliyekamilika ili wawe na kikosi bora kwa mechi za Afrika.

Source;Global

UGANDA BINGWA MPYA SECAFA CHALLENGE 2015

The Cranes

Uganda Cranes leo wametwaa taji la CECAFA kwa mara ya 14 baada ya kuifunga Rwanda kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Addis Ababa National Stadium, Ethiopia.

Mshambuliaji wa klabu ya Burly Express Caesar Okhuti aliifungia Uganda goli pekee dakika ya 15 akiunganisha krosi ya Denis Okot.

Uganda wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Rwanda kwenye michezo ya fainali wakiwa wameshinda fainaliwakiwa wameshinda jumla ya mechi tatu za fainali walizokutana na Rwanda.

Mbali na Uganda kuchukua kombe la Challenge mwaka 2015, pia kuna wachezaji ambao wametwaa tuzo binafsi.

Tuzo hizo zimechukuliwa na wachezaji wafuatao;

Mchezaji bora wa mechi hiyo: Muzamiru Mutyaba

Mchezaji bora wa mashindano: Eliyas Mamo (Ethiopia)

Golikipa bora: Ismail Watenga (Uganda)

Mfungaji bora wa mashindano: Atahir Babikiir (Sudan), magoli 5

Kocha bora: Johnny Mckinstry (Rwanda).


SHULE BINAFSI MARUFUKU KUPANDISHA ADA!

Shule binafsi zapigwa marufuku kupandisha ada.

Shule binafsi zapigwa marufuku kupandisha ada.Serikali imepiga marufuku wamiliki wa shule binafsi kupandisha ada kuanzia Januari mwakani, hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Serikali kutoa tamko la kufuta ada na michango mbalimbali kwa shule zake za msingi na sekondari.
Taarifa ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, profesa Sifuni Mchome, imepiga marufuku shule hizo kuongeza ada kwa mwaka wa masomo unaoanzia Januari 2016 hadi hapo watakapopata maelekezo kutoka kwa Kamishna wa Elimu.‘Wale ambao tayari wameongeza ada kwa mwaka wa masomo wa 2016 bila kibali cha Kamishna wa Elimu, wizara haitambui ongezeko hilo kwa kuwa ni batili na hivyo zimefutwa,’ inasema taarifa hiyo.Taarifa hiyo ilisema, waraka wa Elimu Na. 4 wa Mwaka 2008 uliweka viwango vya ada vinavyotozwa katika shule za msingi na sekondari za Serikali na zile zisizo za Serikali.‘Ada iliyowekwa kwa shule za binafsi za kutwa ni Shilingi 150,000 huku za bweni ikiwa ni Shilingi 380,000 kwa mwaka.Aidha waraka huo ulielekeza kwamba ongezeko lolote la ada lazima lipate kibali cha Kamishna wa Elimu kabla ya kuanza kutumika,’ alisema.Hata hivyo imegundulika kuna baadhi ya shule zisizo za serikali zimekuwa zikiongeza ada kila mwaka pasipo kupata kibali cha Kamishna wa Elimu.Katika taarifa hiyo, Profesa Mchome alisema utamaduni huo wa kuongeza ada kila ifikapo mwishoni mwa mwaka umekuwa ukisababisha usumbufu mkubwa kwa wazazi/walezi na hata baadhi yao kushindwa kuendelea kusomesha vijana wao katika baadhi ya shule.Taarifa hiyo ilisema kuwa, ada zote kwa shule zisizo za serikali zitabaki kama zilivyoidhinishwa na Kamishna wa Elimu.Wamiliki wa shule hizo wametakiwa kuwasilisha taarifa kwa Msajili wa Shule aliyeko Idara ya Ithibati ya Shule inayoeleza kiasi cha ada kinachotozwa kwa sasa na tarehe shule ilipopata kibali kutoka kwa Kamishna wa Elimu kutoza kiwango hicho cha ada.Novemba 27, Serikali ilitoa waraka wa elimu namba 5 wa mwaka 2015, ambao ulifuta ada zote zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya elimu ya sekondari ya kidato cha kwanza hadi cha nne.Chanzo: Mtanzania

Friday, December 4, 2015

SUGU awataka madiwani wa Chadema kufukuzana na kasi ya DR. MAGUFULI




Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amewataka madiwani wa jimbo hilo waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadema kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kushindana na kazi ya rais John Magufuli.
 
Sugu alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha kumchagua diwani atakayewania nafasi ya Umeya kwa tiketi ya chama hicho.
 
Aliwataka madiwani hao kuchapa kazi na kuwafanya wananchi kujivunia kasi ya maendeleo inayoletwa na Mbunge na Meya wa jiji hilo ili wasitamani jimbo hilo lingeongozwa na wapinzani wao wa CCM.
 
“Hata CCM wenyewe wamebadilika, Magufuli anakwenda jalamba. Hakutakuwa na vitu kama ambavyo mnaviwaza, tunaenda kufanya kazi za wananchi ili wananchi wasitamani kwamba afadhali na hapa pangekuwa CCM. Waseme hata kama Magufuli anaenda spidi na sisi Mbeya yetu Meya na Mbunge wanakwenda spidi.”
Mpekuzi blog

WATUHUMIWA 8 WA UPOTEVU WA MAKONTENA 349 WAFIKISHWA MAHAKAMANI




KASI ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa Serikali baada ya maofisa wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.
 
Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51)
 
Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis  ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili.
 
Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi.
 
Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali  kuwa sh. bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya kodi zote kutolewa.
 
Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.
 
Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.
 
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.
 
“Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana,” alisema Hakimu Shahidi
 
Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo imefikishwa mahakamani hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.
 
Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.
Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.



Mmoja wa watuhumiwa hao akiwa ndani ya gari la Polisi.



Gari la polisi lililowabeba watuhumiwa hao likiondoka mahakamani hapo

MAGUFULI PROMISES TO WORK WITH PRIVATE SECTOR


President Dr John Magufuli addresses the business community members at the State House.
 President John Magufuli has promised to work closely with the private sector, saying the fifth phase government strongly believes in private sector partnership in creating citizens welfare and hence the need to come together and discuss how to cooperate to achieve Tanzania’s development objectives for the five years of  his first  term.

37 TRA WASIMAMISHWA KAZI !!!!




Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA,Phillip Mpango  amewasimamisha kazi wafanyakazi 37 mchana huu  kupisha uchunguzi wa sakata la upotevu wa makontena bandarini

Mpango pia ametoa agizo la watumishi wote wa TRA kuwasilisha taarifa za mali zao kwa utawala na kusiwepo na udanganyifu wowote.


Amesema mpaka sasa TRA imekusanya kiasi cha Tsh Bilioni 5 za kodi ya makontena hayo yaliyokuwa yamepitishwa kinyemela,


Powered by Blogger.