Sunday, November 13, 2016

Gavana BOT Afichua Siri ya Kilio Cha Fedha Kupotea Mtaani



Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo.

“Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu.

Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT.

“Fedha hizo zitarudi katika benki hizo wakati zitakapopelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” Profesa Ndulu aliahidi.

Katika hatua nyingine, Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu, huku akibainisha kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni  ongezeko la uzalishaji wa umeme na saraju.

Akizungumzia hali ya deni la taifa, alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka kutoka shilingi  trilioni 8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.

Profesa Ndulu alibainisha kuwa wakati deni linalotokana na kukopa ndani likipaa, deni linatokana na ukopaji wa limepungua baada ya Serikali kupunguza ukopaji nje ya nchi.

Mtoto wa Mjomba Anajilegeza Kwangu Kimapenzi...Ushauri




Ndugu zangu wanajamvi...kwanza naomba niulize, mtoto wa MJOMBA angu ni ndugu kivile?..Tumekuwa tukiishi na huyo mtoto wa mjomba angu kwa kipindi kirefu...mwanzoni ilikuwa kawaida tu maana alikuwa bado mdogo, ila sasahivi chuchu konzi...msambwana umenawili..kwahiyo ameanza kubadilika, muda mwingine anaweza kuwasha mziki nikipita anajisogeza tucheze huku nimbambie ila nakataa,,muda mwingine anakuja kunikaribisha chakula anaingia bila hata kupiga hodi nakuta hata nimetoka kuoga halafu dushe limeninginia yeye anaingia tu..muda mwingine anavaa kanga moko tu au akitoka kuoga anakuja chumbani kwangu hukukhanga imeloa anadai mafuta yake yameisha eti nimpe yangu ila akigeuka anatingisha...Sasa najiuliza nimle? au ntakosea?..
maana namimi ni binadamu stimu huwa zinapanda muda mwingine..Naombeni ushauri jamani..

Kundi la Kigaidi la ISIS Lapiga Marufuku Uvaaji was Chupi na Boxers Kwa

Kile kikundi cha kigaidi kijulikanacho na kuogopwa kwa ukatili wa kutisha hili kuleta hofu kimeenda hatua zaidi mbele kwa kuweka sheria kali.

Wahuni hao Wamepiga marufuku uvaaji wa boxer na Chupi kwa wanaume kwasabab ni kimagharibi badala yake unatakiwa uvae bukta ndefu inayovuka magotini ama kitambaa unachojifunga kiunoni kama taulo. Na ukibainika kuvaa hivyo hatua kali itachukuliwa dhidi yako.

Wanajeshi wa Iraq na Kurd walishangaa kukuta mabandiko hayo yanayokataza uvaaji wa Chupi na Boxers walipoukomboa mji wa Hammam Al Allil kusini mwa Mosul dhidi yao.

Pia ISIS imepiga marufuku kunyoa ndevu, kusikiliza mziki na kuvaa jeans zilizobana.

Donald Trump Kuwarejesha Wahamiaji Marekani Kwao

Donald Trump asema kati ya wahamiaji haramu milioni mbili ama tatu watasafirishwa kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa chi hiyo.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani,CBS, Trump amesema wahamiaji wote wenye rikodi za uhalifu, ikiwemo makundi ya wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele chake .

Hatma ya wahamiai haramu milioni nane na ushee waliosalia itafahamika mara tu mpaka utakapokuwa salama.

Donald Trump ameongeza kuwa semhemu ya ukuta ambao aliahidi kujenga kwenye mpaka baina ya nchi yake na Mexico, unaweza kuwa ni uzio.

Baraka Da Prince Anahitaji Msaada wa Haraka



















MTOTO wa miaka miwili badala ya kusema kikombe akatoa tusi, hufai kumpiga wala kumgombeza. Unachotakiwa kufanya ni kumtia nguvu katika juhudi zake za kujifunza na kumwambia kwa usahihi neno kikombe linavyotamkwa. Hivyo ndivyo hata kwa mtu mgeni katika miji mikubwa.

Mshamba akitoa huko mashambani na kukutana na lifti  katika majengo makubwa na kutaka kuvua viatu kisha ndio aingie, ukimcheka utakuwa juha.

Sasa unamcheka nini na hayo mambo kwao hakuna? Unashanga kitu gani yeye kuvua viatu na kutaka kuingia katika lifti wakati huko kwao kafundishwa ni ustaarabu ukikuta maeneo nadhifu uvue viatu?

Nimetoa mifano hiyo nikikumbuka tabia ya msanii Baraka Da Prince. Kwa siku za hivi karibuni bwana mdogo amekuwa na matukio na kauli za ajabu na cha kushangaza watu wanamshangaa na wengine kumtolea maneno makali.
Ni kweli Baraka anafanya mambo ya kijinga, yasiyofaa kufanywa na mtu anayejitambua. Ila mimi sishangai hayo mambo kufanywa na mtu aina ya Baraka.

Yangefanywa na Diamond, Ali Kiba na akina Chegge  ningeshangaa mno. Nishangae vipi Baraka kuposti nyumba ya mama yake Naj na kusema ni yake wakati najua kijana wetu huyu bado hajatokwa matongotongo machoni?

Katu siwezi kushangaa na yeyote atakayemshangaa, nitamshangaa yeye. Ni jambo linalotarajiwa kabisa kwa kijana ambaye miaka mitatu nyuma alikuwa akishindia kababu na mihogo huku akiwa ndani ya kaptura chafu isiyojulikana rangi yake, viatu vilivyotoboka na akiwa anadhihakiwa na kila msichana anayejaribu kumchombeza, kuwafanyia unyama ndugu zake kisa kuwa na msanii Naj katika mapenzi.

Baraka ni kwanini asitokwe na akili kwa Naj wakati miaka mitatu iliyopita alikuwa akimuona bibie katika magazeti na majarida akiwa kakumbatiwa na Mr Blue, msanii ambaye Baraka huyu amekuwa akimuona toka kipindi anaomba Shilingi ishirini akanunue ice cream kwa mama John?

Siwezi kumlaumu Baraka. Kumlaumu Baraka kwa ujinga anaoufanya ni sawa na kulaumu mtoto mdogo anapotukana kipindi akijifunza kuongea.

Siku moja katika mitandao ya kijamii Baraka baada ya kuposti picha ya mpenzi wake, Najma Dustan, msanii mwenzake, mtoto wa mjini Msami akamtania kwa kujifanya anamtamani Naj.

Kilichotokea kiliniacha hoi kwa kicheko. Baraka akatokwa na matusi kwa Msami na kumwambia akamtamani dada yake.

Baraka anatupa maneno haya kwa mtu ambaye amekuwa akionekana katika video na magazeti kwa zaidi ya miaka sita sasa.
Anatokwa povu la kijinga kwa Msami kwa kudhani kuwa eti ni kweli anamtamani mpenzi wake huku akiwa amesahau ni Msami huyu ambaye aliwahi kudaiwa kutoka na mastaa wengine wakubwa wa Bongo.

Msami ni mtoto wa  mjini sana kuliko Baraka. Msami kaona mengi ya kimjini kuliko yeye. Kutoka  dansa hadi kuwa msanii mwenye kueleweka, Baraka anatakiwa ajue uzito wa Msami.

Yeye bado ni mgeni katika jumba la mastaa, anayofanya ni sehemu ya ulimbukeni wa kawaida kwa mgeni. Kumlaumu au kumkosoa sana ni kumkosea.

Anayofanya Baraka ni sawa na mtu ambaye hajawahi kumiliki au kuendesha gari zuri la thamani. Atatembea kila eneo kutaka kuonesha kuwa anaendesha gari zuri. Huu ni  ulimbukeni.

Muda ukipita atakomaa.

Saturday, November 12, 2016

Wema Sepetu Ashindwa Kujizuia Kwa Ushindi wa Tuzo Tatu Kwa Diamond...Asema Haya



Maneno ya Wemasepetu leo baada ya Diamond Kushinda tuzo tatu

"Makofi matatu kwa Tuzo tatu... "Tanzania's Pride..." Sema picha hii Kali saaaaaaanaaaaa... Utasema sio wa Tandale...(Sorry Bro)... Congrats once again...!!"


Diamond Kuhusu Kumsaliti Zari Asema 'Simba Hawezi Kupita Kundi la Swala Bila Kula Hata Mmoja'


Diamond platnumz amesema kuwa yupo anajichanganya na wanawake wengi sana, anawindwa sana na wanawake na yeye akiamua kuwinda hakosi yoyote
Na pia amejifananisha yeye na simba na wanawake ni swala na kusema Simba akipita kwenye kundi la swala haachi kula angalau mmoja






Wizkid Amtolea Uvivu Shabiki wa Tanzania Aliemtukana Instagram


Baada ya Mtv ema kumpatia Alikiba tuzo ya african act kutoka kwa Wizkid ,mashabiki wa Tanzania hasa wa Alikiba wamevamia ukurasa wa Instagram wa star huyo wa Nigeria na kumtukana.
Leo Wizkid ameshindwa kuvumilia baada ya shabiki mmoja kumtukania mama yake.




Kauli ya Mwisho ya Samwel Sitta Baada ya Daktari Kumueleza Kuwa Asingeweza Kupona











Kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia (2005-2010), Samuel Sitta, mwanae wa kiume ameweka wazi maneno matatu ya mwisho aliyoyatamka, yenye maana nzito katika maisha.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni mtoto wa kiume wa marehemu, alisema kuwa baba yake alitoa maneno matatu ya kuukubali ukweli wa maisha baada ya Daktari kumueleza kuwa asingeweza kupona.

“That’s life (hayo ndiyo maisha),” Benjamin alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo yalikuwa maneno yake ya mwisho baada ya kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.

Maneo ya Sitta ni funzo kubwa kwa watu wote kuwa maisha huanza na huisha, hiyo ndiyo maana ya maisha na hakuna aishie milele hivyo tuishi kwa kuzingatia maana hiyo ya maisha na kuikubali.

Sitta ambaye anakumbukwa kwa kauli mbiu yake na matendo ya kusimamia ‘kasi na viwango’, alifariki kutokana na ugonjwa wa tezi dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Alitangaza kustaafu siasa muda mfupi baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo yeye alikuwa mmoja kati ya waliokuwa msitari wa mbele kumnadi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.

Benjamini alieleza kuwa marehemu atazikwa Urambo Mkoani Tabora na kwamba ratiba ya mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge ambayo ndiyo inayoratibu mazishi

“Tumempoteza baba na kiongozi ambaye tulikuwa tunamtegemea kwa ushauri na masuala mbalimbali, tutafuata yale aliyokuwa akituelekeza,” alisema Benjamini.
Hakika Taifa limempoteza mtu muhimu, pengo lake halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

TATIZO LA FANGAS SEHEMU ZA SIRI












Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast 


infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke.

Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja na  aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi.

Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine kama zilivyoelezewa hapo juu bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya  eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya PH ya eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya uke ni 4.0 – 4.5) au uwiano wake na vimelea (microorganisms) lakini pia uharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics na kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.

Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili;

Maambukizi yasiyo makali yaani ‘uncomplicated thrush’ kwa kiingereza:
Maambukizi makali yaani ‘complicated thrush’ kwa kiingereza:

Kwa kawaida Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni wale wenye;

Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji yaliyochanganywa na jiki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali hiyo husababisha kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina ya lactobacilli
Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo yana tabia ya kushusha kinga ya mwili
Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS) n.k
ANGALIZO Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa.

Dalili na viashiria kwa wanawake;
Kuwashwa sehemu za siri (kwenye tupu ya mwanamke)
Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)
Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness)
Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia)
Maumivu au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo (wakati mtu anakojoa)
Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia minora)
Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini (cottage cheese like discharge) wenye muonekano unaojulikana pia kama curd-like appearance. Kwa kawaida, uchafu huu haumbatani na harufu yoyote isipokuwa panapokuwa na tatizo la ziada kama ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria vaginosis. Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine yaliyokaribu na tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki (groin area) au perineum na kusababisha kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.
Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi wakati mwanamke anapokaribia kupata hedhi.

Dalili na viashiria kwa wanaume ni;
Kuwashwa sehemu za siri
Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye ncha ya uume
Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama nilivyoeleza hapo juu) kwenye sehemu ya juu ya uume.
Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore on the glans)

Powered by Blogger.