Monday, November 14, 2016

Rich Mavoko Akana Kusign Mkataba wa Kuwa Chini ya Diamond..Atoa Ufafanuzi Hapa nini Kinaendelea Kwa Sasa



Baada ya msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize kudai Rich Mavoko tayari ni member wa label hiyo, Rich Mavoko aibuka na kuzungumzia swala hiyo.

Rich amedai bado yeye ni msanii huru.

“Hizi stori nimezisikia kama Harmonize alivyosema, hii issue imetokea kwa sababu aliniona na Salam (Meneja na Diamond) na tulikuwa tunaongea issue nyingine, atakuwa hajaelewa nini kinaendelea na siwezi kumlaumu sana. Lakini sijui kusema nipo official hapana bado, kama ikiwa official kwanini niwafiche?, haya ni maisha ya mtu na hii ni biashara,” alisema Rich Mavoko.

Aliongeza, “Tunapokuja kwenye swala kama hili ni lazima niangalie kama kuna faida ua hasara. Kwa hiyo kitu kikubwa ndio hicho Harmonize aliniona na Salam na simlaumu kwa sababu hajui chochote, kama itakuwa official lazima nitasema kila mtu ajue,”

Pia Mavoko ameeleza nini kinamchelewesha kusaini kwenye label hiyo.

“Hili swala tatizo linazungumza sana mitaani, lakini mimi binafsi nisema vitu vitakapo kuwa tayari mimi nitaweka wazi na kama ikishindikana pia nitasema, lakini kwa sasa kuna mambo yanaendelea,” alisema Rich.

Diamond Plutnumz » Diamond Ndiye Msanii Tajiri zaidi Kwa Sasa Africa


Jarida la Forbes la nchini marekani limetoa wasanii matajiri zaidi duniani ,Africa na kanda mbali mbali ambapo kwa upande wa Africa mashariki.

Diamond platinum ameongoza kwa kuwa na utajiri wa dollar million 4.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania hasa baada ya kununua Nyumba yake ya south Africa.

Vitu vingine anavyomiliki ni Majumba ya kifahari Dar,Magari ya kifahari , Berber shop, Maduka ya nguo za mitindo ya kisasa na vingine Vingi.

Amefatiwa na Dr Jose Kamilioni wa Uganda ambaye anakadiliwa kuwa na utajiri wa dollar milioni 3.9 ... Wanafatia Akothee na Jaguar anashika nafasi ya 4

Wanachokiangalia zaidi sio pesa kwenye account Bali thamani ya vitu anavyomiliki.....

Katika jarida hilo linaonyesha diamond akiwa anafanya wastani wa show 2 kwa wiki show 8 kwa mwezi na show 100 kwa mwaka ambapo show yake ya chini anakadiriwa kulipwa wastani wa dollar elfu 20,000 na show ya juu analipwa wastani wa dollar elfu 75,000 .

Mikataba yake na makampuni kama Cocacola,Vodacom na DSTV

Jarida ilo linaonyesha pia diamond anaweza vaa vitu vyenye thamani ya dollar laki 150,000 ambazo ni zaidi ya milioni 350,000,000 za tanzania mwilini mwake kwenye shoo moja ambavyo ni Pete,cheni,viatu kofia,shati na suruali na vingine.

Kiukweli huyu mwenzetu yupo kwenye another level kabisa.

Ongera kwa diamond platinum na wapenda maendeleo wote wa nchi hii tuendelee kumsaport msanii huyu aweze kufika mbali zaidi...

Fuata Njia Hizi, Mwanamke Hakukatai Ng`oo Hata Awe Vipi



Kifupi unakuta mwanaume ana status nzuri tu lakini anakosa mwanamke anayejielewa.yaani wengine hadi wananiuliza sometimes mimi "hivi wewe unawapataje wanawake wazuri na wanaojimbua hivo".

Sasa leo nimeona ni vyema nikishare na nyinyi namna ya kumnasa demu hata awe ni anajitambua vipi!

1: Unapoomba namba ya simu hakikisha huombi kwa papara, yaani usioneshe kama una shida sana na usioneshe kama unataka kumtongoza, bali onesha kama unataka tu ulafiki wa kawaida,yaani lafiki wa kuchati nae tu kawaida.

2: Akikupa namba leo kausha usimtafute leo leo, mtafute baada hata ya wiki,msalimie tu na umpigie, hapa uangalie na muda ambao unadhani mtu anakuwa free, sio kupiga simu asubuhi sana au mchana au usiku sana, piga mida ya saa mbili usiku,na usiongee nae zaidi ya dakika 5.

3: Hakikisha kila siku unamtumia msg mara 3 na kumpigia simu mara moja, yaani asbh mtakie asbh njema, mchana, jioni na usiku piga kumpa pole na heka heka za mchana, ongea nae si zaidi ya dakika 5 ili usimchoshe.

4: Hakikisha hutumii maneno ya mtaani sana mfabo oya,inakuwaje,michongo vipi, barida, mzuka, poa n.k. Tumia maneno mazuri ya busara mfano sawa, haya, umeshindaje, habari yako, n.k. yaani asikuone wewe hujitambui.

5: Weka nae urafiki wa kudumu kiasi kwamba awe anakumiss, na ukimtext asipojibu mtumie vocha hata ya buku. Ila angalia usitumie pesa sana.

6: Omba outing nae, na akikubali basi mpeleke sehemu tulivu yenye adabu na sio mnaenda bar, mkiwa huko ongelea zaidi maisha ya kawaida ya mwanadamu, usiongelee ishu za X wako kamwe, ishu za mapenzi usiongelee kabisa, weka vistory vya kuchekesha ili awe anafurahi na kukumiss mkitoka hapo.

7: Ukiwa unapiga nae stori kwenye simu usiwe unaongea sana, na hata mkiwa pamoja basi usiongee sana kama chiriku, pangilia maneno sana ya kuongea(waza kabla ya kusema).

Baada ya urafiki wa kama miezi miwili hivi, hapo sasa mtamkie wazi wazi kwamba unampenda tangu muda mrefu, na umtongoze kwa heshima sana. Nakuhakikishia hapo hachomoki hata kwa dawa.

NB: Mbinu hizi ni za kuwapata tu wanawake wanaojielewa, wanaotaka mwanaume/mpenzi na sio wanaotaka pesa. Kwa wale wanawake vicheche, we tumia pesa tu, ukimtongoza leo jioni basi kesho unamfunua

TB Joshua Afunguka 'issue' ya kumtabiria Clinton Ushindi Marekani Ambao



Mhubiri mashuhuri raia wa Nigeria TB Joshua amevunja kimya baada ya utabiri wake kuwa mgombea urais nchini Marekani Hillary Clinton angeshinda, kugonga mwamba.

Mhubiri huyo alikejeliwa kwenye mitandao ya kijamii wakati ujumbe wa utabiri wake, kufutwa na baadaye kurejeshwa katika akaunti yake ya Facebook kufuatia ushindi wa Donald Trump.

Hata hivyo, wafuasia wake wamekuwa wakimtetea wakisema kuwa utabiri wake ulitimia kwa sababu Bi Clinton alishinda wingi wa kura licha ya yeye kushindwa kutokana mfumo unaotumiwa kwenye uchaguzi nchini Marekani unaofahamika kama "electoral College".

Ujumbe mpya katika akaunti ya Joshua ya Facebook unaunga mkono maoni hayo,ukisema:

"Tumeona matokeo ya uchaguzi nchini Marekani. Baada ya kusoma, utaelewa kuwa hii inahusu kura nyingi, kura ya waamerika wengi"

"Kwa hali hii tunahitaji roho ya nabii kutambua au kumuelewa nabii." TB Joshua anaendelea kusema.

Majina ya Watu 4 Matajiri zaidi Tanzania



Uchumi mkubwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unategemea zaidi kilimo kwa takriban asilimia 25 ya GDP na asilimia 85 Exports. Aidha, Tanzania ina madini kama dhahabu, almasi, makaa yam awe, uraniamu, chuma, shaba, Tanzanite n.k.

Tanzania imetengeneza matajiri wengi sana, na hawa ni wanne wakubwa kwa mujibu wa jarida la Forbes. Na mamilionea hawa wametudhihirishia kwamba kila kitu kinawezekana, na kila mtu ananafasi ya kuwa tajiri ili mradi tu aweke juhudi katika kazi yake na kwa makini

4) Reginald Mengi – Thamani: $560 Million

Bwana Reginald Mengi ni mmiliki wa wa moja ya kampuni kubwa inayomiliki vyombo vya habari ya IPP  Media Group, yenye magazeti 11, stesheni za redio na TV na mitandao ya intaneti.



3) Said Salim Bakhresa – Thamani: $575 Million

Umri wake ni miaka 65, nay eye alianza mwenyewe mpaka kufikia hapo. Mfanyabiashara huyu ameanzisha Azam TV, yenye mfumo wa kulipia chaneli za TV Afrika ya Mashariki. Aliacha shule akiwa na miaka 14 na kuanza kuunza Mix (Urojo) na baadae kufungua mgahawa mdogo na kisha kuhamia katika biashara ya mazao ya kilimo. Katika miongo mine iliyopita  ameongeza mauzo yake kwa dola za kimarekani milioni 750, na kuifanya Bakhresa Group kuwa moja ya kampuni kubwa Afrika ya Mashariki kwa kuwa na wafanyakazi zaidi ya 5,000 na kujikita zaidi kwenye bidhaa za vinywaji na chakula, Upakiaji wa bidhaa, huduma za feri na Mafuta ya Petroli na usafirishaji.


2) Rostam Azizi –Thamani: $1 Billion

Rostam Azizi ni tajiri wa kwanza kutokea Tanzania. Mnamo mwezi Mei mwaka 2014 aliuza hisa zake 17% alizokuwa akimiliki katika kampuni ya Vodacom. Vile vile ana miliki kampuni Caspian Mining, inayojihusisha na uchimbani wa madini kwenye kampuni kubwa kama BHP Billiton na Barrick Gold. Kampuni hiyo ya Caspian Mining pia inamiliki sehemu kubwa ya ardhi yenye uwezekano wa kuwa na madini kama dhabu, chuma na shaba hapa Tanzania. Aidha, Rostam ana hisa katika Bandari ya Dar es salaam ambapo yuko pamoja na Hutchison Whampoa na ana miliki sehemu ya ardhi kubwa hapa Tanzania, Dubai, Oman na Lebanon.



1) Mohammed Dewji – Net Worth: $1.3 Billion

Ana umri wa miaka 40, na ndio mdogo kuliko matajiri 50 wa Afrika yote kwa mfululizo wa miaka 3 sasa, ana miliki 75% ya kampuni ya METL Group, inayohusika na viwanda nchini humu iliyoanzishwa na Baba yake. Kizuri kuhusu Mohammed Dewji aliibadisha nyumba ya kufanyia manunuzi ya bidhaa za kilimo kuwa kiwanda cha uzalishaji.

Mshindi wa Tuzo ya Nobel Wole Soyinka Adai 'Nitaondoka Marekani Trump akiapishwa'



Mshindi wa Tuzo la Nobel na mwandishi raia wa Nigeria Wole Soyinka, anasema kuwa ataondoka Marekani siku ambayo Donald Trump ataapishwa kuwa rais.

Wiki iliyopita Soyinka aliahidi kuwa angeirarua green Card yake, ikiwa Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Green Card humpa mtu kibali ya kuishi rasmi nchini Marekani na hupewa umuhimu mkubwa na wahamiaji kutoka nchi za Afrika.

Soyinka alitoa matamshi hayo wakati akihutubia wanafunzi katika chuo cha Oxford nchini Uingereza.

Mwandishi huyo maarufu alionekana kuchukua msimamo mkali kupinga seza za uhamiaji za bwana Trump.

Soyinka alishinda tuzo la Nobel la fasihi mwaka 1986 na kuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hilo.

Waziri Mahiga: Mkataba Kusaka Walioficha Mabilioni Uswisi Wasainiwa Tanzania



Serikali ya Tanzania na Uswisi zimesaini Mkataba utakaowawezesha Makachero wa Tanzania kwenda nchini Uswisi na kufanya uchunguzi katika mabenki ya huko ili kupata taarifa sahihi za walioficha mabilioni toka Tanzania.

Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli.

Hata hii ni moja ya hatua muhimu ya Serikali awamu ya tano katika kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umm

Boss Ananitaka Kingono, Nipo Njia Panda Naomba Ushauri


Katika harakati za kutafuta kazi nilibahatika kufika ofisi moja maeneo ya Mwenge (Dar es salaam) kwangu ilikua faraja kubwa sababu kiukweli nilikua nahangaika sana na hali ya ugumu wa maisha na sikutaka kabisa kuwa tegemezi kwa mtu yoyote (wakiwemo wazazi) niliamini kunipa elimu ni mtaji muhimu na tosha na lilikua jukumu langu kuandaa maisha yangu mwenyewe na kujitegema

Nilipofika pale niliomba kuonana na boss ila nikaambiwa haiwezekani labda ningekua na appointment, kutokana na uzoefu hii kauli nilikua nimekutana nayo mara kadhaa hivyo ilikua hainisumbui sana, nikamwambia yule receiptionist kuwa nilikua na appointment (kiukweli sikua nayo na nakiri nilidanganya na nilikosea ila sikuwa na namna mbadala) akaniuliza nimwambie we ni nani nikasema mwambie (tax consultant)

Waliongea mawili matatu then nikaruhusiwa kuingia nadiriki kusema shida ni mwalimu mkubwa sana kwani sikuwa na woga wowote kuonana na yeyote na kujinadi, baada ya mazungumzo na mahojiano ya kama dakika sita yule manager (mwanamke) akaniambia alhamisi niende nikafanye interview na kutokana na intro niliyoitoa hiyo siku (Jumanne).

Haikua kazi kwangu kupata hiyo kazi hata baada ya interview ya alhamisi, tulikubaliana terms za kazi na mshahara then nikapewa mkataba. Nilifurahi sana nikijua sasa mipango yangu itaenda vema (kwakweli mshahara ulikua mzuri tu) hadi nikaanza kupangilia biashara ndogondogo ili kuinua uchumi wangu.

Nilianza kazi wiki iliyofuata na wafanyakazi wenzangu walikua watu wema sana kwangu hivyo nilifanya kazi kwa furaha na ufanisi sana mpaka hali ilipokuja kubadilika.

MABADILIKO

Baada ya wiki moja mambo yalianza kubadilika pale ofisini, mara kwa mara boss alikua na vikao visivyokua na mbele wala nyuma na mimi na akawa mkali kwa wafanyakazi wenzangu especially wa kike na taratibu wakaanza kuniogopa.

Siku moja aliniita ofisini (ilikua Ijumaa) na akaniambia nifunge mlango nilishtuka sababu normally ukiingia ofisini lazima ufunge mlango cha kushangaza akaniambia ni-u lock nikafanya alivyotaka,

Hakuna cha maana alichoniambia zaidi ya story za kifamilia tu oooh mara mumewe (aliekuwa meneja kabla hajaumwa) anasumbuliwa na kisukari na presha na anapata taabu sana mi nikawa 
msikilizaji tu na aliongea muda mrefu hadi jua likazama na watu waliondoka ofisini alibaki mlinzi tu.

Aliongea mengi na mwisho akaniambia anataka nimsaidie (ngono) kitu ambacho kilinishtua kidogo ukizingatia ni mtu mzima rika la mamaangu, nilimbembeleza kuwa hapo si pahali salama ili tu aniache siku hiyo ili nikajipange jinsi ya kuepukana nae na kuikabili ile hali.

Alinikomalia sana hadi kunivamia physically na alionekana wazi alikua desperate for sex ila nilifanikiwa kumpanga na akanielewa baada ya hiyo siku ofisi nzima wakahisi nilizini na yule boss hivyo kukawa na minong'ono mingi na sikuwa na namna ya kuwaaminisha vinginevyo.

Tangu hapo ni wiki ya pili sasa huyu mama ananisumbua sana, ananiahidi mambo mengi kama nitakubali kusex nae na ni dhahiri nikimtamkia kuwa SITAKI nitapoteza kibarua kwani ye ndo meneja hapa na ndo anaajiri na kusitisha ajira,

Leo hii (Jmosi) kanipigia simu na kuniambia kesho saa saba ana kikao na mimi cha kikazi ila location naona hata aibu kuisema. Wakuu najua kuna watu humu wakike na kiume ambao wamekutana na hali kama yangu,

Naipenda kazi na sina pa kushikilia kwa sasa lakini pia sitaki kuisaliti imani yangu na msimamo kwa kupenda vitu vya dezo na kufanya uzinzi na mtu wa rika la mama yangu, ni dhambi kubwa na pia ni kinyume cha maadili ya jamii yetu lakini pia nikifikiria matokeo ya kuachishwa kazi (na mipango niliyokwisha iweka kichwani kwangu) roho inaniuma sana nabaki nikiwaza na kuwazua bila kujua haswaa nishike wapi.

Msimamo wangu ni kutokulala na huyu mama no matter the consequences ila naomba mnipe chakula cha akili ili akinifukuza kazi basi niwe nimeimarika kisaikolojia kwa ushauri wenu na nisitetereke sana kisaikolojia.

Asanteni

» MSICHANA WA MIAKA 25 ALIYEFANYA MAPENZI NA WANAUME 5,000



Ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni. Wakati wapo wanawake ambao hawapati salamu barabarani, Nikki Lee, 25 amevunja rekodi baada ya kutimiza idadi ya wanaume 5,000 aliofanya nao ngono.

Nikki ambaye aliibukia katika fani ya urembo anasema alifanya vitendo hivyo kwa muda wa miaka tisa sehemu mbalimbali alizokuwa akitembelea.

Anasema alikuwa anafanya ngono katika klabu za usiku, ndani ya ndege, mbuga za wanyama, sehemu za kupaki magari, ndani ya gari, sinema na disko.

Anasema kwamba alianza kufanya hivyo tangu alipotolewa bikira yake akiwa na umri wa miaka 16.

Anasema aliweza kufanya ngono na wanaume wawili kwa siku. "Nilikuwa nasikia raha  ya ajabu na ndiyo maana nilipenda kufanya ngono wakati wote," anasema Nikki. Alipokuwa na miaka 21 alifikisha idadi ya wapenzi 2,289 ambao alikuwa amewaandika katika kitabu chake chekundu.

"Hakuna mwanaume aliyepita mbele yangu asinitamani kwa waliotaka kufanya nami mapenzi nilifanya hivyo, kwa sasa nimeathirika na ngono," anasema Nikki.

Sunday, November 13, 2016

Tanzania yaongoza Duniani Kwa Utoaji wa Huduma za Kifedha kwa Kutumia Simu



Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.

Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” alisema.

Kuhusu mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, alisema umelenga kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo.

“Mkutano huu unasimamiwa na shirika la mawasiliano duniani ITC ambao umelenga kujadili namna ya kutumia mitandao ya simu kupeleka huduma za kifedha katika maeneo yasiyofikiwa na huduma za kifedha hasa ambako hakuna mabenki. Mkutano huu nchi imeamua kuuanda kwa ushirikiano wa TCRA na BOT, ” alisema.

Naye Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu alisema hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

“Hadi kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii inakua kwa kasi,” alisema.

Profesa Ndulu alisema kuwa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imesaidia kukuza uchumi wa nchi.

“Malipo ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi hususani kwamba muda ndio muhimu,” alisema.
Aliongeza kuwa “Mitandao ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account, mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo umepungua kwa sasa,”

Powered by Blogger.