Home »
KITAIFA
» Majina ya Watu 4 Matajiri zaidi Tanzania
Uchumi mkubwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unategemea zaidi kilimo kwa takriban asilimia 25 ya GDP na asilimia 85 Exports. Aidha, Tanzania ina madini kama dhahabu, almasi, makaa yam awe, uraniamu, chuma, shaba, Tanzanite n.k.Tanzania imetengeneza matajiri wengi sana, na hawa ni wanne wakubwa kwa mujibu wa jarida la Forbes. Na mamilionea hawa wametudhihirishia kwamba kila kitu kinawezekana, na kila mtu ananafasi ya kuwa tajiri ili mradi tu aweke juhudi katika kazi yake na kwa makini4) Reginald Mengi – Thamani: $560 MillionBwana Reginald Mengi ni mmiliki wa wa moja ya kampuni kubwa inayomiliki vyombo vya habari ya IPP Media Group, yenye magazeti 11, stesheni za redio na TV na mitandao ya intaneti.3) Said Salim Bakhresa – Thamani: $575 MillionUmri wake ni miaka 65, nay eye alianza mwenyewe mpaka kufikia hapo. Mfanyabiashara huyu ameanzisha Azam TV, yenye mfumo wa kulipia chaneli za TV Afrika ya Mashariki. Aliacha shule akiwa na miaka 14 na kuanza kuunza Mix (Urojo) na baadae kufungua mgahawa mdogo na kisha kuhamia katika biashara ya mazao ya kilimo. Katika miongo mine iliyopita ameongeza mauzo yake kwa dola za kimarekani milioni 750, na kuifanya Bakhresa Group kuwa moja ya kampuni kubwa Afrika ya Mashariki kwa kuwa na wafanyakazi zaidi ya 5,000 na kujikita zaidi kwenye bidhaa za vinywaji na chakula, Upakiaji wa bidhaa, huduma za feri na Mafuta ya Petroli na usafirishaji.2) Rostam Azizi –Thamani: $1 BillionRostam Azizi ni tajiri wa kwanza kutokea Tanzania. Mnamo mwezi Mei mwaka 2014 aliuza hisa zake 17% alizokuwa akimiliki katika kampuni ya Vodacom. Vile vile ana miliki kampuni Caspian Mining, inayojihusisha na uchimbani wa madini kwenye kampuni kubwa kama BHP Billiton na Barrick Gold. Kampuni hiyo ya Caspian Mining pia inamiliki sehemu kubwa ya ardhi yenye uwezekano wa kuwa na madini kama dhabu, chuma na shaba hapa Tanzania. Aidha, Rostam ana hisa katika Bandari ya Dar es salaam ambapo yuko pamoja na Hutchison Whampoa na ana miliki sehemu ya ardhi kubwa hapa Tanzania, Dubai, Oman na Lebanon.
1) Mohammed Dewji – Net Worth: $1.3 BillionAna umri wa miaka 40, na ndio mdogo kuliko matajiri 50 wa Afrika yote kwa mfululizo wa miaka 3 sasa, ana miliki 75% ya kampuni ya METL Group, inayohusika na viwanda nchini humu iliyoanzishwa na Baba yake. Kizuri kuhusu Mohammed Dewji aliibadisha nyumba ya kufanyia manunuzi ya bidhaa za kilimo kuwa kiwanda cha uzalishaji.
0 comments:
Post a Comment