Sunday, January 22, 2017

Kwa walevi Mnaotaka Kuacha Pombe Dawa Soma HAPA!!!



makala iliyopita nilizungumzia madhara ya unywaji wa pombe na kama hukuipata makala hiyo basi isome hapa........, watu wengi ambao ni walevi sana kwenye jamii hudharauliwa na kulaumiwa sana kwa kuendekeza tabia hizo, ni kweli wanaweza kua wanapaswa kulaumiwa lakini upande wa pili ni kwamba watu hawa pia hawapendi kua hivyo na wanashindwa kuacha kwasababu pombe ina kitu kinaitwa addiction yaani mazoea na sio rahisi kuacha kirahisi kwani mwili umeshazoea na unataka zaidi, ikitokea umeacha ghafla hata shughuli zako zitakushinda kwani utapata dalili kitaalamu kama withdraw syndrome ambazo ni kutetemeka, kichwa kuuma, kutapika , kushindwa kula na kua mgonjwa muda wote.

maana yangu ni kwamba mlevi aonekane kama mgonjwa kwenye jamii na kama anataka kuacha pombe basi mpeni msaada na sio kumtenga, swala la kuacha pombe linawezekana kabisa kwa walevi waliopindukia au watu wanaokunywa kawaida tu. yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa kuacha pombe..

amua kutoka moyoni; hakikisha maamuzi haya yametoka moyoni mwako kulingana na wewe unavyoona na sio kwamba unataka ili kuacha kuridhisha kikundi fulani au mtu fulani, hii itakupa nguvu ya kupambana na majaribu ya kutaka kunywa pombe tena.

wajulishe wanywaji wenzako nia yako; waambie rafiki zako kwamba umeamua kuacha pombe kwa muda fulani, wape sababu zako za msingi na kama huna waambie ni sababu binafsi za kifamilia, wajulishe kwamba inaweza kua ngumu na utaomba msaada wao iwapo ukiwaka tamaa ya kunywa pombe tena.

jiwekee malengo mafupi; anza kwa kujiwekea kwamba sitakunywa pombe mwezi huu wote wa kwanza, ukifanikisha ongeza mwezi mwingine...hii itakuapa motisha ya kuendelea kuacha kuliko kusema kwanzia leo sinywi tena kwani utajikuta unakunywa. kama mwezi ukiisha na kujikuta umesevu pesa nyingi kwa kutokunywa basi jinunulie zawadi yeyote.

pangilia starehe zako; kama starehe zako nyingi zinahusisha kunywa pombe basi pangilia starehe zingine ambazo hazitaki pombe mfano kwenda bichi, kwenda kuangalia sinema, kungalia mpira uwanjani na kadhalika. epuka kwenda disko na bar kwa kipindi hiki cha mwanzo.

jitoe nje ya raundi za pombe
; kama umeacha pombe usijihusishe na kuwanunulia watu pombe kwa kuzungusha kama wanywaji wanavyofanyiana wakiwa bar, nunua kinywaji chako kimoja kama ni soda au juisi kisha kaa pembeni ukinywa. kuwanunulia watu utajikuta na wewe unanunuliwa pombe.

kama mnatoka kwenda kwenye starehe basi endesha gari; kuendesha gari ni sababu kubwa ya wewe kutokunywa pombe kama sheria inavyotaka na hata ukilazimishwa kunywa utawaambia rafiki zako kwamba mimi ni dereva leo.

kua tayari kuzungumzia swala lako; watu wengi watakua wanakuuliza kwanini umeamua kuacha pombe, basi andaa sababu za msingi za kuwaambia kama jinsi pombe inavyoharibu maisha yako ya kijamii, kiuchumi na kiafya na wakati mwingine ukiona umezidiwa waambie ni sababu za kifamilia zaidi.

badilisha sehemu za kukutana na watu;
 kama ulikua ukipanga kuonana na mtu, unaenda bar basi badilisha sehemu ili ue unaenda kuonana nao kwenye mgahawa au sehemu zingine za wazi ambapo pombe haziuzwi.

furahia faida za kuacha kwa muda huo;
 angalia ni kaisi gani cha fedha umesevu kwa kuacha pombe, unajisikiaje kukaa muda mrefu bila kupata hangover, unajisikiaje jamii iliyokudharau sasa inakuheshimu na hii itakupa nguvu zaidi a kusonga mbele.

dawa za kuacha pombe kwa walevi sana;
 kuna dawa maalumu ambazo zimetengenezwa kuwatibu watu ambao wanataka kuacha pombe hasa wale ambao wameshindwa kuacha kwa njia nilizotaja hapo juu, utaratibu huu hufanyika chini ya uangalizi wa daktari hasa kwa nchi zilizoendelea...dawa hizi hufanya kazi kwa kukosesha mtu hamu ya kunywa pombe, kuongeza muda wa hangover mpaka siku tatu, na kuzuia madhara mtu anayopata kwa kuacha pombe haraka mfano disulfiram.[sina uhakika kama zinapatikana nchini], pia unawea kutumia virutubisho mbalimbali vya kuondoa sumu mwilini baada ya kuacha pombe, hivyo unaweza kuvipata hapa nchini.

SIMANZI: Ajinyonga Baada ya Kusalitiwa na Mpenzi wake! Aacha barua yenye ujumbe mzito!!



Kijana mmoja kwa Jina la Fredrick Richard amefikia hatua ya kujinyonga baada ya mpenzi wake (Rose) kumsaliti na kugawa tunda kwa rafiki yake kwa jina Robert.


Kabla ya kufikia maamuzi ya kujitoa uhai, kijana huyo aliandika barua ya simanzi kusikitishwa kwa kitendo alichofanyiwa na wawili hao.

Hii hapa chini ni picha ya huyo inaesadikika alikuwa mpenzi wake;




Wednesday, January 18, 2017

Mwenyekiti Chadema Ahukumiwa Miezi Nane Jela Bila Faini,Kisa Hiki Hapa..!!!



VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Selemani Mathew na Katibu wa Chadema Kijiji cha Nyangamara ‘A’ mjini Lindi, wamehukumiwa kifungo cha miezi minane jela bila ya faini kutokana kufanya mkutano bila ya kibali cha Jeshi la Polisi katika kijiji hicho wilayani Lindi.

Viongozi hao waliohukumiwa ni kati ya viongozi sita waliokamatwa na kutuhumiwa kufanya mkutano bila ya kibali cha Jeshi la Polisi nchini.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Lindi, Muhini alitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza mashtaka pande zote mbili na kubaini viongozi hao walitenda kosa la kisheria.

Tukio lililotokea Aprili 3, mwaka jana kwa viongozi na wanachama kwa pamoja kufanya mkutano bila ya kibali cha Jeshi la Polisi wilayani Lindi.

Alitaja kifungu cha sheria kilichovunjwa ni Kipengele 74(1) na 75 kinachozungumzia Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinachosomeka kwa pamoja na sheria ya Jeshi la Polisi.

Alisema washitakiwa wengine wanne wanaachiwa huru, kwani walibainika hawana hatia. Hao ni Bashiru Rashidi, Hassani Mchilima, Abdallah Mmasikini na Isimael Kupilila.

Akizungumzia hukumu hiyo, Mratibu wa Wanawake wa Chadema Mkoa wa Lindi, Sina Kikuwi alisema mahakama haikutenda haki kwa watuhumiwa hao.

Alisema taarifa walikuwa nayo kwenye vikao hivyo vya ndani havihitaji kibali, bali kutoa taarifa ambazo zilishatolewa katika mamlaka husika.

Selemani Mathew aliwahi kuwa D
iwani wa Vijibweni wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM. Aligombea katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi mwaka juzi, ambapo katika kura za maoni za CCM alishindwa na Nape Nnauye.

Baadaye alihamia Chadema ambako alikuwa mgombea ubunge wa chama hicho, lakini pia alishindwa na Nape ambaye sasa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Sio kila EX wako anaeomba mrudiane anakuwa kakumbuka utamu wengine hutest tu


Sio Kila EX Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha! Wengine Huomba Kurudi Ili Wakutesti Tu Jinsi Ulivyo Mbulula,Jinsi Usivyo Na Msimamo Na Jinsi Ulivyo CHEAP Na Huna Misimamo Wala Future.
.
Jitu Mmeachana Miezi 6,Leo Linakutesti Lirudishe Majeshi,Na Wewe Ulivyo Kiazi,Upo-Upo Tu,Ina Maana Miezi Yote Hii Ulikuwa Umeganda Unasubiria Rehema Zake Ama?? Kurudia Matapishi Ya EX Ukitegemea Amebadilika Ni Sawa Na Kupika Sufuria La Makande Kwa Mshumaa,Utaambulia Masizi Tu..
.
Kipi Kipya Kakiona Kwako Hadi Arudi??Nini Kilimshinda Huko Nyuma Ambacho Leo Anakiweza Anataka Kurudi??Akafie Mbele Huko. 
.
KUWA NA MSIMAMO,Ukisema Its Over Umaanishe,Sio Unakuwa Na Hisia Zinapepea Tu Kama Bendera Ya Katibu Kata Wa Kishumundu... Mtu Kama Hajielewi Achana Nae,Siku Akijirudisha Mwambie Kwanza Akapimwe Minyoo Ya Kinyarwanda. 
.
Umekazana Kuwaambia Marafiki Zako 'Siku Hizi Hakuna Mapenzi Ya Dhati Watu Wote Majanga Tu',Nani Amekwambia Hayapo?? Yapo Sana Ila Wewe Unatumia Mbinu Tofauti..
.
Huwezi Kusoma Degree Ya Law Halafu U-Apply Kazi Ya Chief Accountant Wa Bodi Ya Tumbaku...Kila Siku Utasingizia Balance Sheet Haina Jurisprudence..Lawyersl

Mmenielewa! Acha Kudate Watu Wasiojielewa,Usidate Kwa Sababu Uko Lonely,Usiwe Desperate Kuingia Mahusiano Kwa Sababu Shosti Zako Wanakusimulia Walivyopelekwa Ruwenzori Waterfalls.. 
.
Ingia Kwenye Mahusiano Pale Moyo Wako Ukiwa Tayari Na Mtu Uliyemfia Kihisia Na Amekuwa Approved Na Veins,Auricles,Na Aorta Za Moyo Wako Kwamba He/She Is Really The One.. Unadate Na Mtu Ambaye Mustakabali Wake Mwenyewe Haujui,Ukimuuliza Anataka Kuwa Wapi Ndani Ya Miaka 5 Ijayo Anakwambia Mungu Anajua Dont Worry,Halafu BBM Na Instagram Unajiita Baby Ake Mie Iam In Love..

Utaishia Kufua Boxer Hadi Kucha Zinukie Gololi! Mbwa Kamwe Hashughuliki Na Kesi Za Paka Kufungiwa Kabatini.Date The Right Person,With Right Reasons,In A Right Time Uone Kama Mapenzi Hayapo...
.
Nikipanic tena nitarudi

Monday, January 16, 2017

Jacqueline Wolper Apigilia Msumari ishu ya Kumpiga chini Harmonize


Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amedai kwa sasa anauguza majareha ya moyo aliyoyapata kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Harmonize.


Wiki moja iliyopita muigizaji huyo aliweka wazi kuwa hayupo tena kwenye mahusiano na muimbaji huyo wa wimbo ‘Matatizo’ kauli ambayo ilileta ukakakasi cha mashabiki wakidhani huwenda ikawa ni kiki.

Jumamosii hii malkia huyo wa filamu alirudi tena na kuweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano Harmonize na kudai habari zinazoendelea katika mitandao kwamba wapo pamoja sio za kweli.

“Kuna watu wengi napokea simu zao na wengine mmekuja hadi dukani kuniuliza kama mnayoona niya kweli au lah wengi nimewaambia sina la kusema ila baada ya kutafakari nimeona bora niwaambie upande wangu. Since i’m young yaani hata ukiuliza wanaonizunguka watakuambia mi napenda mapenzi, na naheshimu sana mahuasiano. Yaani kutoka rohoni usanii pembeni as a person mimi Jacky ukiniona niko na mtu na nimemuweka hadi public basi ujue nina mapenzi nae kingine nina moyo wa nyama ninayo ambayo naweza kubeba kifuani mengine siwezi kuumizwa moja wapo,” aliandika Wolper Instagram.

Aliongeza, “Yaani nawaapia mimi kitu kidogo naweza kikanikaba rohoni nikawa naumia muda wote. Halafu ikishakuja kwenye maumivu siwezagi tena drama, naongeaga ukweli hata uwe wa aina gani, mashabiki zangu nyie mashahidi ninaelezeaha story nzima pasipo kuficha japo yaweza kuwa na aibu ama vitu nilivyokua navumilia yakinishinda naongeaga. Kwa sasa hivi naugulia moyoni. Hizi drama na story za kutunga zinazoendelea please please.. naomba! Heshimuni feelings zangu na mimi nina moyo, naombeni nideal na hili personal kwanza nikiweza kulimeza nitawashirikisha. Hayo mengine mnayosIkia nawahakikishia ni drama tu na kiki ambazo watu wanajitengenezea story wapate listeners, followers na likes,”

Mtoto wa ajabu!! soma jeuri ya huyu mwanafunzi...kujibu maswali




Dogo wa darasa la tatu anataka apelekwe darasa la 5.. Mwalimu wa darasa akamfikishia habari mwalimu mkuu wakamwita kwa maswali..

.
M/MKUU:
Wewe ndio Samweli?.
.
SAMWELI:
Ndio mimi mwalimu.
.
M/MKUU:
Mwalimu yeyote amuulize swali Samweli.
.
Mwalimu # Vero akaanza na maswali
.
MWALIMU:
Ni vitu gani ambavyo Ng'ombe
anavyo vinne lakini mimi ninavyo viwili?.
.
SAMWELI:
Miguu.
.
MWALIMU:
Unanini ndani ya kaptura yako
lakini mimi sina?.
.
SAMWELI:
Mifuko ya kaptura.
.
MWALIMU:
Ni kitu gani kimezungukwa na manyoya cha mviringo na kina maji mweupe?.
.
M/mkuu akiwa katumbua macho.
.
SAMWELI:
Nazi.
.
M/mkuu akashusha pumzii!!..
.
MWALIMU:
Nikitu gani huingia mwilini kikiwa kikavu na hutoka kimelowa?.
.
M/mkuu jasho jembamba likiwa linamtoka.
.
SAMWELI:
Jojo Au Bigiji.
.
MWALIMU:
ni neno gani huanzia na F na huishia na K pia kama usipopata utatumia mikono yako.
.
SAMWELI:
Fork "uma".
.
MWALIMU:
Ni kitu gani kila mwanaume anacho, nikirefu kwa wanaume pia nikifupu kwa wengine. Mapadri na Ma papa hawakitumii na mwanaume humpa mwanamke wake baada ya kuoana?.
.
M/mkuu akiwa anataka kumsimamisha dogo asijibu Samweli akajibu.
.
SAMWELI:
Jina la Ukoo (surname).
.
MWALIMU:
Ni sehemu gani katika mwili wa Mwanaume haina mifupa, Lakini ina misuli na mistari kama ya maboga?.
.
.M/mkuu akiwa anahaha na maswali magumu.
.
SAMWELI:
Moyo.
Mwalimu Mkuu akadakia. "Huyu kijana apelekwe Sekondar"...
.
.
NAJUA WEWE MASWALI YANGEKUSHINDA MAANA AKILI ZAKO UNAZIJUA MWENYEWE...

Zitto Atoa Tamko la Kumsulubisha Rais Magufuli Bungeni,Ampa Onyo Juu ya Njaa..!!!



Watanzania wakifa njaa tutamwajibisha Rais kwa mujibu wa Katiba ibara ya 46A 
(Sehemu ya Hotuba ya Kiongozi wa Chama katika Mkutano wa Kampeni za Udiwani - Kijichi) 15/1/2017


Pamoja na masuala haya ya uchaguzi mdogo hapa Kijichi ninaomba nizungumzie masuala machache ya kitaifa. Nafanya hivi kwa sababu baada ya siku saba hatutakuwa tena na nafasi ya kuzungumza majukwaani kama viongozi wa vyama vya siasa kwa sababu ya zuio lisilo la kikatiba ambalo limewekwa na Rais dhidi ya mikutano ya hadhara. Hivyo, sisi tuliamua kutumia majukwaa haya ya kampeni za uchaguzi mdogo kuzungumzia mambo ya kitaifa pia. Hatujui chaguzi ndogo nyengine zitakuja lini.
 
Tulitumia mikutano hii ya kampeni kuelezea hatari ya njaa ambayo inaikabili nchi yetu hivi sasa. Nikiwa katika kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro nilieleza kuhusu kupanda kwa bei za vyakula na kiwango kidogo cha akiba ya chakula kwenye maghala ya Taifa (NFRA). 

Tunashukuru kwamba suala hili limekuwa ni ajenda ya Taifa hivi sasa na tunawapongeza sana viongozi wetu wa dini kwa kutoa matamko ya kuhamasisha watanzania kuliombea Taifa kuepukana na adha ya njaa. Viongozi wa dini wameonyesha utu na uwezo mkubwa wa uongozi wa kutafuta jawabu la mwenyezi mungu kuhusu adha hii.
 
Serikali kupitia kwa Rais imewaambia watanzania kuwa hali ni shwari kabisa na kwamba Serikali haitatoa chakula cha msaada kwa sababu "Mzee Bure" ameshatoka madarakani. Lakini Rais pia alituhumu wanasiasa na wafanyabiashara kwamba ndio wanachochea hali ya njaa kwa kupitia vyombo vya habari kadhaa. Na akaenda mbali zaidi kwa kufikia hatua ya kutisha vyombo vya habari na kusema siku zao zinahesabika, kosa lao kubwa likiwa ni kuandika yale ambayo yeye hayapendi.
 
Sisi ACT Wazalendo tunamsihi Rais awe msikivu. Hii ni nchi ya kidemokrasia na watu wana uhuru wa mawazo. Haiwezekani kila mwenye mawazo tofauti awe ni mtu anayehongwa au mpiga dili. Kazi yetu sisi kama chama cha upinzani ni pamoja na kuikosoa Serikali iliyopo madarakani na kuonyesha sera mbadala kwa wananchi.
 
Tutaendelea kuichokonoa Serikali mpaka ianguke, maana ndio kazi yetu ili kuondoa sera mbovu zilizopo na kuweka sera bora.
Tumesema hili la njaa katika kutekeleza wajibu wetu, Rais na Serikali wamejibu na kufunga mjadala. Wakati utaamua na kuonyesha mkweli nani na mpiga propaganda nani. 

Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao. 

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.
 
Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni. 

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.
 
Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais. 

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais. Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.
 
Tunayasema haya kwa Uzalendo mkubwa kwa nchi, sisi kama chama, ACT Wazalendo, tulimwunga mkono Rais toka mwanzo wa utawala wake na kumkabidhi Ilani ya uchaguzi ya chama chetu kama ishara ya kwamba uchaguzi umekwisha na sasa tujenge nchi yetu. Hatujutii kumwunga mkono kwa sababu kuna mambo mazuri amefanya kuhusu nchi yetu. 

Rais amefanya kazi nzuri ya kupambana na rushwa na ufisadi nchini. ameondoa hali ya ‘impunity’ iliyokuwa imeshika mizizi nchini. Hatua kubwa alizochukua za kuwajibisha watendaji na Waziri aliyekiuka maadili ya kazi tunaziunga mkono. 

Hata hivyo, nchi huendeshwa kwa zaidi ya kutumbua majipu. Kuna uchumi unapaswa kuendeshwa ili watu waweze kujenga maisha yao. Rais anaelekea kushindwa kwenye eneo hili la 'Menejimenti' ya Uchumi kutokana na matamko yake ambayo yanakimbiza uwekezaji na hata mahusiano yetu na mataifa mengine duniani. 

Rais bado anahutubia kana kwamba bado tupo kwenye kampeni. Huu ni mwaka 2017, ni muhimu, ajielekeze katika kujenga uchumi wetu ili kutengeneza ajira kwa wananchi wake.
 
Vile vile, sisi tunaona Rais anahangaika na majipu madogo na kuacha majipu makubwa yanayoathiri uchumi wetu na kupoteza fedha nyingi sana za nchi yetu. Kwa mfano, Rais ameacha kabisa kushughulika na ufisadi mkubwa wa IPTL ambapo kila mwezi TANESCO inalipa shilingi bilioni 8 kwa kampuni ya kitapeli ya PAP. Moja ya sababu za TANESCO kutaka kupandisha bei ya umeme ni kwa ajili ya kupata fedha za kulipa PAP. 

Rais amemfukuza kazi Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akijua kuwa Mkurugenzi huyo alikuwa anatekeleza mpango wa Serikali. Barua ya Waziri wa Nishati na Madini kwenda kwa Waziri wa Fedha kuhusu kupandisha bei ya Umeme imenukuliwa kwa Rais. Hivyo Rais alikuwa anajua kuwa bei ya umeme itapanda na Serikali imeijulisha hivyo IMF katika barua yake ya Disemba 20, 2016, siku 10 kabla ya Tamko la EWURA la kupandisha bei ya umeme. 

Jambo hili kubwa la IPTL ambalo lilihusisha mabilioni ya fedha kuchotwa Benki Kuu Rais analiacha na hataki kabisa kulizungumzia, maana yake ni kwamba Rais anaogopa wakubwa na kuonea wadogo, amemtumbua Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO kwa sababu tu EWURA imetangaza bei mpya ya umeme ambayo Serikali yenyewe iliagiza kupandishwa toka mwezi Septemba mwaka 2016. 

Lakini Rais huyu huyu anaendelea kutetea mkataba unaowalipa matapeli shilingi bilioni 8 kila mwezi. Rais wa wanyonge anawalinda matapeli wanaoiba fedha za umma.
 
Lingine ambalo Rais anaonyesha woga kwa wakubwa ni lile la mkopo wa Hati Fungani kutoka Benki ya Standard ya Uingereza. Serikali ilikopa dola milioni 600 mwaka 2013 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Licha ya mkopo ule kugubikwa na ufisadi katika upatikanaji wake, Serikali imeanza kuulipa na deni litakapokwisha baada ya miaka 6 itakuwa imelipa dola milioni 983. 

Lakini sheria zote za kimataifa zinaibeba Tanzania kwamba kama mkataba na kampuni za kimataifa umepatikana kwa rushwa, nchi inaweza kukataa kulipa deni. Niliiambia serikali Bungeni kuhusu jambo hili na nimepeleka maswali kama manne bungeni kuhusu jambo hili lakini Serikali inaogopa hata kujibu maswali husika. Kwa sababu gani? Serikali inaogopa makampuni ya kigeni. 

Najua kuna kesi mahakamani na sitaki kuingilia kesi hiyo. Lakini hiyo kesi iliyopo mahakamani na hao waliopo rumande ndio wangekuwa mashahidi wa Serikali kwamba Benki ya Standard ya Uingereza ilitoa rushwa kupata biashara nchini na hivyo Serikali ingeishitaki Benki hiyo na kukataa kulipa mkopo huo. Rais na Serikali yake hata kujibu maswali ya bunge wanaogopa. Sisi tunamtaka Rais ahangaike na mambo haya makubwa na aachane na watu wadogo. Rais ni mtu kubwa sana na akitumia ujasiri wake vizuri anaweza kuokoa nchi dhidi ya deni kubwa la kifisadi la Standard Bank ya Uingereza.
 
Lingine nataka kuongea nanyi ni suala la Bajeti ya Serikali na Utekelezwaji wake. Serikali ilileta Bungeni Bajeti ya matumizi ya shilingi 29.5 trilioni mwaka 2016/17. Katika hiyo, ilitarajia kupata mikopo na misaada kutoka nje pamoja na mikopo ya kibiashara ya shilingi 5.7 trilioni. Kutokana na mahusiano mabaya kati ya Serikali na nchi marafiki, mpaka sasa nusu ya mwaka wa Bajeti imekatika na Serikali haijaweza kupata hata thumni katika matarajio hayo. Vile vile Serikali imeanza kukusanya chini ya matarajio kwenye kodi na mapato yasiyo ya kikodi. 

Miradi ya Maendeleo imechelewa kutekelezwa kwa sababu Serikali inafanya kazi ya kulipa mishahara na kulipa madeni tu. Ndio maana miradi mingi inayozinduliwa hivi sasa hakuna mradi mpya bali ni miradi iliyoachwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Serikali hii inahitaji kurekebisha mahusiano yake na nchi marafiki zetu ili uchumi wetu usisimame. Masuala haya Rais hawezi kuambiwa na Mawaziri wake kwa sababu amejenga hulka ya kuogopwa. Sisi wa Upinzani ni lazima tumwambie maana ni wajibu wetu.
 
Katika Barua (letter of intent) ambayo Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu wameandika kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Serikali inasema inataka kukopa mikopo ya kibiashara (syndicated loans and Eurobond) ili kupata fedha. Hata hivyo Mabanki ya Dunia yanataka kujua 'Credit Rating' ya Serikali yetu. 

Hiyo pekee itachukua miezi mingi iwapo mfumo wa kawaida wa zabuni utapaswa kufuatwa. Hata hivyo IMF wameiambia Serikali kuwa soko la mikopo ya dunia hivi sasa ni baya maana Serikali itakopa kwa gharama kubwa, mpaka riba ya 9% kwenye fedha za kigeni. 

Serikali inataka kuiingiza nchini kwenye madeni ghali kwa sababu tu ya kutaka kufanikisha Bajeti isiyotekelezeka, iliyotungwa kwa sifa bila kuzingatia uhalisia wa nchi yetu. Kwa maoni yetu sisi ACT Wazalendo, Bajeti ya Serikali haikupaswa kuzidi shilingi 24 trilioni. Ushauri wetu kwa Serikali ni kuitaka ikae chini na kuleta Bajeti ndogo Bungeni ili kurekebisha Bajeti iliyoko kulingana na uwezo wetu kama Taifa ili kujiepusha na mikopo ghali itakayoumiza wananchi.
 
Serikali ilitangaza kuwa ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa utaanza mwezi Disemba mwaka huu kwa msaada kutoka nchi ya China. Leo ni mwezi Januari hata zabuni ya kampuni iliyoshinda kutekeleza mradi huo Serikali haijatangaza. Hata hivyo tumesikia kuwa kampuni kutoka Uturuki imeshinda zabuni hiyo na China (ambao ndio watoa mkopo wa mradi husika) wamekasirika na wamegoma kutoka fedha zao. 

Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa Rais wa Uturuki anakuja nchini wiki ijayo. Hatukatai kuimarisha mahusiano na Uturuki, lakini ni muhimu Serikali ijitazame upya kuhusu mahusiano yake na China. China ni rafiki wa Tanzania wa misimu yote. Tanzania imekuwa na China muda wote na China imekuwa na Tanzania muda wote. Maamuzi ya Serikali ya kutozingatia taratibu za China katika masuala ya mikopo yanaweza kugharimu sana mahusiano yetu ya zaidi ya miaka 50. 

Tunamsihi Rais awe makini sana na mwenendo wake wa kutojali misingi imara ya Sera yetu ya mambo ya nje. Serikali ikae chini na China kutazama upya suala la Reli ya Kati vinginevyo hatutajenga Reli hiyo, ama itachukua miaka mingi sana kuijenga Reli hiyo. Madhara ya kuchelewa kujenga Reli ya Kati ni makubwa mno kwani washindani wetu wa kibiashara, Kenya, wanamaliza Reli yao sasa kuunganisha na nchi za Rwanda na Mashariki ya Kongo.
 
Namkumbusha Rais na Serikali namna ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani walivyovunja misingi yetu kadhaa ya Sera ya Mambo ya Nje, hasa kuhusu Sahara Magharibi na Mashariki ya Kati. Tumeikumbatia Moroko kwa ahadi ya viwanja vya mipira na misikiti na kuwaacha wananchi wa Sahara Magharibi ambao Mwalimu Nyerere aliwalinda kwa gharama zote. Juzi juzi kwa mara ya kwanza tumewasaidia Israel kwenye Umoja wa Mataifa bila ya kujali msimamo wetu wa 'Two States Solution' kati ya Palestine na Israel. 

Sasa tunakwenda kuweka nyufa kwenye mahusiano yetu na China. Serikali ijitazame upya. Tanzania haikuanza na awamu ya Tano, nchi hii imekuwapo na itaendelea kuwapo. Hatuwezi kukaa kimya tukiendelea kuona misingi ya nchi yetu inavunjwa vunjwa. Lazima tukemee.
 
Mwisho ni haya masuala ya Demokrasia. Juzi nilipokuwa Kahama nimezungumzia suala la ubinywaji wa demokrasia na kuwaweka ndani wawakilishi wa wananchi kwa makosa yanayodhaminika. Nilionya kuhusu tabia ambayo imeanza ya kuitumia mahakama kutekeleza matakwa ya kisiasa ya Serikali. 

Wakati mbunge wa Arusha Mjini bado angali kizuizini, Mbunge wa Kilombero amehukumiwa kwenda jela miezi 6 kwa kosa ambalo lina adhabu ya faini. Kuna maamuzi ya mahakama ya rufaa kuhusu kwamba kosa lenye faini, faini ndio adhabu stahili na sio kifungo. Lakini kwa kuwa lengo ni kukomoa wanasiasa wa upinzani Mbunge wa Kilombero ameswekwa jela. 

Narudia kutoa wito kwa Serikali kuwa makini sana na chuki inazozijenga kwa wananchi kutokana na uonevu huu. Ninaamini kuwa vyama vya siasa vyenye wabunge hao pamoja na taasisi za kutetea haki zitashiriki kikamilifu kuchukua hatua za kisheria dhidi ya matendo yanayoendelea nchini mwetu hivi sasa. 

Tusiache kuinua mikono yetu kupinga uonevu kwa sababu uonevu wa dola ni mtego wa panya. Tukemee kabla hatujafikiwa pia.
 
Watu wa Kijichi, ninawatakia Uchaguzi mwema hapo Januari 22, 2017. Nina imani kwamba mwaka 2017 tutaweza kupata haki yetu ya kikatiba ya kufanya mikutano ya hadhara ili tuendelee kuwaelimisha wananchi ubaya wa Sera za CCM na ubora wa sera zetu za ACT Wazalendo. Tunawaomba wanaKijichi mumchague ndugu Edgar Mkosamali awe Diwani wenu ifikapo jumapili ijayo. Na tunawaomba WanaKijichi pamoja na Watanzania wote waichague ACT Wazalendo, ifikapo mwaka 2019 watupe mitaa mingi na mwaka 2020 watupe Serikali ili tuweze kuwaongoza kwa kuzingatia Utu, Uadilifu na Uzalendo.
 
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam 
Januari 15, 2015

KKKT Nao Watoa Tamko Juu ya Hali ya Njaa Nchini,Waitaka Serikali Ifanye haya



Serikali imeombwa kufanya tathmini ya haraka kubaini upungufu wa chakula nchini uliosababishwa na ukame wa muda mrefu.


Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo ametoa ombi hilo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Meru, Elias Nassari katika Usharika wa Usa River, Wilaya ya Arumeru.

Amesema Serikali haitakiwi kungoja hadi watu wafe ndiyo waanze kutafuta chakula.

Dk Shoo ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Tarcisius Ngalalekumtwa kuwaandikia maaskofu wote wa kanisa hilo kuwataka waumini wao wafanye maombi, hija, mfungo kwa lengo la kukabiliana na ukame unaolikabili taifa.

Vilevile, hivi karibuni Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) lilitoa wito kama huo kwa waumini wake, huku Serikali ikisisitiza kuwa hakuna njaa nchini na kuwa haitatoa chakula cha msaada.

Saturday, January 14, 2017

Mapokezi ya Diamond Gabon Yatisha,Apokelewa na Rais wa Nchi Hiyo

diamond-5



Diamond akiwa katika picha ya pamoja na Rais Ali Bongo wa Gabon pamoja na msanii wa Nigeria, David Adekeye ‘Davido’, Akon pamoja na wasanii wengine na watoto nchini humo.


diamond-2

diamond-3
Rais wa nchi Gabon, Ali Bongo akisalimiana na Diamond Platnumz.


diamond-4
Diamond Platnumz akisalimiana na Akon. 


:Harusi za Gharama Kubwa, Sherehe Mahotelini Vyapigwa Marufuku ..!!!




Mji wa Bula Hawa nchini Somalia umepiga marufuku harusi za gharama ya juu ili kuwashawishi vijana wengi zaidi kuoa.


Kamishna wa Mji wa Bula Hawa uliyo karibu na mpaka wa Kenya, Mohamud Hayd Osman amesema kwamba, mbuzi wasiozidi watatu ndio wanaofaa kuchinjwa pekee ili kuwalisha wageni na kwamba sherehe katika hoteli hazitaruhusiwa.

Amesema kuwa mahari itakuwa chini ya dola 150 (sawa na TZS 350,000/=) pekee ambapo uamuzi huo umekuja baada ya maafisa kubaini kwamba takriban watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa hivi karibuni

Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio maswala yanayowafanya watu kulihama eneo hilo.

Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia.

“Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini,”alisema Osman.

Hatua ya kupunguza matumizi kuhusu sherehe za kifahari pamoja na matumizi mengine baada ya ya maafisa kugundua kwamba ni kwa nini watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa mjini humo. Wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha, alisema.
Powered by Blogger.