Monday, November 30, 2015

Daraja juu ya Bahari Dar es salaam… Rais Magufuli alivyohakikishiwa ujenzi wake leo.

Daraja la salender

Vichwa vya habari za siasa Tanzania bado vinaendelea kubeba stori kila mara kuhusu Rais Magufuli… inawezekana ni kawaida kabisa kila siku kukutana na habari zaidi ya tatu au nne kuhusu Rais Magufuli tangu siku ya kwanza alipoapishwa na kuanza kazi ya Urais wa Tanzania.
MAGUFULI
Rais Magufuli akionesha ramani ya daraja la Salender, enzi hizo alikuwa Waziri wa Ujenzi.
Ninayo nyingine kutoka Ikulu sasahivi, hii inahusu Rais Magufuli kumuaga Balozi wa Korea Kusini, Chung IL ambapo Balozi huyo amemhakikishia Rais Magufuli kwamba daraja hilo litajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini.

Sunday, November 29, 2015

Matokeo Ya Ligi Kuu Ya Uingereza (English Premier League)

original

Msimamo Wa ligi Kuu Ya Uingereza

#TeamMPWDLFAGP
1Manchester City149233014+1629
2Leicester City148512921+829
3Manchester United148422010+1028
4Arsenal148332412+1227
5Tottenham Hotspur146712411+1325
6Liverpool146531815+323
7Crystal Palace147161914+522
8West Ham United146442521+422
9Everton145632719+821
10Southampton145542017+320
11Watford145451516-119
12Stoke City145451114-319
13West Bromwich Albion145361318-518
14Chelsea144371723-615
15Swansea City143561419-514
16Norwich City143471725-813
17Sunderland143381626-1012
18AFC Bournemouth142481730-1310
19Newcastle United142481430-1610
20Aston Villa1412111227-155

Matokeo Ya ligi Kuu Ya Uingereza

November 29, 2015
Liverpool1 - 0Swansea City
Norwich City1 - 1Arsenal
West Ham United1 - 1West Bromwich Albion
Tottenham Hotspur0 - 0Chelsea



By, Shaibu Kibiki - Hapa Kazi tu BLOG

WAZIRI MKUU MH> KASSIM MAJALIWA AIBUKA KANISANI ATOA KAULI NZITO KWA WATANZANIA

Waziri Mku Mh. Kassim Majaliwa


Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa meza kuu na viongozi wa kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015.





Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2015.
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.
Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida. “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015. 
“Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza. 
Akinukuu kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu ili watu wetu wasigue,” alisema.
Aliwataka viongozi wa kanisa hilo waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo 

taendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote.
Alisema wao kama kanisa wanaamini kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu inapatikana kwenye neno la Mungu.
Akisoma risala ya kanisa hilo, Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu walewale isipokuwa katika malengo tofauti. 
Alisema kanisa hilo linahubiri maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa watu kufanya kazi. 
Akisisitiza kuhusu uadilifu, aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto hawawezi kuwa waadilifu. 
“Wazazi tunao wajibu wa kupanda mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna tunachopanda.”
“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao, ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema yanaanzia nyumbani,” alisisitiza.



BREAKING NEWS:HAPA KAZI TU YAZUIA MAKONTENA YA BAKHRESSA

Mamlaka ya Mapato Tanzania imezuia kampuni ya Bakhresa kupeleka makontena yake katika bandari yake kavu.
Hii ni kutokana na baadhi ya makontena kugundulika kuwa yalipitishwa bila kulipa kodi.

Tukumbushane; Utumishi Wa Umma Na Swali La ' Nani Atauzima Mshumaa Wa Serikali?'

Ndugu zangu,
Kuna wakati Mama Maria Nyerere alipata kuulizwa swali la kukera kutoka kwa mwandishi kijana.
Mwandishi huyo alimuuliza Mama Maria Nyerere: “Hivi, inakuwaje Mwalimu ameondoka na kuacha familia yake ikiishi katika hali ya kawaida sana bila kuwa na mali nyingi wakati tunaona watendaji wa siku hizi wana mali na wengine wanasomesha watoto wao nje ya nchi?”
Mama Maria Nyerere alimjibu mwandishi yule: “Naona wewe bado ni kijana sana, hukuwepo wakati
ule wa Azimio la Arusha, lakini hiyo si sababu ya wewe kushindwa kufahamu ya nyuma, maana ulitakiwa kusoma.
Wakati wa Mwalimu kulikuwa na Azimio la Arusha na miiko ya viongozi. Na Mwalimu kama kiongozi, asingeweza kufanya tofauti na yale ambayo aliyasimamia na aliwataka wenzake katika uongozi wayafuate.”
Ndiyo, katika utaratibu wa sasa, na hasa baada ya kuondokana na kanuni, miiko na maadili ya uongozi ya enzi za Mwalimu, ni kawaida kukuta Watendaji wenye miradi ya biashara, mashamba na hata viwanda ambavyo wao wenyewe ndio wasimamiaji.
Hivi, Waheshimiwa hawa watapata wapi muda wa kusimamia biashara, mashamba na viwanda vyao kama si kuiba muda wa kuwatumikia wananchi na hata kutumia rasilimali za umma?
Inahusu swali hili; Ni nani atauzima mshumaa wa Serikali? Hapa kuna kisa nilichopata kusimulia.
Naam, miongoni mwa viongozi waliopata kuongoza dola ya Kiislam, hususan baada ya Mtume Muhammad (SAW) na baada ya masahaba, ni Amir muumini na Khalifa Umar bin Abdulaziz.
Wanazuoni wa Kiislamu wanatwambia, kwa utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz ulijaa uadilifu. Si kwa viongozi tu, hata kwa raia wake.
Inasemwa kwamba moja ya mafanikio makubwa ya utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz, ni kukusanya zakka. Katika Uislamu, zakka ni ibada ya lazima kwa mwenye nacho kuwapa masikini, yatima, wajane, wasafiri, raia na wengineo wenye kuhitaji.
Watu walijengewa imani kubwa, kiasi hakuna aliyethubutu kukwepa kutoa zakka. Hata wale waliopokea zakka walikuwa waadilifu, hawakupokea zakka mara mbili kama walishapokea kabla. Wote waliostahili kupata zakka , walipata zakka. Hakika, zakka zilitolewa zikajaa mabohari.
Siku moja raia mmoja alikwenda kwenye ofisi ya Khalifa Umar bin Abdulaziz. Wakati wa maongezi yao, Khalifa Umar alikuwa akihangaika kuupuliza na kuuzima mshumaa mmoja na kuwasha mwingine.
Alikuwa na mishumaa miwili mezani. Kadri mazungumzo yalivyoendelea, Umar aliendelea kufanya hivyo. Alipuliza mshumaa mmoja ukazimika, kisha akawasha mwingine.
Jambo hilo lilimstaajabisha sana mgeni wa Khalifa Umar bin Abdulaziz. Akauliza: "Je; ni kwanini unazima mshumaa huu na kuwasha mwingine, kisha huo nao unauzima na kuwasha ule wa kwanza?
Khalifa Umar bin Abdulaziz akamjibu: "Mshumaa huu ni wa Serikali, wewe unaponiuliza habari za Serikali, nauwasha. Lakini naona mara unauliza habari za familia yangu, ndiyo maana nauzima wa Serikali na kuuwasha mshumaa wangu mwingine nilioununua kwa pesa za mfukoni mwangu. Nachelea nisije fanya dhuluma kwa mali ya nchi."
Ndugu zangu,
Bila shaka, hicho ni kisa chenye kutupa mafundisho muhimu
juu ya dhana nzima ya maadili katika utumishi wa umma. Tafakari!
Maggid,
Iringa.

HAPA KAZI TU” YAWAWEKA SAWA WAFANYAKAZI WA DAWASCO.


 Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano na wafanyakazi uliofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Dawasco jijini Dar es Salaam kuhusu utendaji kazi wa kazi.
 Wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wao.


Na Mwandishi Wetu

Ule usemi maaarufu wa Hapa kazi tu” 

unaendelea kuimbwa na kufanyiwa kazi na watanzazia wengi hususani watumishi wa Umma na serikali ili kuendana na kasi ya awamu ya Tano ya Raisi Magufuli. Kauli mbiu hiyo imekumbushwa tena na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha pamoja na  wafanyakazi wa shirika hilo mapema wiki hii.
“lazima tuendane na kasi na speed ya Mheshimiwa Rais, tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, kutojali malalamiko ya Wateja sasa ni mwisho” aliongeza Luhemeja
Aliwataka wafanyakazi kujali muda wao wa Kazi kwa kutenda yale ambayo yataondoa kero ya Maji kwa Wateja hususani kuziba mivujo ya Maji katika maeneo mengi ya Jiji pamoja na kupambana na wizi wa Maji ili kila mwananchi apate huduma ya Maji kihalali.
Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa DAWASCO kutekeleza kauli ya Rais aliyoitoa mapema wakati akifungua Bunge katika sekta ya Maji pale aliposema “LAZIMA TUWATUE KINA MAMA NDOO KICHWANI” kwa kuhakikisha huduma ya Maji inamfikia mwananchi na kuondokana na malalamiko ya upatikanaji huduma hiyo kwa maeneo stahili.
  Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)


Saturday, November 28, 2015

KENYA WAMTAMANI MAGUFULI

Something very special is happening in Tanzania after their most recent election. Our Southern neighbour got a new president called John Pombe Magufuli from the ruling Chama Cha Mapinduzi party in spite of there being serious competition from the opposition for the first time since independence.
When the new president was inaugurated, he immediately swung into action as his election tagline "hapa kazi tu" promised. On his first day on the job he visited the Muhimbini National Hospital, their national referral hospital equivalent to our Kenyatta Hospital, and found patients sleeping on the floor with equipment that was not working. He immediately fired the management of the hospital and within days the available equipment was fixed. He followed this quickly buy stripping down his inauguration party and insisted the excess monies for the event be used to buy beds for patients at Muhimbini Hospital.
As we were just recovering from this magnanimous act, more reports started filtering in of his work from the Southern border. This all-action hero president had gone all out to ensure his government cut out excessive spending. Thus he was cancelling foreign trips for all levels of government, putting an end to seating allowances and ending retreats when there were offices available. Then the biggest story came through as he cancelled elaborate celebrations for Uhuru Day, the country's Independence Day. He instead instructed that the money planned for the fete be used for cleaning the country - he didn't see the need for celebrating when people were suffering from cholera.
 was a revolution at our doorstep, nothing like our dynamic duo turned world travelling selfie presidency that we have got used to here. While our president seemed to be having problems with cutting back on excesses in his administration, we as individuals can try and do things in our own lives to channel our 'inner Magufuli'. This is by stating aloud: "What would Magufuli do?" whenever one is about to embark in a course of action that will affect our financial lives and asking ourselves like some do for a popular religious figure.
The first step this saving cash crusade has to start with our families as this is where we spend a huge proportions of our income on. Let's start with these graduations for young kids who are leaving kindergarten and are now going to 'big school' for the first time in November. In days gone by, this transition wouldn't be heard of because it was a cost that no parent in their right mind could have invested in. After all kids are known not to remember these things at older ages anyway. Today social media channels are filled with parents hosting more and more elaborate events for these kids in their mini graduation gowns which just won't do in these austerity friendly days. What would Magufuli do in such a situation then? Following his lead you would insist that on finishing kindergarten, all a child would expect is a favoured meal cooked by one parent and a handshake or hug from their other parent. The monies saved would be invested in the child's primary and high school education.
It's not just the kids who will be enjoying the new austerity measures as even the significant other will also be feeling the heat of the "hapa kazi tu" mantra. Gone from the family calendar are ostentatious spending habits for both her birthday and your wedding anniversary to save hundreds of thousands of shillings. What is the use of people having expensive gifts when there are husbands suffering from the burden of paying for it all?
One of the most important ways of ensuring one's 'inner Magufuli' is channeled, is cancellation of external drinking done by husbands to cut down on huge family budgets. This means that henceforth, drinking at places with fancy names ending in "lounge" or "Bistro" will be removed from the lexicon while using taxis at night will be banned. Instead the method will be buying drinks from the supermarket at as close as recommended retail prices as possible while drinking at home will be employed.
With these methods you can be sure to find a more conducive home budget for the income that is earned therein. However, knowing the way Nairobians operate, these reforms will quickly end when the child of the wannabe Magufuli starts wailing about them needing their kindergarten graduation party. It will go so badly that the budget won't go down as hoped but triple, leaving the family living in debt.
Powered by Blogger.