Friday, February 10, 2017

Hivyo Joti amkana Gigy money mchana kweupee!!!!



Baada ya Mtangazaji wa ChoiceFM, Gigy Money kuonekana akimpost mchekeshaji Joti na alipoulizwa na Soudy Brown kwenye U heard iliyopita alikiri kuwa mapenzini na Joti.

Sasa leo kupitia XXL ya clouds FM, Mtangazaji Soudy Brown kwenye U heard amepiga stori na Joti ili kuujua ukweli, haya yalikuwa majibu yake. ‘Mimi kwa heshima ambayo nimeitengeneza na watu wangu ninaofanya nao kazi  halafu wewe unataka kuiharibu kwa mara moja, huyo Gigy unayemzungumzia picha ambazo amepost umeona picha ambayo mimi nafanya nae mapenzi?” 

“Mimi siilewi…………mimi nina mke wangu, nina familia yangu, mbona unataka kuniweka kwenye maisha ambayo wanaishi watu, mimi siishi huko’ – Joti

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.