Sunday, January 29, 2017

Breaking News: Waliofukiwa na Kifusi Mgodini Geita Waokolewa Wote



WATU 15 waliofukiwa kwa kifusi katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita, wameokolewa wote wakiwa hai kutokana na  jitihada zilizofanywa na wataalamu wa mgodi huo na mingine kwa kushirikiana na serikali.



Habari zilizotufikia punde ni kwamba watu hao wameokolewa baada ya kukaa takribani siku tatu ndani ya mgodi bila kupata chakula na bila kuona mwanga wa jua.



Aidha, taarifa za awali zinasema kuwa baada ya kuokolewa watu hao  wamewekwa chini ya uangalizi wa 
karibu na wataalamu wanaendelea na uchunguzi huo ambapo baada ya muda itatolewa ripoti kamili.



Thursday, January 26, 2017

Inahuzunisha Sanaa..!! Mtoto Ambaka Mama`ke Hadi Kifo ,Stori Kamili Hii Hapa..!!!



Dunia imekwisha! Hiyo ndiyo lugha nyepesi na rahisi unayoweza kuitumia kuelezea tukio hili. Januari 11, mwaka huu Tambani, Mbande wilayani Temeke jijini hapa, kijana mdogo, Hamis Lutani Kilumbi (21) anadaiwa kumbaka mama yake mzazi, Fatuma Mohammed Matutu (48) sambamba na kumchoma visu shingoni hali iliyomfanya apate maumivu makali hadi kufariki dunia Januari 21, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


dsc02127

Kaka wa mtuhumiwa
HII HAPA SIMULIZI YAKE

Akizungumza kwa uchungu na Amani wakati wa mazishi ya mwanamke huyo, mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye Mohammed Ali, alisema kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa ambaye ni mdogo wake anayemfuata kuzaliwa, alifika nyumbani kwao, alipokuwa akiishi mama yake majira ya mchana lakini hakumkuta.


“Baada ya kumkosa mama, alikuja nyumbani kwangu maana si mbali na anapoishi mama. Lakini pia mimi, mke wangu na mdogo wetu wa mwisho wa kike, Asma, ambaye naishi naye hatukuwepo. Kwa hiyo, Hamis aliacha ujumbe kuwa, tukirudi tupewe taarifa yeye alifika na mama alikuwa anatuhitaji.
dsc02074

Kaka wa Marehemu
UJIO WA MTUHUMIWA WATIA SHAKA
“Sasa baada ya mimi kurudi nyumbani na kupewa taarifa hizo nilishangaa sana, kilichonishangaza si kuitwa na mama bali ujio wa Hamis nyumbani kwangu, maana nilikuwa sijaonana naye kwa muda usiopungua mwaka mzima kwa vile tuliwahi kutofautiana nikampiga marufuku kuja nyumbani kwangu na yeye akaahidi akiniona popote atanipiga na nondo,” alisema Mohammed
dsc02079

…Mwili wa Marehemu ukitolewa Mochwari
Hata hivyo, Mohammed alisema baada ya kuuliza juu ya wito wa mama yake, aliambiwa kuwa, Asma alishakwenda nyumbani na hakuwa anawaita kama alivyosema Hamis.

Mohammed akaendelea kueleza kuwa, baada ya maelezo hayo, aliamua kuendelea na mambo yake na alikwenda kutazama mechi ya mpira wa miguu kati ya Simba na Yanga runingani zilizokuwa zikicheza Zanzibar.

MLANGO WAGONGWA, WATOLEWA UJUMBE MBAYA

“Baada ya mechi nilirudi nyumbani na kulala. Jambo ambalo sikulitegemea ni kwamba, kufika usiku wa manane, ilikuwa yapata kama saa 8 hivi, majirani wa nyumbani kwa mama walikuja kunigongea, wakaniambia mdogo wangu Hamis anamuua mama.

“Nilikimbia mpaka eneo la tukio. Kiukweli nilimkuta mama akiwa na hali mbaya, alikuwa akivuja damu sana, kitenge na kanga alizokuwa amevaa vilikuwa vimelowa damu chapachapa.

dsc02078
Mwili wa Marehemu ukitolewa Mochwari

“Niliumizwa mno na hali aliyokuwa nayo mama. Nilimuuliza nini kilimpata na kauli yake ya mwisho alisema; ‘mdogo wako Hamis anataka kuniua.’ Bila kupoteza muda, haraka tulimbeba mama na kumkimbiza kwa mwenyekiti lakini hatukumkuta, tukampeleka kwa mjumbe, akatuandikia karatasi kwa ajili ya kumkimbiza polisi.”

MAJERUHI ALALA NA MAUMIVU
Mohammed alizidi kusimulia kuwa, kutokana na mazingira wanayoishi, haikuwa rahisi kumkimbiza muda huohuo, wakasubiri kupambazuke kwanza na alfajiri walimpeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai, wakaandikiwa PF3 na kisha kumpeleka Hospitali ya Temeke.

MADAKTARI WABAINI MAZITO
Mohammed: “Mama alifanyiwa vipimo na madaktari walithibitisha kuwa, aliingiliwa kinyume na maumbile lakini pia alichomwa visu shingoni. Alianza kupewa matibabu lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya, tukamhamishia Hospitali ya Muhimbili kwenye wodi ya Kibasila. Bado hali ilizidi kuwa mbaya zaidi na Jumamosi ya tarehe 21, alipoteza maisha.”


dsc02081

…Mwili wa Marehemu ukitolewa Mochwari

HUYU HAPA KAKA WA MAREHEMU

Naye kaka wa marehemu, Said Matutu, mkazi wa Mbagala Kokoto, Dar  alisema kuwa, amesikitishwa sana na tukio hilo lililosababisha kifo cha dada yake na kuongeza kwamba, mtuhumiwa anatafutwa na polisi ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Kiukweli hili suala linasikitisha mno, huwezi kumfanyia mama yako mzazi kitendo kama hicho. Huo ni unyama uliopitiliza, mtu wa namna hii ni wa kuogopwa katika jamii,” alisema Said ambaye msiba ulifanyikia nyumbani kwake.

dsc02089
…Jeneza likiandaliwa kuswaliwa.
TABIA ZA MTUHUMIWA
Hata hivyo, kaka huyo aliongeza kuwa, kabla ya tukio hilo alikuwa akipata malalamiko kutoka kwa dada yake (marehemu) juu ya tabia za uvutaji bangi, utovu wa nidhamu na tabia nyingine nyingi mbovu alizokuwa nazo mtuhumiwa, lakini pia aliwahi kuambiwa kijana huyo alikuwa ni mmoja wa vijana wahalifu maeneo ya Posta Mpya


dsc02098

…Mwili ukiswaliwa
MAZISHI YAKE
Marehemu Fatuma alizikwa Jumatatu iliyopita kwenye Makaburi ya Mbagala Mponda na ameacha familia ya watoto wanne, akiwemo mtuhumiwa.

KAMANDA WA POLISI TEMEKE
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, SSACP Gilles Muroto, alipotafutwa na mwandishi wetu na kuulizwa kuhusu tukio hilo, alisema taarifa hizo bado hazijamfikia lakini atafuatilia ili kujua kilichotokea.



Wednesday, January 25, 2017

Elewa A to Z kuhusu mwanaume aliyejinyonga kisa mapenzi,.Mengi yafichuka nyuma ya Pazia. Yadaiwa Kauawa!!


Jumapili mchana, picha za kijana mmoja aliyetambulishwa kama Fredrick Richard zilianza kusambaa mitandaoni, ikidaiwa kuwa amejinyonga, kisa ni mapenzi kwa mwanamke mmoja ambaye alitajwa kwa jina la Rose, kabla ya baadaye jina hilo kurekebishwa na kuwa Mariam.
 
Tukio hilo lililozua gumzo kubwa lilidaiwa kutokea huko Korogwe mkoani Tanga, ikidaiwa kuwa marehemu alichukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa mpenzi wake wa kike, ambaye anadaiwa kuitwa Mariam, aliamua kumuacha na kuolewa na mwanaume mwingine, ambaye alitajwa kuwa anaitwa Robert.

robert-2
Katika ujumbe uliodaiwa kuandikwa na marehemu huyo, alidai kuwa amechukua uamuzi wa kujitoa roho kufuatia mpenzi wake huyo kumuacha yeye na kukubali kuolewa na mtu aliyetajwa kuwa ni Robert, licha ya kuwa alipata huduma nyingi za thamani kutoka kwa marehemu.

Aidha, ujumbe huo ulimtaja Robert kuwa siyo tu ni rafiki wa marehemu, bali ni bosi wake, hivyo aliamua kutumia cheo chake kama fimbo ya kumchapia. Sambamba na madai hayo, kulikuwepo na picha zilizotajwa kuwa ndizo za mwanamke anayedaiwa kumkoroga Fredrick, akionekana mrembo hasa, pia za Robert.

Kama ilivyo ada yake, RISASI MCHANGANYIKO liliamua kuchimba ili kubaini ukweli wa tukio hilo ambalo licha ya kuzua maneno mengi miongoni mwa wachangiaji mitandaoni, pia liliacha simanzi kwa ndugu na jamaa wa wahusika hao.

robert-1

KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alipatikana kupitia simu yake ya mkononi na baada ya kuulizwa kuhusu tukio hilo, alikiri kutokea wilayani Korogwe.

“Taarifa hizo zimenifikia, tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita, katika mtaa wa Mbezi wilayani Korogwe. Katika chumba chake alichojinyongea, marehemu aliacha ujumbe mfupi uliosomeka; 

“Asilaumiwe mtu yeyote, nimeamua kujinyonga mwenyewe kutokana na matendo yangu.”
Hata hivyo sisi tunaendelea kumtafuta mtu aliyeshirikiana naye kufanya hayo matendo kwa sababu hawezi kufanya peke yake,” alisema.

kujiua-2

Mariam.

KUHUSU PICHA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI?

Alipoulizwa kuhusu kama marehemu ndiye ambaye picha yake ipo katika mitandao ya kijamii, alisema amesikia juu ya jambo hilo, lakini hawezi kuthibitisha kama huyo ndiye aliyejinyonga na kuongeza kuwa polisi hawafahamu chanzo cha tukio hilo.

Chanzo chetu cha kuaminika kililidokeza Risasi Mchanganyiko kuwa mtu anayeitwa Robert yupo na ni kweli ndiye aliyeonekana katika picha akiwa kwenye gari, lakini hahusiani na habari hizo hata kidogo. Chanzo hicho kilitoa namba za simu za kaka wa jamaa huyo aliyefahamika kwa jina la Sheck, ambapo alipopatikana, alifunguka hivi;

“Sisi tuna nyumba kule Korogwe, ambako kaka yake Fredrick (marehemu) alikuwa amepanga. Ninamfahamu huyo kijana kwa sababu alikuwa akija pale mara kwa mara, Robert anayetajwa siyo huyo ambaye picha zake zipo mtandaoni, huyu ni mdogo wangu na haishi Korogwe, yupo hapa Dar na ana mke na familia yake.

“Mara ya mwisho Robert kufika hapa ilikuwa ni Krismas iliyopita na hata huyo Mariam mwenyewe hamfahamu, kilichotokea naona watu wanataka tu kumchafua mdogo wangu kwa kufananisha majina.”


kujiua-3

Fredrick, akiwa amembeba mpenzi wake na Mariam, enzi za uhai wake.

UTATA JINA LA MARIAM

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya uhakika wilayani Korogwe, ni kweli kwamba marehemu Fredrick alikuwa akishiriki mapenzi na msichana mwenye jina la Mariam, lakini pia jina hilo ni la dada yake. Baadhi ya majirani wanasema walikuta ujumbe unaodaiwa kuandikwa na Fredrick ukitaka Mariam asihusishwe na kifo chake kwa namna yoyote, hali inayowatia shaka ni yupi aliyelengwa, iwapo ni dada au mpenziwe.

“Sasa inakuwa vigumu kuelewa ni Mariam yupi ambaye anahusika na tukio hili ambaye marehemu alisema asihusishwe. Kama ni dada yake pengine anaufahamu ukweli juu ya kilichotokea, lakini hata kama ni aliyekuwa mpenzi wake, pia hakuna anayejua lolote, kama amechangia katika kifo hicho au la,” kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa mpenzi wa marehemu huyo, ambaye alikuwa akimiliki saluni wilayani hapo ametoweka tokea kutokea kwa tukio hilo.

kujiua-4


HUYU HAPA ROBERT, MSOME ANAVYOSEMA

RISASI MCHANGANYIKO liliweza kumfikia Robert ambaye alikiri kuwa hilo ni jina lake na ndiye mwenye picha zinazosambaa mtandaoni, lakini hana uhusiano wowote na tuhuma zinazotolewa, kwani hata mwanamke anayezungumzwa hamfahamu na hata alipoomba picha zake zaidi na kutumiwa, alishindwa kumtambua.

“Mimi siishi Korogwe na wakati tukio la Fredy linatokea mimi nilikuwa njiani kurudi kutoka Kigoma kuja Dar kikazi. Nimedhalilishwa, nimefedheheshwa sana, nimetukanwa, familia yangu imezodolewa, mke wangu kila anapopita ananyooshewa vidole kuwa mumewe nimesababisha kifo cha rafiki yangu.

“Nimesikitika sana na taarifa za uongo zinazoenezwa mitandaoni ila nashukuru ndugu zake marehemu wamenipigia na kunipa pole na kusema kuwa ukweli wao wanaujua kuwa si mimi ambaye nahusika katika tukio hilo.”

kujiua-5

MSIKIE MARIAM, DADA WA MAREHEMU

RISASI MCHANGANYIKO lilimpata dada wa marehemu, Mariam ambaye alisema Robert asihusishwe na kifo hicho kwani hakuna ukweli wowote. Wala huyo Robert anayetajwa kuwa alikuwa na cheo kikubwa kumzidi kaka yake pia siyo kweli, kwani hakuwa akifanya kazi zaidi ya kuwa mtu wa mishemishe tu za kawaida.

“Mimi ninachoona ni kuwa mdogo wangu ameuawa. Kuna watu watakuwa wamemuua na ili kuficha ushahidi, ndiyo wakamtundika na kuanza kueneza maneno ya uongo mitandaoni.”

FREDRICK NI NANI?

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Fredrick alikuwa ni ofisa mikopo katika Saccos iliyomilikiwa na familia yao, iitwayo Single Microfinance Company akiwa amezaliwa mwaka 1989 na alizikwa Jumatatu katika Kijiji cha Kongoto, kilichopo Butiama mkoani Mara.

kujiua-6

MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA
“Ni kweli tukio hilo limetokea ila habari zinazoandikwa kwenye mitandao ya kijamii nyingi zinaongezewa, zinapotosha ukweli, barua inayosambazwa kuwa imeandikwa na marehemu na ile inayodaiwa kuandikwa na Mariam siyo zenyewe, marehemu aliacha kipande kidogo cha karatasi, sijaona mtu ambaye ameshikiliwa na polisi kuhusu tukio hilo ila nadhani wanaendelea na uchunguzi wao,” alisema mwenyekiti huyo, Rajabu Nzige.
Mwisho


Tuesday, January 24, 2017

Rais Magufuli Kuzindua ‘Mwendo Kasi’ Dar, Kesho..!!



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe anatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa huduma ya mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam siku ya kesho.

Uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika kwenye stendi kuu ya mabasi hiyo ya Gerezani jijini Dar es Salaam, utaanza majira ya asubuhi.

Kwa mujibu wa matangazo yanayotolewa na kampuni inayosimamia mradi huo ya UDART, rais Magufuli anatarajia anatarajiwa kuzungumza na wananchi watakaojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Mabasi ya mwendo wa haraka maarufu kama ‘Mwendo Kasi’ yalianza kazi mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka jana baada ya kukamilika kwa zoezi la majaribio ya utoaji huduma pamoja na kupangiwa njia za kusafirisha abiria

Fanya Mazoezi Haya kwa Wiki Tatu Kuongeza Nguvu za Kiume..!!!




Kuna jambo linanishangaza sana, utakuta mwanaume anapata muda wa kukaa kitako muda wa dakika tisini au zaidi akiangalia mpira, au masaa manne, matano na wengine wanakesha kabisa katika baa wakinywa na kula tu, lakini wanasahau kabisa kutenga muda tena mdogo tu kama dakika tano mpaka nane kwa siku kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume kwa kufanya mazoezi ya kuongeza nguvu za kiume.

Mwanaume anefanya mazoezi ya kuimarisha misuli ya uume hawezi kuwa sawa na mwanaume asiyefanya mazoezi haya sio tu katika kuimarisha nguvu zake za kiume lakini pia kuweza kujitawala katika tendo la ndoa na kuweza kumfikisha mwanamke katika raha ile inayotakiwa.

Mazoezi  haya yakifanywa kwa dhati yanaweza kumpa mtu matokeo mazuri sana ilimradi afuate utaratibu atakao takiwa aufuate.

Hizi ni miongoni mwa faida zinazopatikana kwa kufanya mazoezi haya ni hizi zifuatazo:

Kwanza humpa uwezo mwanaume kuweza kusimamisha uume wake kwa muda mrefu zaidi kuliko ambavyo alikuwa anaweza kuusimamisha  kabla ya kufanya mazoezi haya.

Pili mazoezi haya hufanya mtiririko wa damu kwenye uume uwe mzuri hivyo kuufanya uume uwe na nguvu na kuondoa kabisa tatizo la nguvu za kiume.

Tatu humpa uwezo mfanyaji wa mazoezi haya kukawia kumwaga mbegu hivyo kumpa nafasi mwanamke aweze kufikia katika kilele chake pasi na kumkatishia njiani.'

Vifaa Unavyohitaji

1.   Mafuta ya mizeituni (Olive Oil) au mafuta ya nazi au Alizeti au mafuta ya mgando (gel)

2.   Jiko  lolote ili upate mvuke wa kutosha unaweza kutumia jiko la mchina, stove, au hata la mkaa lakini isiwe moto mwingi uwe kiasi tu lengo ni mvuke

3.   Kitambaa kisafi na laini na maji safi ya uvuguvugu
Namna ya kufanya mazoezi ya Kuongeza nguvu za kiume

1. Loweka kitambaa chako katika maji ya uvugu vugu kisha anza kwa kuusafisha uume wako kwa kitambaa laini cheye maji ya uvugu vugu kama unauchua uume kwa kuuvuta mbele. Fanya zoezi hili kwa dakika tatu.

2.  Pakaa mafuta yako kwenye viganja vyako viwili vya mikono yako kama vile unataka kujipaka mafuta mwilini.

3.  Weka viganja vyako ili vipate mvuke wa moto kutoka katika ama jiko la mchina, stove au kitu chochote utakachotumia. Ukiona viganja vimepata joto kiasi cha kutosha siyo mpaka uungue mikono, kisha

4.  Kamata uume wako ukiwa unauchua kwa kuuvuta mbele kwa nguvu kidogo sana ukianza na mkono wa kulia alafu wa kushoto au kushoto halafu kulia vile utakavyoona inafaa. Joto kwenye mikono likiisha rudisha mikono yako uipashe tena ili ipate joto kisha rudia  kuuvuta vuta tena uume kwa muda wa dakika kumi.
Kumbuka

Mazoezi haya hufanywa mara mbili asubuhi tu mtu ukiamka na wakati ukitaka kwenda kulala na ni kwa muda wa wiki tatu. Utaona matokeo yake

Sunday, January 22, 2017

Baada ya Bilicanas na Shamba, Serikali ‘Yakamata’ Hoteli ya Mbowe Arusha



 Ikiwa ni takribani miezi mitano sasa tangu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe alipoondolewa katika jengo la Bilicanas lililokuwa pia na ofisi za Free Media na siku moja tangu serikali imzuie kuendeleza shughuli za kilimo kwenye shamba lake, kiongozi huyo amepata pigo jingine katika hoteli yake anayoimiliki.

Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amepewa siku 14 na serikali awe amelipa kodi ya hoteli yake ya Aishi takribani TZS milioni 13.5 vingine vyo hoteli hiyo itafungwa.

Hoteli ya Aishi inayomilikiwa na Freeman Mbowe iliyopo Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro





Uamuzi huu wa serikali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekuja siku moja tangu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa alipotangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe kwa madai kuwa lipo katika eneo la chanzo cha maji cha Mto Weruweru.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mujibu wa taarifa alizozipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Freeman Mbowe amekuwa akikwepa kulipa kodi kwa miaka mitano na kusababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato.

Kwa miaka mitano imeelezwa kuwa Mbowe hakupeleka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hali ya mauzo yake ambayo inapaswa kutumika kujua ni kodi kiasi gani anatakiwa kulipa.

Kuhusu shamba lake, DC alisema kuwa shughuli za kilimo katika eneo hilo limepeleka uharibifu wa mazingira huku kiongozi huyo akivuna miti ya asili bila kibali cha Mkuu wa Wilaya kinachotolewa baada ya uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).

MAHABA NIUE: Trump Alivyoonyesha Mahaba Kwa Mke wake Ikulu White House Jana!!




Donald Trump na mkewe, Melania juzi walilionyesha jiji la Washington mvuto wa familia yao  wakati walipopanda kudansi kwenye jukwaa lililopambwa kwa taa za rangi nyekundu, nyeupe na bluu ambazo ni za bendera ya Marekani.

Wimbo wao wa kwanza kwa wawili hao kucheza ulikuwa “My Way (Kivyangu)” wa mwaka 1969 uliorekodiwa na gwiji wa muziki, Frank Sinatra. Lakini katika sherehe ya juzi, kibao hicho kiliimbwa na nyota wa muziki wa jazz, Erin Boheme.

Melania Trump alivutia waalikwa kwenye sherehe hiyo alipoibuka na gauni lake jeupe la kung’aa, lililoacha mabega wazi, lakini lenye mikono ya mchinjo, na refu hadi kufikia kifundo cha mguu, lakini likiwa na mpasuo unaofikia juu kidogo ya goti.

Hafla hiyo ilikuwa ya kusherehekea kukabidhiana madaraka kwa amani baada ya rais aliyemaliza muda wake, Barack Obama kumpisha Trump. Hafla hiyo ya burudani hufanyika kuzindua kipindi cha rais mpya ambaye huitumia kuonyesha mapenzi yake katika mavazi, muziki na dans

Huu Ndio Upasuaji wa kurudisha Bikra Kwa Mwanamke Unavyofanywa ..!!!




bikra ni nini?

hii ni ngozi laini sana inayofunika uke kwa wanawake ambao hawajawahi kushiriki ngono kabisa, kikawaida mwanamke anaacha kuitwa bikra pale ngozi hii inapoondolewa.... ngozi hii kitaaamu inaitwa hymen.

hymenorrhaphy ni nini?

huu ni upasuaji unaofanyika kuirudisha bikra ya mwanamke ambayo imeshatoka tayari kwa sababu mbalimbali.

aina hii ya upasuaji mara nyingi hazipatikani kweye hospitali za kawaida kwani hazina umuhimu wowote kwenye matibabu na zinaweka kwenye kikundi cha plastic au cosmetic surgery,hivyo mara nyingi hufanyika kwenye hospitali au clinic binafsi na mabingwa wa magonjwa ya akina mama yaani gynacologist..

idadi ya wanawake wanaofanyiwa aina hizi za upasuaji inazidi kuongezeka miaka inavyozidi kwenda mbele kutokana na watu kuanza ngono mapema sana.

watu gani wanatakiwa wafanyiwe aina hizi za upasuaji?

wanawake ambao wanataka kurudisha bikra zao ambazo zimeshatoka wanatakiwa kufanya upasuaji huu kwani hakuna dawa yeyote inayoweza kurudisha bikra na ukiisikia ujue ni utapeli.

katika hali ya kawaida bikra inaweza kutoka kwa kushiriki ngono, kupata ajali na kuumia, tabia ya kujichua, mazoezi kama kuendesha baiskeli au farasi, matumizi ya aina fulani za pedi  au magonjwa fulani fulani.

wakati mwingine ngozi ila ya bikra inaweza kua ngumu sana kiasi kwamba ikakataa kuchanika hata kwa kuingiliwa kingono. hivyo mwanamke kutotoka damu wakati wa ngono kwa mara ya kwanza haimaanishi kwamba mwanamke sio bikra.

kwanini wanawake wanafanya aina hizi za upasuaji?

wanawake hua wanasababu mbalimbali kama ifuatavyo

   1 kuwaonyesha wanaume zao au jamii zao kwamba wao ni mabikra kipindi cha ndoa hasa kwenye jamii fulani fulani ambazo bikra ni muhimu sana siku ya ndoa.

  2  kuwasaidia wenye maumivu ya kisaikolojia baada ya kubakwa, hii inawafanye wapate amani kidogo baada ya upasuaji huu.

   3 kurudisha bikra ambayo imeharibika sababu ya kuumia kwa ajari.

upasuaji huu unafanyikaje?

hii ni aina ya upasuaji mdogo ambayo inafanyika kwa kuchoma sindano ya ganzi tu na wala haihitaji kwanamke kupewa dawa za usingizi, japokua kuna wakati mwingine kutokana na mazingira ya mgonjwa daktari anaweza kulazimika kutoa dawa ya usingizi.

kuna aina tatu za upasuji za kurudisha bikra kama ifuatavyo.

  1  kuishona tena ngozi ile ya ya hymen ambayo inamfanya mwanamke aitwe bikra kwa kuirudisha pamoja na kuiacha ipone kisha kurudi kama zamani

  2  kuweka ngozi ya hymen ya bandia na kuishonea pale kisha kuweka ndani yake aina fulani ya kimiminika kinachofanana kabisa na damu ili damu ionekane ikitoka  wakati wa ngono

  3  kuikata ngozi ya hymen ambayo ilichanika mwanzoni na kuitoa nje kisha kuirudishia upya na kuishona kabisa kama mwanzo.

wanawake wanaofanya aina hii za upasuaji wanatakiwa wafahamu kwamba wanatakiwa wakae bila kushiriki ngono wiki tatu mpaka miezi mitatu ili bikra ishike vizuri hivyo ni vizuri kuifanya mapema kabla ya ndoa sio unataka ufanyiwe leo afu wiki ijayo uolewe.

nyuzi zinazotumika kushona ngozi ile ya bikra hua haziondolewi yaani baadae huyeyuka ndani kwa ndani.

madhara ya upasuaji huu

upasuaji huu ni salama kabisa ila hua una madhara madogo madogoambayo ni kawaida hata kwa uparesheni zingine kama ifuatavyo.

kutokwa damu; hii ni kawaida hata kwa uparesheni zingine lakini damu hii inatakiwa ikauke na kuondoka baada ya siku chache.

kubana sana; wakati mwingine daktari anaweza akaishona ngozi ile na kuibana sana kiasi kwamba ikawa ngumu sana siku ya kuitoa wakati wa kushiriki ngono. hua na maumivu makali ambayo huisha bila dawa yeyote baadae.

infection; hii husababishwa na kushambuliwa na bacteria baada ya upasuaji lakini huweza kuzuiliwa kwa kupewa dawa za kuzuia hali hii mfano antibiotics

mwisho; aina za upasuji hizi zinapatikana nje ya nchi kwa wingi, kwa nchini tanzania na afrika kwa ujumla zipo pia lakini ni sehemu chache sana.

dunia inakwenda kwa kasi sana hivyo mwanaume ukijikuta umeoa bikra mwenye watoto wanne usishangae..

Kwa walevi Mnaotaka Kuacha Pombe Dawa Soma HAPA!!!



makala iliyopita nilizungumzia madhara ya unywaji wa pombe na kama hukuipata makala hiyo basi isome hapa........, watu wengi ambao ni walevi sana kwenye jamii hudharauliwa na kulaumiwa sana kwa kuendekeza tabia hizo, ni kweli wanaweza kua wanapaswa kulaumiwa lakini upande wa pili ni kwamba watu hawa pia hawapendi kua hivyo na wanashindwa kuacha kwasababu pombe ina kitu kinaitwa addiction yaani mazoea na sio rahisi kuacha kirahisi kwani mwili umeshazoea na unataka zaidi, ikitokea umeacha ghafla hata shughuli zako zitakushinda kwani utapata dalili kitaalamu kama withdraw syndrome ambazo ni kutetemeka, kichwa kuuma, kutapika , kushindwa kula na kua mgonjwa muda wote.

maana yangu ni kwamba mlevi aonekane kama mgonjwa kwenye jamii na kama anataka kuacha pombe basi mpeni msaada na sio kumtenga, swala la kuacha pombe linawezekana kabisa kwa walevi waliopindukia au watu wanaokunywa kawaida tu. yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa kuacha pombe..

amua kutoka moyoni; hakikisha maamuzi haya yametoka moyoni mwako kulingana na wewe unavyoona na sio kwamba unataka ili kuacha kuridhisha kikundi fulani au mtu fulani, hii itakupa nguvu ya kupambana na majaribu ya kutaka kunywa pombe tena.

wajulishe wanywaji wenzako nia yako; waambie rafiki zako kwamba umeamua kuacha pombe kwa muda fulani, wape sababu zako za msingi na kama huna waambie ni sababu binafsi za kifamilia, wajulishe kwamba inaweza kua ngumu na utaomba msaada wao iwapo ukiwaka tamaa ya kunywa pombe tena.

jiwekee malengo mafupi; anza kwa kujiwekea kwamba sitakunywa pombe mwezi huu wote wa kwanza, ukifanikisha ongeza mwezi mwingine...hii itakuapa motisha ya kuendelea kuacha kuliko kusema kwanzia leo sinywi tena kwani utajikuta unakunywa. kama mwezi ukiisha na kujikuta umesevu pesa nyingi kwa kutokunywa basi jinunulie zawadi yeyote.

pangilia starehe zako; kama starehe zako nyingi zinahusisha kunywa pombe basi pangilia starehe zingine ambazo hazitaki pombe mfano kwenda bichi, kwenda kuangalia sinema, kungalia mpira uwanjani na kadhalika. epuka kwenda disko na bar kwa kipindi hiki cha mwanzo.

jitoe nje ya raundi za pombe
; kama umeacha pombe usijihusishe na kuwanunulia watu pombe kwa kuzungusha kama wanywaji wanavyofanyiana wakiwa bar, nunua kinywaji chako kimoja kama ni soda au juisi kisha kaa pembeni ukinywa. kuwanunulia watu utajikuta na wewe unanunuliwa pombe.

kama mnatoka kwenda kwenye starehe basi endesha gari; kuendesha gari ni sababu kubwa ya wewe kutokunywa pombe kama sheria inavyotaka na hata ukilazimishwa kunywa utawaambia rafiki zako kwamba mimi ni dereva leo.

kua tayari kuzungumzia swala lako; watu wengi watakua wanakuuliza kwanini umeamua kuacha pombe, basi andaa sababu za msingi za kuwaambia kama jinsi pombe inavyoharibu maisha yako ya kijamii, kiuchumi na kiafya na wakati mwingine ukiona umezidiwa waambie ni sababu za kifamilia zaidi.

badilisha sehemu za kukutana na watu;
 kama ulikua ukipanga kuonana na mtu, unaenda bar basi badilisha sehemu ili ue unaenda kuonana nao kwenye mgahawa au sehemu zingine za wazi ambapo pombe haziuzwi.

furahia faida za kuacha kwa muda huo;
 angalia ni kaisi gani cha fedha umesevu kwa kuacha pombe, unajisikiaje kukaa muda mrefu bila kupata hangover, unajisikiaje jamii iliyokudharau sasa inakuheshimu na hii itakupa nguvu zaidi a kusonga mbele.

dawa za kuacha pombe kwa walevi sana;
 kuna dawa maalumu ambazo zimetengenezwa kuwatibu watu ambao wanataka kuacha pombe hasa wale ambao wameshindwa kuacha kwa njia nilizotaja hapo juu, utaratibu huu hufanyika chini ya uangalizi wa daktari hasa kwa nchi zilizoendelea...dawa hizi hufanya kazi kwa kukosesha mtu hamu ya kunywa pombe, kuongeza muda wa hangover mpaka siku tatu, na kuzuia madhara mtu anayopata kwa kuacha pombe haraka mfano disulfiram.[sina uhakika kama zinapatikana nchini], pia unawea kutumia virutubisho mbalimbali vya kuondoa sumu mwilini baada ya kuacha pombe, hivyo unaweza kuvipata hapa nchini.

SIMANZI: Ajinyonga Baada ya Kusalitiwa na Mpenzi wake! Aacha barua yenye ujumbe mzito!!



Kijana mmoja kwa Jina la Fredrick Richard amefikia hatua ya kujinyonga baada ya mpenzi wake (Rose) kumsaliti na kugawa tunda kwa rafiki yake kwa jina Robert.


Kabla ya kufikia maamuzi ya kujitoa uhai, kijana huyo aliandika barua ya simanzi kusikitishwa kwa kitendo alichofanyiwa na wawili hao.

Hii hapa chini ni picha ya huyo inaesadikika alikuwa mpenzi wake;




Wednesday, January 18, 2017

Mwenyekiti Chadema Ahukumiwa Miezi Nane Jela Bila Faini,Kisa Hiki Hapa..!!!



VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Selemani Mathew na Katibu wa Chadema Kijiji cha Nyangamara ‘A’ mjini Lindi, wamehukumiwa kifungo cha miezi minane jela bila ya faini kutokana kufanya mkutano bila ya kibali cha Jeshi la Polisi katika kijiji hicho wilayani Lindi.

Viongozi hao waliohukumiwa ni kati ya viongozi sita waliokamatwa na kutuhumiwa kufanya mkutano bila ya kibali cha Jeshi la Polisi nchini.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Lindi, Muhini alitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza mashtaka pande zote mbili na kubaini viongozi hao walitenda kosa la kisheria.

Tukio lililotokea Aprili 3, mwaka jana kwa viongozi na wanachama kwa pamoja kufanya mkutano bila ya kibali cha Jeshi la Polisi wilayani Lindi.

Alitaja kifungu cha sheria kilichovunjwa ni Kipengele 74(1) na 75 kinachozungumzia Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinachosomeka kwa pamoja na sheria ya Jeshi la Polisi.

Alisema washitakiwa wengine wanne wanaachiwa huru, kwani walibainika hawana hatia. Hao ni Bashiru Rashidi, Hassani Mchilima, Abdallah Mmasikini na Isimael Kupilila.

Akizungumzia hukumu hiyo, Mratibu wa Wanawake wa Chadema Mkoa wa Lindi, Sina Kikuwi alisema mahakama haikutenda haki kwa watuhumiwa hao.

Alisema taarifa walikuwa nayo kwenye vikao hivyo vya ndani havihitaji kibali, bali kutoa taarifa ambazo zilishatolewa katika mamlaka husika.

Selemani Mathew aliwahi kuwa D
iwani wa Vijibweni wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM. Aligombea katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi mwaka juzi, ambapo katika kura za maoni za CCM alishindwa na Nape Nnauye.

Baadaye alihamia Chadema ambako alikuwa mgombea ubunge wa chama hicho, lakini pia alishindwa na Nape ambaye sasa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Powered by Blogger.