WATU 15 waliofukiwa kwa kifusi katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita, wameokolewa wote wakiwa hai kutokana na jitihada zilizofanywa na wataalamu wa mgodi huo na mingine kwa kushirikiana na serikali.
Habari zilizotufikia punde ni kwamba watu hao wameokolewa baada ya kukaa takribani siku tatu ndani ya mgodi bila kupata chakula na bila kuona mwanga wa jua.
Aidha, taarifa za awali zinasema kuwa baada ya kuokolewa watu hao wamewekwa chini ya uangalizi wa
karibu na wataalamu wanaendelea na uchunguzi huo ambapo baada ya muda itatolewa ripoti kamili.
0 comments:
Post a Comment