Sunday, January 22, 2017

Baada ya Bilicanas na Shamba, Serikali ‘Yakamata’ Hoteli ya Mbowe Arusha



 Ikiwa ni takribani miezi mitano sasa tangu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe alipoondolewa katika jengo la Bilicanas lililokuwa pia na ofisi za Free Media na siku moja tangu serikali imzuie kuendeleza shughuli za kilimo kwenye shamba lake, kiongozi huyo amepata pigo jingine katika hoteli yake anayoimiliki.

Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amepewa siku 14 na serikali awe amelipa kodi ya hoteli yake ya Aishi takribani TZS milioni 13.5 vingine vyo hoteli hiyo itafungwa.

Hoteli ya Aishi inayomilikiwa na Freeman Mbowe iliyopo Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro





Uamuzi huu wa serikali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekuja siku moja tangu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa alipotangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe kwa madai kuwa lipo katika eneo la chanzo cha maji cha Mto Weruweru.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mujibu wa taarifa alizozipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Freeman Mbowe amekuwa akikwepa kulipa kodi kwa miaka mitano na kusababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato.

Kwa miaka mitano imeelezwa kuwa Mbowe hakupeleka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hali ya mauzo yake ambayo inapaswa kutumika kujua ni kodi kiasi gani anatakiwa kulipa.

Kuhusu shamba lake, DC alisema kuwa shughuli za kilimo katika eneo hilo limepeleka uharibifu wa mazingira huku kiongozi huyo akivuna miti ya asili bila kibali cha Mkuu wa Wilaya kinachotolewa baada ya uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.