Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga dhamana yake, baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha notisi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa wakipinga kusikilizwa kwa rufani hiyo .Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma Maghimbi alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa ya Jamhuri iliyopinga Lema kupatiwa dhamana Novemba 11 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ambapo siku hiyo Jamhuri iliwasilisha notisi ya mdomo.Baada ya Lema kufikishwa mahakamani saa 3.25 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali, huku pia polisi wakiwa wametanda viwanja vya Mahakama Kuu ndani na nje sanjari na gari moja la maji ya kuwasha, baada ya mawakili wa pande zote kujitambulisha Jaji Maghimbi alisoma notisi ya Jamhuri kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa na kueleza kufungwa kisheria kutoa uamuzi wa rufani hiyo.
0 comments:
Post a Comment