Monday, December 7, 2015

KASI YA MAGUFULI YAINGIA UTUMISHI - Wafanyakazi watakiwa kusaini kiapo cha uadilifu



Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza rasmi kutekeleza Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma nchini .

Akiongea na vyombo vya habari leo, Katibu Mkuu Hab  Mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi Desemba, 2015 ambapo kila Mtumishi wa Umma ataweka saini  ya kiapo  kwa kuzingatia  taratibu zilizowekwa na  mazingira ya taasisi husika.

“Utaratibu wa Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma umetolewa kupitia waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma  Na. 2 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa viongozi, Watumishi wa Umma na sekta binafsi wa tarehe 1 Agosti, 2015.” alisema Mkwizu.

Mkwizu aliongezea kwa kusema, uanzishwaji wa Ahadi na Uadilifu  ni muendelezo wa uundwaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu, utoro sehemu za kazi na kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya themanini na tisini.

Alivitaja vyombo vingine ambavyo vilianzishwa kusimamia ahadi na uadilifu kuwa ni Sekretariate ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Mkwizu alivitaja vipengele ambavyo mtoa ahadi anatakiwa kuvitamka ni, kuwa mzalendo wa nchi yake na kutii Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhudumia Umma na watumishi wenzake kwa heshima, kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma, kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi wa dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu.

Vipengele vingine ni kutumia rasilimali za Umma kwa manufaa ya Umma, kutotoa siri za Serikali au mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya Umma, kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kutoomba kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa na kutotumia madaraka kwa manufaa binafsi ya ndugu, rafiki au jamaa.

Aidha, Mkwizu ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Ahadi na Uadilifu unakamilika  ifikapo tarehe 31/12/2015 na kuwasilisha Ofisi ya Rais – UTUMISHI kabla ya tarehe 25/02/2016 na utekelezaji wake kuwa kila ifikapo Juni 30 ya kila mwaka. 

Fomu za Ahadi ya Uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI yenye anwani www.utumishi.go.tz.

KASI YA MAGUFULI YAIKUMBA CLOUDS FM, MWAKA HUU HAKUTAKUWA NA FIESTA







Mkurugenzi wa Clouds Media Group ambao ni waandaaji wa tamasha la Fiesta, Ruge Mutahaba amesema kuwa tamasha hilo halitakuwepo mwaka huu.

Amesema wameamua kuahirisha kufanya tamasha hilo mwaka huu kutokana na ufinyu wa muda uliobaki hasa baada ya kupisha kipindi cha uchaguzi.

“Tulijua tukimaliza kampeni tutafanya kwa mikoa michache lakini tumeona kwamba hakuna kitu kizuri kama kumsupport mheshimiwa Magufuli , hebu sasa hivi turudi kwanza tutulie tuache hii amsha amsha aliyoanza nayo ianze kufanya kazi tujipange kwaajili ya Fiesta 15 ambayo itafanyika mwaka kesho,” Ruge aliiambia XXL ya Clouds Fm.

“Tutakuwa tunafikisha miaka 15 ya Fiesta na nina uhakika itakuwa na ukubwa inayostahili kuliko kufanya kitu kidogo mwaka huu. Tumeona tuache mwaka kesho mikoa 15, miaka 15 ya Fiesta itakuwa kubwa zaidi. Hapa Kazi imebidi iivae Fiesta pia,” alisema.

Sunday, December 6, 2015

Siku 30 za Kuwa Madarakani Kama Rais , Magufuli Aokoa Sh1trilioni

 Rais John Magufuli leo ametimiza mwezi mmoja tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo huku akiweka rekodi ya kuokoa kiasi cha Sh997.4 bilioni (karibu Sh 1trilioni) ambazo zilikuwa zitumike kwa matumuzi yasiyo ya lazima, na ukwepaji kodi.

Sh997.4 bilioni zilizookolewa zitaweza kutumika kununua magari ya wagonjwa, kujenga zahanati, kujenga barabara za lami, kununua madawati, kujenga vyumba vya madarasa, kuchimba visima, kununua mashine za uchunguzi wa magonjwa, magari ya wanafunzi, pikipiki kwa maofisa kilimo, mikopo ya elimu ya juu au kujenga viwanja vya michezo kadri Serikali itakavyoelekeza.

Dk Magufuli aliapishwa Novemba 5 katika hafla iliyofana na alianza kazi ya kutafuta na kuziba mianya ya upotevu wa fedha Novemba 6 alipotembelea Hazina. Katika mazungumzo ya watendaji wa wizara hiyo Rais Magufuli alipiga marufuku safari zote za nje na kwamba zitakuwa zinaruhusiwa kwa kibali maalumu.

Novemba 7 alitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako aliagiza mashine za MRI na CT-Scan zitengenezwe na aliagiza Sh3 bilioni zitolewe kugharimia matengenezo kati ya Sh7 bilioni zilizokuwa zinahitajika.

Novemba 19, Dk Magufuli aliwasilisha bungeni jina la Kassim Majaliwa, mbunge wa Ruangwa kwamba ndiye alimpendekeza kuwa Waziri Mkuu. Baada ya jina kupitishwa na Bunge, Novemba 20 Kassim Majaliwa aliapishwa.

Jioni alilihutubia Bunge akionyesha mwelekeo wa Serikali yake ya awamu ya tano. Katika hotuba hiyo iliyowasisimua wabunge na hata wananchi waliosikiliza kupitia televisheni na redio, Dk Magufuli aliahidi kupambana na mafisadi, kubana matumizi, kuhimiza utendaji kazi, kuinua uchumi na kulinda amani na utulivu.

Baada ya hapo Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa wamekuwa wakitembelea maeneo muhimu kwa uchumi wa nchi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bandari na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)

Utendaji huo wa Serikali wa Magufuli ndani ya mwezi moja na kipindi kabla hajaunda baraza la mawaziri, umetazamwa na jamii kuwa ni mbinu ya kusafisha nchi na kutengeneza mazira safi ili mawaziri watakaoteuliwa wafuate kasi hiyo.

Fedha zilizookolewa

Kwa kuzingatia ripoti ya matumizi ya fedha za safari zilizolipwa kama nauli na posho kwa kipindi cha kati ya mwaka 2013 na 2015 kiasi hicho ni pamoja na Sh356.3 ambazo zingeweza kutumika kwa safari hizo. Dk Magufuli aliagiza kwamba baadhi ya shughuli zitafanywa na mabalozi wa Tanzania walioko nje.

Novemba 19 alipozindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma, Dk Magufuli aliagiza Sh225 milioni zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili ya hafla ya wabunge, zipelekwe kununua vitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Fedha hizo zilinunua vitanda 300, magodoro 300, mablanketi 1675, na viti vya magurudumu 30.

Pia, katika hotuba yake bungeni, Dk Magufuli alirejea uamuzi wake wa kufuta safari za nje kwa watendaji wa Serikali na kueleza safari hizo zimeigharimu Serikali Sh356.3bilioni ambazo zingeweza kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 400.

Novemba 23, Dk Magufuli alitangaza kufutwa kwa maadhimisho ya Siku ya Uhuru Desemba 9 na akaagiza Sh4 bilioni ambazo zingetumika zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Morocco kwenda Mwenge. Kazi hiyo imeanza.

Novemba 25, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitangaza kufutwa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani na akaelekeza kwamba fedha zilizopangwa kwa ajili ya sherehe hizo zitumike kununua dawa za kufubaza makali ya ukimwi (ARVs).

Novemba 27, Waziri Mkuu Majaliwa alitembelea bandarini na kubaini makontena 349 ambayo yalitolewa bandarini bila kulipiwa ushuru na kuifanya Serikali kukosa mapato ya Sh80 bilioni.

Tayari wenye makontena hayo wameanza kulipia na jana  TRA ilitangaza kukusanya Sh6.3 bilioni kati ya hizo Sh80 bilioni. Katika ziara yake nyingine ya kushtukiza Desemba 3 Majaliwa alibaini makontena 2,431 yalitolewa bila kulipiwa kodi. Ikiwa makontena hayo yangelipiwa kodi viwango sawa na yale 349 Serikali ingepata Sh557.2 bilioni.

Desemba 3, Dk Magufuli alifanya mazungumzo na jumuiya ya wafanyabiashara nchini na akawataka wote ambao waliondoa mizigo yao bandarini bila kulipa kodi, wajitahidi kulipa katika kipindi cha siku saba kuanzia juzi vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Makontena ni shida

Desemba 1, makontena mengine tisa yalikamatwa na TRA eneo la Mbezi, Tangibovu yakiwa yametoroshwa bila kulipuiwa ushuru wa Sh58 milioni. Jumla ya Sh637.2 zimeokolewa kutokana na mkakati wa kukusanya fedha kutoka kwenye makontena 2,431 pamoja na 349 na hayo tisa.

Matumizi ya Sh 997.4 bilioni

Kwa muda mrefu, Serikali imekuwa ikikwama kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kutokana na kukosa fedha. Dk Magufuli alikiri juzi kuwa hakuna fedha za maendeleo zilizokuwa zimetolewa kwa wizara zote katika mwaka huu wa fedha wa 2015/16, lakini baada ya miezi sita juzi ndiyo zimetolewa Sh120 bilioni.

Dk Magufuli hakusema Serikali imepata wapi fedha hizo, lakini huenda ni sehemu ya fedha ambazo ameokoa katika kipindi cha mwezi mmoja.

Kama fedha hizo zingeelekewa katika ujenzi wa barabara, na kwa kuzingatia kilomita moja inajengwa kwa Sh1 bilioni, fedha hizo zitaweza kujenga karibu au zaidi ya kilomita 1,000, ambao ni umbali kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma au Dar es Salaam mpaka Tunduma.

Aidha, Sh997.4 bilioni zingeweza kununua magari 3,325 ya kubebea wagonjwa kwa gharama ya Sh300 milioni kwa kila moja na kuwezesha kila mkoa kupata magari 133 ya aina hiyo.

Pia, zahanati moja yenye vifaa vyote muhimu ujenzi wake unagharimu kati ya Sh600 milioni na Sh700 milioni. Hivyo, fedha hizo zingeweza kujenga zahanati 1,425 yaani kila mkoa ungepata zahanati 57.

Vilevile, wakati maelfu ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wanasoma kwa kukaa chini kutokana na kukosa madawati, Sh997.4 bilioni zitaweza kutengeneza madawati yenye miguu ya chuma 33,249,142 kwa gharama ya Sh30,000 kwa kila moja na kuwezesha kila mkoa kupata madawati 1,329,966.

Pengine, fedha hizo zinaweza kujenga vyumba vya madarasa 132,996 kwa bei ya Sh7.5 milioni kwa darasa moja, hatua ambayo itawezesha kujengwa kwa vyumba vya madarasa 5,319 kila mkoa nchini.

Kipimo maarufu cha CT-Scan ambacho ufanyaji wake wa kazi unasuasa Muhimbili kwa muda mrefu, kinauzwa kwa wastani wa Sh900 milioni, hivyo, Sh997.4 bilioni zitaweza kununua mashine 1,108 ambazo zingesambazwa na kila mkoa ukapata mashine 44.

Gharama za kuchimba kisima kifupi ni kati Sh1 milioni na Sh3 milioni kulingana na jiografia ya eneo husika, hivyo Sh997.4 bilioni zitaweza kuchimba visima 332,491; kila mkoa ukapata visima 13,299.

Pia, kwa kuwa Serikali inahimiza uboreshaji wa sekta ya kilimo, Sh997.4 bilioni zitaweza kununua pikipiki 332,491 na kugawiwa kwa maofisa kilimo kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa kilimo vijijini na kila mkoa ungepata pikipiki 13,299.

Kama fedha hizo zitaelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu, zitaweza kugharamia wanafunzi 249,368 wa mwaka wa kwanza kwa asilimia 100 kwa wastani wa Sh4 milioni kwa kila moja kwa ajili ya chakula, malazi na ada.

Imeandikwa na Fidelis Butahe, Joyce Mmasi na Peter Saramba

Gazeti la Dagens Nyheter(Sweden); Magufuli atajwa Kuwachonganisha Marais Wenzake na Wapiga Kura Wao!

Dagens Nyheter ni gazeti kubwa kushinda yote nchini Sweden, ndio 'Daily News' lao kwa maana ya jina la gazeti.

Katika toleo lake la Ijumaa Desemba 4, habari za John Magufuli zimepamba pia gazeti hilo.

Amemwagiwa sifa, na ikaandikwa pia, kuwa Magufuli amewaweka katika wakati mgumu marais wenzake wa nchi jirani kwa vile wapiga kura wao wameonyesha wivu wao kwa Watanzania kupata Rais wa aina ya Magufuli.

Hata hivyo, kwenye gazeti hilo, imeandikwa pia, kuwa hata kabla ya kuingia milango ya Ikulu, Magufuli tayari ameshajipatia maadui wakiwamo wa ndani ya chama chake kwa hatua zake anazozichukua, hususan za kubana matumizi ya Serikali.

 Habari nzima  unaweza kuitazama kupitia Website ya Hilo gazeti kwa kubofya link hii hapa .Imeandikwa kwa lugha yao.


Tafsiri ya maelezo waliyoandika  kwa Kiingereza ni kama inavyosomeka hapa chini......

The newly elected President John Magufuli barely had time to move into Tanzania's presidential palace before he got his first enemies - the members of his own party CCM, which snuvats at the annual independence celebration. The money will instead go to a cleaning campaign.

The newly elected President John Magufuli barely had time to move into Tanzania's presidential palace before he got his first enemies - the members of his own party CCM, which snuvats at the annual independence celebration. The money will instead go to a cleaning campaign.

December 9 is the 54 years since the then Tanganyika gained independence from Britain, which is usually celebrated with pomp and circumstance in Tanzania's economic hub of Dar es Salaam. On vipl?ktaren sitting members of the party, CCM, who has ruled the country since then.

CCM's long hold on power has contributed to Tanzania is one of the world's poorest countries. Lately Tanzanians started playing with the idea that change is possible even in a system where the same party again and again win elections.

This year there will be no celebration, the newly elected President John pombe Magufuli declared on state television.

Instead, the money should be used for a national cleaning campaign. This year's Christmas card from the government has also been abolished in order to save money.

The budget for a grand opening celebration for the new parliament in the capital Dodoma were cut from the equivalent of 1.2 million SEK to 100 000 SEK. The surplus was used to buy new beds to the run-down hospital Muhumbili in Dar es Salaam, whose director was fired in the rebound after Magufuli made an impromptu visit.

Newspapers report on a delegation of 50 leaders who were off on a tour to the other countries of the British community. Magufuli shrank delegation to four people, which should have saved 2.4 million.

Civil servants and politicians forbidden to travel abroad on state funds and conferences will be held in the meeting rooms rather than in expensive resorts.

Magufuli, called the bulldozer because of its persistent road construction in his previous role as Minister, is now living up to his nickname in the more figurative sense, and voters in neighboring countries look with envy on development.

On social media spread nowadays continental success stories - that Muhammadu Buhari corruption fight in Nigeria, Malawi's former president Joyce Banda who sold the government plane and 60 Mercedes limousines or Namibia EX-PRESIDENT Hifikepunye Pohamba, who was awarded this year's Mo Ibrahim prize for good leadership.

Tanzania, one in all the years have had a big brother attitude to become a model harbors its own leaders in a difficult position where they have to feel ashamed or explain himself.

Balozi Sefue: Maagizo Ya Rais Magufuli Hayavunji Sheria ya Ununuzi



Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema maagizo ya Rais  Magufuli kutaka fedha zilizokuwa zitumike kwa matumizi yasiyo ya lazima, kupelekwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, hayavunji sheria ya manunuzi wala utaratibu mwingine wa kisheria.
Hivi karibuni,Rais Magufuli aliagiza sh.milioni 225 zilizokuwa nimechangwa kwa ajili ya hafla ya wabunge zipelekwe Hospitali ya Muhimbili kununua Vitanda na Mashuka.
Aligiza pia Bilioni 4 zilizokuwa zitumike katika sherehe za Uhuru Disemba 9 zitumike kupanua barabara ya Mwenge- Morocco

Akitoa ufafanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco, Balozi Sefue  amesema mradi huo sio mpya na kwamba taratibu zote zilishafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwalipa waliokuwa wamejenga  kando ya barabara.

Amesema kilichokuwa kinakwamisha mradi huo ni  pesa.
Akizungumzia sakata la wakuu wa mikoa na wilaya kuwanyima likizo wafanyakazi huku wengine  wakitiwa rumande kwa masaa  6, Balozi Sefue  amesema serikali haina taarifa rasmi hivyo akalitaka shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) kuwasilisha malalamiko serikalini badala ya kuishia kulalamika katika vyombo vya habari
Mpekuzi blog

Kiama Cha Waliotorosha Makontena 2431 Kimekaribia.....Majina Yao Yameshatua Kwa Waziri Mkuu



Baada ya moto kuwawakia watumishi wa Mamlaka ya Mapato wanaotuhumiwa kujihusisha na ukwepaji kodi wa kifisadi kwenye Bandari Kavu (ICDS) na kupelekea wanane kati ya watuhumiwa 37 kufikishwa mahakamani, zamu ya Mamlaka ya Bandari inakaribia, imefahamika.
 

Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam, waliohusika na kupitisha makontena 2,431 bila kulipiwa kodi wanakaribia kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria baada ya majina ya wahusika kutua mezani kwa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa, kama alivyoagiza.
 

Kuwasilishwa kwa majina hayo katika Ofisi ya Waziri Mkuu Majaliwa, kunafuatia ziara ya kushtukiza katika Bandari hiyo ambapo aligundua kuwapo kwa ufisadi huo.
 

Katika ziara hiyo, Majaliwa alimtaka Kaimu Meneja wa Bandari, Hebel Mhanga kupeleka ofisini kwake majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji huo wa kodi unaokadiriwa kufikia shilingi bilioni 600 ifikapo saa 11 jioni Alhamisi.
 

Jana  Mwandishi wa Habari wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Irene Bwire, alithibitisha  kuwa majina hayo yameshamfikia Waziri Mkuu.
 

“Ninachoweza kukwambia ni kwamba majina yamefika mezani kwake kama alivyoagiza lakini siwezi kukutajia majina ya wahusika... Waziri Mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kuyataja hadharani iwapo ataamua kufanya hivyo,” alisema Irene.
 

Kwenye ziara hiyo, Majaliwa alimpa Meneja huyo siku saba kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye mfumo wa ankara na kuwa wa malipo wa kielektroniki.
 

Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaban Mwinjaka, aliuonya uongozi wa Bandari kutofanya ujanja wa kuficha majina ya watu wakubwa waliohusika na upotevu wa makontena 2,431 yaliyotolewa bila kulipiwa ushuru.
 

Mwinjaka alitoa onyo hilo baada ya uongozi huo kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kupeleka majina ya watu hao ofisini kwake juzi.
 

“Lazima uongozi wa Bandari ujihakiki kama watu wote waliohusika katika hujuma ile majina yao yamo kwenye orodha iliyopelekwa kwa Waziri Mkuu,” alisema katibu Mkuu huyo. 
“Hata akiwa papa lazima ajulikane na wasiwachukue watu wadogo wadogo peke yao maana itawagharimu.”
 

Waziri Mkuu Majaliwa alifanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini katikati ya wiki kwa kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo wa malipo baada ya kupewa taarifa kuna makontena 2,431 yalitolewa bandarini bila kulipiwa ushuru.
Majaliwa, alikagua idara mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia Scanners.

 

Katika ukaguzi huo, Majaliwa alieleza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne ambazo ni JEFAG, DICD, PMM na Azam huku watumishi 10 tu wa ngazi za chini ndio wakiwa wamesimamishwa kazi kutokana na makosa hayo.
 

Ziara hiyo ilikuwa ya pili bandarini katika kipindi cha siku tano, baada ya ile ya awali kubaini upotevu wa makontena 349 bila kulipiwa ushuru, kitendo kilichosababisha awasimamishe kazi watumishi tisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bandari, huku Rais John Magufuli akimsimamisha kazi kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade.
Mpekuzi blog

Saturday, December 5, 2015

TANESCO KUNUNUA NGUZO AFRIKA KUSINI KWAZUA MASWALI NCHINI

Uagizaji huo wa nguzo kutoka nje ya nchi,

Uagizaji huo wa nguzo kutoka nje ya nchi, unaelezwa kwenda kinyume na Sera ya Serikali ya maendeleo ya kiuchumi
Moshi. Rais John Magufuli ameombwa kuzuia uagizaji wa nguzo za umeme kutoka Afrika Kusini kunakofanywa na Shirika la Umeme (Tanesco) kupitia wazabuni ili kunusuru mamilioni ya fedha za kigeni.
Vyanzo kutoka Tanesco vimedokeza kuwa shirika hilo liko katika hatua ya mwisho kutangaza zabuni ya nguzo 700,000 ambazo, zinaweza kugharimu Dola 115 milioni (sawa na Sh250 bilioni) kwa mwaka 2015-2018.

Sehemu kubwa ya fedha hizo inatarajiwa kutumiwa na kampuni za nje zinazojipanga kuomba zabuni hiyo ili kuagiza nguzo kutoka Afrika Kusini na Kenya kama ilivyokuwa kwa zabuni ya 2013-2015.

Hata hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba alikanusha kuzibeba kampuni za kigeni, bali akasema katika kutafuta wazabuni, wanaongozwa na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011.
Sheria hiyo ndiyo ambayo Rais Magufuli wakati analihutubia Bunge Novemba 11, aliikosoa kwamba ni mbaya na kuwa Serikali ingepeleka muswada bungeni ili kuifanyia marekebisho.

Mramba alifafanua chini ya sheria hiyo, kuna zabuni za aina mbili, ambazo ni zabuni kwa kampuni za ndani ya nchi (NCB) na zabuni kwa kampuni za kimataifa (ICB).

Mramba aliwataka wanaohoji nguzo kuagizwa nje ya nchi, wasisahau kuna wakati Tanesco ilitangaza zabuni chini ya NCD, lakini wazabuni wa ndani wakashindwa hadi waziri akavunja zabuni hiyo hadharani.

Kuhusu thamani ya zabuni wanayokusudia kuitangaza hivi karibuni, alisema hafahamu jambo hilo na kushangaa inakuwaje wanaohoji wawe wanafahamu  thamani ya zabuni wakati bei hupangwa na wazabuni wanapoomba.

Uagizaji huo wa nguzo kutoka nje ya nchi, unaelezwa kwenda kinyume na Sera ya Serikali ya maendeleo ya kiuchumi inayohamasisha matumizi ya bidhaa za ndani.

Baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco, waliozungumza na gazeti hili, walidai hayo ni matumizi mabaya ya fedha za kigeni kwa kuwa Tanzania inao uwezo wa kuzalisha nguzo za kutosha kwa shirika hilo.

Maofisa hao wa Tanesco, waliliambia gazeti hili jana kuwa zabuni iliyopita ya miaka mitatu (2013-2015), ilisababisha asilimia 65 ya nguzo za umeme kuagizwa kutoka Afrika Kusini.

Ni kutokana na msingi huo, wafanyakazi hao wamemwomba Rais Magufuli kuzuia zabuni hiyo ambayo itatangazwa hivi karibuni. “Kwenye hotuba yake Rais alisema hataki samani ziagizwe nje ya nchi, sioni sababu kwanini hata nguzo zitoke nje ya nchi wakati tuna kampuni zinaweza kusambaza kutoka kwenye misitu yetu,” alidai ofisa mmoja wa Tanesco.

Hata hivyo, chanzo kingine kutoka sekta ya nishati ya umeme, kimedokeza kuwa kanuni za manunuzi zimekuwa zikipendelea kampuni za nje na kuziruhusu kuomba zabuni kwa Dola ya Marekani.

Wataalamu wa uchumi wanadai matumizi ya Dola kuagiza bidhaa ambazo zingeweza kupatikana hapa nchini, yanachangia kuporomosha thamani ya shilingi.

“Kuanzia mwaka uliopita shilingi yetu imeporomoka kwa asilimia 23 ya thamani yake kutoka Sh1,765 kwa Dola moja Desemba mwaka jana hadi Sh2,160,” alidokeza mchumi huyo.

Alisema kununuliwa kwa nguzo zinazozalishwa nchini, kungeongeza mapato ya Serikali kutokana na kodi ya ongezeko la thamani, kodi ya mapato na kodi nyingine ambazo hazilipwi na kampuni za nje.

Pia, itaongeza hamasa ya wananchi kuanzisha vitalu vya miti na wawekezaji kutoka nje ambao wataanzisha mashamba ya miti nchini kwa kuwa kutakuwa na soko la uhakika la Tanesco.
Kampuni za ndani zilizoshinda zabuni ya kusambaza nguzo nchini mwaka huo wa 2013-2015 zilikuwa Critical Engineering Solutions Construction Co, Sao Hill Industries Ltd na Mufindi Wood Poles.Kampuni za nje ambazo ni kutoka Afrika Kusini zilizoshinda zabuni hiyo ni Treated Timbers Products, Low’s Treated Timbers (Ptg), Rousant International na Maghilika Timber Ptg Ltd.
Ofisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud alisema hakuna ukweli kwamba nguzo za nje ni ghali kuliko za ndani, bali ni fitna za ushindani wa kibiashara za baadhi ya watu wanaokosa zabuni.
Alisema Tanesco inanunua nguzo kulingana na zabuni, ubora na bei, ziwe za ndani au nje lakini wapo wazabuni wa ndani ambao hushinda, lakini wakashindwa kukidhi mahitaji ya Tanesco.
“Kuna kipindi nikiwa pale Tanesco hata waziri wa nishati aliamua kuingilia kazi na kuwakemea wazabuni wa ndani walioshindwa kukidhi mahitaji ya zabuni,” alisema Badra.

Source;Mwananchi

MAWAZIRI WA JK WANASWA KWA UFISADI WA MABILIONI

‘Kuwa mtumishi wa Stanbic wakati tukio hilo

‘Kuwa mtumishi wa Stanbic wakati tukio hilo linatokea haimaanishi kuwa watumishi wote walihusika. Nadhani ni uhusiano uliopo kati yangu na waziri ndio unafanya nihusishwe.” Godfrey Mgimwa




Dar es Salaam.  Watu tisa wakiwamo mawaziri wawili wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jakaya Kikwete wametajwa kushiriki kwenye kashfa ya rushwa ya Sh13 bilioni wakati Serikali ya Tanzania ilipokopa Dola za Kimarekani 600 milioni (Sh1.3 trilioni) kutoka benki ya Standard ya Uingereza.



Ripoti ya Taasisi ya Kuchunguza Ufisadi (SFO) ya Uingereza iliyokuwa inafuatilia kashfa hiyo imewataja maofisa hao kuwa ni Waziri wa Fedha ambaye alifukuzwa kazi Mei 2012, na Waziri wa Fedha aliyefariki dunia Januari 2014.



Waziri wa Fedha aliyefukuzwa kazi Mei 2012 alikuwa Mustafa Mkulo wakati aliyerithi nafasi hiyo na baadaye akafariki akipatiwa matibabu Afrika Kusini Januari 2014 alikuwa Dk William Mgimwa.



Wakati ilipowasilisha barua ya pendekezo la mkataba wa mkopo wa Dola za Kimarekani 600 milioni (Sh12 trilioni) wizarani, Februari 2012, wizara ilikuwa chini ya Waziri Mkulo na mazungumzo ni kama yalififia kwa muda kabla hayajaanza upya Septemba chini ya Dk Mgimwa.



Kipindi cha uhai wake na kudumu kwake wizarani hapo, ripoti ya SFO iliyowasilishwa katika mahakama ya Southwark Crown ya jijini London, Uingereza inasema Dk Mgimwa ndiye aliyeidhinisha kuzinduliwa kwa hati fungani hiyo pamoja na nyaraka nyinginezo.



Mbali ya mawaziri hao, wengine waliokuwamo kwenye timu ya Serikali ya majadiliano ni Ofisa mwandamizi wa Hazina ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Madeni ya Serikali (NDMC). Huyo ndiye aliidhinisha barua ya ada ya mkataba na ile ya mamlaka.



Pia, alikuwamo msaidizi wa ofisa mwandamizi (Msajili wa Hazina) ambaye alipokea barua ya mapendekezo ya mkataba na waraka wa mamlaka kutoka Stanbic. Alihusika pia katika mapendekezo yaliyopitiwa na Waziri Mkulo.



Kamishna Msaidizi na Mshauri wa Sera wa wizara, alipokea barua ya mapendekezo ya mkataba na barua ya mamlaka kutoka Stanbic. Mwenyekiti wa Ufundi wa Kamati ya Madeni ya Serikali (TDMC) alipokea mapendekezo ya barua ya mamlaka na ile ya ada ya mkataba.



Hao ndio walikuwa wanakutana na timu ya maofisa wanne kutoka benki ya Stanbic. Kiongozi wa timu ya Stanbic alikuwa Bashir Awale, ambaye kwa wakati huo alikuwa mkurugenzi mtendaji wa Stanbic. Ingawa ripoti inamtaja kama alifukuzwa kazi Agosti 19, 2013 baada ya kushindwa kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi wa kesi hii, lakini inafahamika kuwa aliacha kazi mwenyewe.



Mwingine alikuwa Shose Sinare, ambaye alikuwa kaimu mkuu wa uwekezaji wa benki hiyo. Alikuwa anawajibika moja kwa moja kwa Bashir na alikuwa kiungo muhimu katika mkataba huu akimjuza mkuu wake kila lililojiri. Alijiuzulu Juni 3, 2013 na hivyo akawa amekwepa uchunguzi.



Ofisa wa  tatu ametajwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Fedha (Mgimwa) aliyefariki dunia 2014. Mtoto huyo, kwa mujibu wa ripoti ya SFO ni mhitimu aliyekuwa kwenye mafunzo ya kazi.



Mtoto wa waziri huyo, Godfrey Mgimwa, ambaye sasa ni mbunge wa Jimbo la Kalenga, Iringa alipoulizwa jana kama amewahi kufanya kazi katika benki ya Stanbic alikiri kuwa kwa wakati huo alikuwa akifanya kazi katika benki hiyo, lakini hajui chochote kuhusu mchakato huo.









“Nimesikia habari hizo lakini sifahamu lolote. Kuwa mtumishi wa Stanbic wakati tukio hilo linatokea haimaanishi kuwa watumishi wote walihusika. Nadhani ni uhusiano uliopo kati yangu na waziri ndio unafanya nihusishwe…ni vile tu hatupo naye hivyo hakuna wa kuelezea zaidi. Kwa kuwa mzee amefariki naona inatafutwa namna ya kutengeneza uhusiano uliokuwepo kati ya taasisi zilizohusika,” alisema Godfrey.



Mtu wa nne kwa upande wa Stanbic alikuwa mkuu wa huduma za sheria na usuluhishi wa benki hiyo. Ingawa hakuwa sehemu ya mpango huo lakini alishirikishwa na alifukuzwa kazi Oktoba 31, 2013 baada ya kushindwa kufuata maagizo ya bodi ya wakurugenzi ya kutoa taarifa juu ya ushiriki wa kampuni ya Egma.



Tukio la kwanza kuwakutanisha wahusika wengi waliotajwa ni mkutano kati ya wawakilishi wa benki ya Standard, Stanbic na Waziri Mgimwa Mei 28, 2012 kujadili pendekezo la mkopo wa Dola za Kimarekani 550 milioni na siyo Dola 600 milioni. Bashir na Sinare waliiwakilisha Stanbic.



Siku chache kabla ya mkutano huu, Bashir alikuwa ametuma barua wizarani hapo akifafanua na kubadili baadhi ya vipengele vya pendekezo la mkataba wa Februari 2012. Katika barua hiyo, alieleza kuwa endapo wizara ingeendelea na mpango huo basi mkataba wa mkopo na nyaraka nyingine za kisheria ziwe kati ya wizara na serikali na si mamlaka nyingineyo.



Siku chache baada ya mkutano huo, Dk Mgimwa alimtuma mwanaye na kumpatia barua ya utambulisho kwa mkurugenzi wa Stanbic. Bashir aliahidi kuwa angemsaili yeye mwenyewe. Alikutana naye Julai na akaidhinisha kuajiriwa kwake chini ya mpango wa wahitimu walio kwenye mafunzo ya kazi na kukabidhiwa kwa vijana walioongozwa na Shose Sinare. Kwenye mchakato huo, inaelezwa kuwa mtoto huyo wa waziri alikuwa na ushiriki fulani mdogo uliofanikisha mkataba huo.



Waziri Mgimwa, Msajili wa Hazina pamoja na msaidizi wake wakiwa na aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwenyekiti wa Bodi ya Egma, Harry Kitillya walisafiri kama ujumbe wa Tanzania ulioshiriki mkutano wa wawekezaji kwa lengo la kunadi pendekezo la kuuza hati fungani hiyo ambao uliandaliwa Benki ya Standard. Mkutano huo ulifanyika Februari 2013 na akihudhuriwa pia na Bashir na mwakilishi wa Standard.



Haya yamewekwa wazi na ripoti hiyo ya SFO yenye kurasa 55 ambayo ni matokeo ya uchunguzi wa ndani uliofanywa na mwanasheria wa benki ya Standard ya Uingereza, Jones Day. Baada ya uchunguzi huo Day aliwasilisha SFO ushahidi wote wa kimaandishi, baruapepe, simu na mazungumzo mengine aliyokusanya ya wote waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za kibenki. Ripoti hiyo iliyotolewa Novemba 25, ndiyo imetumiwa na SFO katika shauri lililoendeshwa kwa mfumo wa mtindo wa makubaliano ya kumlipa fidia mlalamikaji (DPA) kwenye mahakama ya Southwark Crown ya jijini London, Uingereza.



Kwa mujibu wa ripoti hiyo hadi Februari 2012 mapendekezo yalikuwa riba ya mkopo huo iwe asilimia 1.4. Baada ya Mukulo kuondolewa Sinare aliwahakikishia maofisa wa benki ya Standard ya Uingereza kwamba japokuwa hati ya uthibitisho ilikuwa haijatiwa saini “dili letu liko salama kwa sababu Serikali inahitaji fedha na dili letu linaungwa mkono na timu ya ufundi pamoja na maofisa waandamizi serikalini.”



Dk Mgimwa alipoiingia Mei 2012 mazungumzo yalizorota lakini yalipofufuliwa Septemba 2012 riba ilipandishwa hadi asilimia 2.4 kwa maelezo kuwa asilimia moja ni kwa ajili ya wakala wa Tanzania kampuni ya Egma (Enterprise Growth Markets Advisors Limited).



Benki zote mbili yaani Standard ya Uingereza na Stanbic zilijulishwa na Serikali ilifahamishwa.



Waliosimamia kidete ongezeko la asilimia hiyo moja ni Awale na Sinare. Novemba 2012 yaani miezi miwili baada ya kuipenyeza Egma katika mpango huo na kuilipa asilimia moja, ndipo Serikali iliwasilisha rasmi barua yake kwenye benki ya Standard na Stanbic ya mkopo wa Dola 550 milioni. Hadi mkataba huo unakamilishwa Machi 2013 kiwango cha mkopo kiliongezeka hadi Dola 600 milioni.



Stanbic ndiyo iliilipa Egma Dola 6 milioni (Sh12 bilioni) ambapo Mkurugenzi mtendaji wake Dk Fratern Mboya alizichota katika mikupuo minne kati ya Machi 18 na 27, 2013.



Ufisadi huu umeishtua Serikali ambapo juzi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema Serikali imeanza kuzichunguza benki ya Stanbic na Egma kutokana na kuhusika katika udanganyifu wa riba ya mkopo huo. Tayari Stanbic imekubali kurejesha fedha hizo.

Source;Mananchi

GARI LA WEMA MIKONONI MWA RAIS MAGUFULI

WEMA37 (1)

Hali ni tete! Chanzo kimoja kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kimenyetisha kwamba, kasi ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuhakikisha hakuna Mtanzania anayekwepa kodi imepamba moto na sasa, imetua kwa mastaa wa Bongo ambapo kuna madai lile gari la kifahari la Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu (pichani) aina ya Range Rover Evogue linachunguzuwa na TRA, Amani limenyetishiwa.
SI YEYE TU

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mbali na Wema, mastaa wengine ambao nao magari yao yako kwenye orodha ya kuchunguzwa mwenendo wa kodi ni Jacqueline Wolper Massawe (Toyota Prado), Kajala Masanja (Toyota Hilux) na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (BMW X6).
8
MAELEZO YAKO HIVI

“Unajua serikali imedhamiria kukusanya kodi. Anachotaka Rais Magufuli ni kila mtu mwenye haki ya kulipa kodi ya kitu fulani, afanye hivyo bila kukwepa. Na hakuna kumuonea mtu.

“Sasa bwana…bwana! Huko makao makuu (TRA) hakukaliki, huyo Kaimu Kamishna Mkuu, Phillip Mpango ni mkali balaa, anadhani Magufuli atamzukia wakati wowote wakati cheo kapewa juzi tu. Lakini nasikia Magufuli anataka ripoti mezani kwake.

“Na ujue si magari ya hao mastaa tu ndiyo yako kwenye orodha, hata watu wasio na majina hapa mjini, utaratibu umewekwa kuhakikisha magari yote yanalipiwa kodi kama sheria inavyotaka. Kwa hiyo kama mtu ana malimbikizo, imekula kwake, lazima alipe yote,” kilisema chanzo hicho.

WASIWASI WA VIPATO

Hata hivyo, chanzo hicho kilipoulizwa kama kuwabana mastaa kunatokana na maisha yao ya kifahari huku vipato vyao vikiwa haviko wazi, alijibu: “Ni zoezi. Linazingatia mambo mengi. Pengine hilo limo. Lakini ni zoezi maalum.”
ymCTBkp
AMANI LAWASAKA

Ili kuthibitisha madai hayo, Amani lilianza kuwasaka mastaa hao, mmoja baada ya mwingine ili kuona ukweli wa kuwepo kwa madai hayo.






WOLPER

Wolper alikuwa wa kwanza kutafutwa kwa simu ambapo alipopatikana alishtuka na kusema:

“Yesu! Sijafuatwa na mtu yeyote, lakini na mimi jana (Jumatatu) nimeisikia hii. Lakini mimi nipo oke, ushuru nimeshalipa mwenyewe. Kimbembe kipo kwa wale wenye mbwembwe ndiyo nasikia soo…Teh! Teh! Teh!”

KAJALA

Kajala alipotafutwa kwa njia ya simu ya mkononi juzi, hakupatikana hewani.

WEMA SASA

Amani likamsaka Wema ambaye kwa bahati njema alikuwa hewani na alipokea simu. Baada ya kusomewa madai hayo, alijibu:
wema3
Usumbufu ulianza wakati linaletwa (mwezi Oktoba) lakini haukuwa mkubwa. Ila hivi karibuni walikuja jamaa wa TRA kwa mambo ya miliki. Lakini kuna huyu jamaa yangu (hakumtaja jina) alimalizana nao, ongea naye.”

Jamaa: “Ni jambo dogo tu, wala siyo ishu kubwa. Kwani nani kasema?”

Amani: “Tumezinyaka kivyetuvyetu.”

DIAMOND

Kwa upande wake, Diamond ilionekana kuwa ishu zaidi kwani, licha ya yeye kutojibu meseji baada ya kutumiwa, BMW X6 lake linadaiwa bado lina deni kutoka kwa mtu aliyemuuzia. Na mbaya zaidi, mtu huyo alifariki dunia Aprili, mwaka huu.

MANUNUZI YAO

Wema alisema Range lake alilinunua kwa dola za Kimarekani 90,000 (si chini ya shilingi milioni 200). Diamond yeye awali alisema BMW hilo alipewa na mameneja wake (Said Fella na Hamis Taletale ‘Babu Tale’) ambao walilinunua kwa shilingi milioni 90.

Wolper yeye Prado lake aliliingiza ndani kwake kwa shilingi milioni 60 huku gharama ya gari la Kajala zikiwa hazijulikani.

Wafanyakazi Tanesco, Wachina Kizimbani kwa tuhuma za ufisadi.


Bukoba.Wafanyakazi wawili wa Tanesco na raia wawili wa China wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Kagera kwa tuhuma za kutenda makosa kumi na sita na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni moja.
Watuhumiwa kutoka Tanesco Isaack Tibita na Olver Mushumbusi kwa nyakati tofauti walikuwa mameneja Wilayani Karagwe wanadaiwa kushirikiana na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya Chico kufanya udanganyifu na kujipatia fedha hizo.
Raia wa China katika kesi hiyo ni Wang Lei na Zhang Shuaitong ambao kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa 16 wakati wa kuhamisha miundombinu ya umeme zikiwemo nguzo ili kupisha ujenzi wa barabara ya lami ya Kyaka,Bugene.

Katika kesi hiyo namba 65 ya mwaka 2015 Wakili Mfawidhi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hashimu Ngole alisema watuhumiwa kati ya mwaka 2011 na 2014 kwa nyakati tofauti walitenda makosa hayo na kusababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Miongoni mwa makosa waliyosomewa washitakiwa ni kughushi nyaraka zikiwemo hundi za malipo zinazonyesha kuwa kampuni ya Chico imelipwa fedha kupitia mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya Kyaka Bugene.

Mtuhumiwa wa tatu ambaye ni raia wa China Wang Lei alikuwa meneja wa mradi huo na alisomewa mashitaka mawili peke yake huku mtuhumiwa wa nne Zhang Shuaitong akifanya tafsili kutokana na raia mwenzake kufahamu lugha ya Kichina pekee.

Pia wafanyakazi hao wa Tanesco miongoni mwa mashitaka mengine yanayowakabili ni kughushi nyaraka zilizoonyesha kuwa shirika hilo lilikuwa linadai kulipwa na kampuni ya Chico na kuwa kwa nyakati tofauti walipokea fedha kutokana na nyadhifa zao.


Watuhumiwa wote walikosa dhamana baada ya hakimu Charles Uiso kusema kuwa hakimu anayehusika na kesi hiyo alikuwa na majukumu mengine na itatajwa tena Desemba 7,na kupewa masharti ya dhamana.

Source: Mwananchi

Powered by Blogger.