Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema maagizo ya Rais Magufuli kutaka fedha zilizokuwa zitumike kwa matumizi yasiyo ya lazima, kupelekwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, hayavunji sheria ya manunuzi wala utaratibu mwingine wa kisheria.
Hivi
karibuni,Rais Magufuli aliagiza sh.milioni 225 zilizokuwa nimechangwa
kwa ajili ya hafla ya wabunge zipelekwe Hospitali ya Muhimbili kununua
Vitanda na Mashuka.
Aligiza pia Bilioni 4 zilizokuwa zitumike katika sherehe za Uhuru Disemba 9 zitumike kupanua barabara ya Mwenge- Morocco
Akitoa
ufafanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco, Balozi Sefue amesema mradi
huo sio mpya na kwamba taratibu zote zilishafuatwa ikiwa ni pamoja na
kuwalipa waliokuwa wamejenga kando ya barabara.
Amesema kilichokuwa kinakwamisha mradi huo ni pesa.
Akizungumzia
sakata la wakuu wa mikoa na wilaya kuwanyima likizo wafanyakazi huku
wengine wakitiwa rumande kwa masaa 6, Balozi Sefue amesema serikali
haina taarifa rasmi hivyo akalitaka shirikisho la vyama vya wafanyakazi
(Tucta) kuwasilisha malalamiko serikalini badala ya kuishia kulalamika
katika vyombo vya habari
Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment