Kama ulikuwa na mpango wa kumwambia mwanao aishie ka-digrii kamoja shuleni awahi siasa na uteuzi basi think again enzi hizo zimeisha. Alianza na mawaziri hebu check hii ya makatibu wakuu
Pro. Kamuzora
Pro. Mkenda
Pro. Msanjila
Pro. Gabriel
Pro. Ntalikwa
Pro. Mdoe
Pro. Mchome
Dr. Ndumbaro,
Dr. Mtasiwa,
Dr. Mwinyimvua,
Dr. Turuka,
Dr. Mashingo,
Dr. Budeba,
Dr. Chamuluho,
Dr. Yamungu,
Dr. Kusiluka,
Dr. Meru,
Dr. Akwilapo,
Dr. Ulisubudya,
Dr. Pallangyo,
Dr. Likwelile,
Dr. Aziza,
Eng. Itombe
Eng. Mwihava
Eng. Nyamhaga
Eng. Malingo
Eng. Futakamba
Eng. Emannuel
TAFAKURI: Kwa muda mrefu sana. Wasomi wa nchi hii walisahaulika na kwa maana hiyo wakawa mstari wa Mbele kuikosoa Serikali zilizotangulia na hasa pale mambo yalipokwenda ndivyo sivyo. Rais wa awamu ya Tano, Dr. John Pombe Magufuli amewaona wasomi. Hatutegemei kuona wakimwangusha kwani ukosoaji wao wa serikali zilizotangulia utakosa maana kabisa.
Jambo la pili ambalo sasa vijana na wazazi tunapaswa kuachana nalo ni ile dhana kwmba Siasa ndiyo mpango mzima(ndiyo pa kutokea) , jambo ambalo lilipelekea vijana wetu kuona kama kama stashaha na shahada ya kwanza kama ni viwango tosha vya elimu kuwawezesha kutoka kupitia Siasa. Alichokianzisha Dr. Magufuli huenda kikawa kama mila na desturi ya serikali zitakazofuata.
Thursday, December 31, 2015
Monday, December 28, 2015
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WALIOBAKI

Rais Dkt. John Magufuli akimuapisha Prof. Makame Mbarawa kuwa Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano Ikulu DSM

Rais Dkt. John Magufuli akimuapisha Dkt. Joyce Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia,Ufundi Ikulu.

Rais Dkt. John Magufuli akimuapisha Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Ikulu DSM.

Rais Dkt. John Magufuli akimuapisha Prof Jumanne Maghembe kuwa Waziri wa Maliasilina Utalii Ikulu DSM

Rais Dkt. John Magufuli akimuapisha Mhe. Hamad Masauni kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ikulu DSM

Rais Dkt. John Magufuli akimuapisha Mhandisi Gerson Lwenge kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Ikulu DSM
Monday, December 21, 2015
WAKENYA WAVUTIWA NA MAGUFULI
Ule usemi wa "HAPA KAZI TUU" ambao amekuwa akiutumia sana rais JPM umesababisha rais huyu kuwa kivutio kwa baadhi ya majirani wetu ambao ni wa Kenya wamesema kuwa hiyo kasi aliyokuja nayo Pombe wanatamani kama na wao wangeipata kwa sababu kwa mwezi mmoja tuu Tanzania imeanza kukaa kwenye mstari .
KWELI "HAPA KAZI TUU"
KWELI "HAPA KAZI TUU"
Hatima ya Duni kujulikana Januari
Mwanasiasa mkongwe nchini, Juma Duni Haji amesema hatima yake ya kubakia au kuondoka ndani ya Chadema itajulikana mwezi ujao.Duni aliihama CUF na kujiunga Chadema ambayo ilimsimamisha kuwa mgombea mwenza wa urais wa Chadema iliyokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Vyama vingine vinavyounda Ukawa ni NLD na NCCR Mageuzi.

Tangu kuisha kwa Uchaguzi Mkuu na mgombea wa Chadema kushika nafasi ya pili,* Duni amekuwa kimya, lakini juzi alisema itakapofika Januari mwakani ataeleza mustakabali wake kisiasa.“Kwa sasa sisemi jambo lolote, nitakuambia baadaye kidogo kama nitarudi CUF au nitabakia Chadema. Kuna mambo ninafanya kwanza, nisingependa kusema,” alisema Duni.
Pia, Duni alizungumzia hisia zake za kisiasa visiwani Zanzibar, akisema anashangazwa na kauli ya aliyekuwa Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mark Bomani kumshawishi Maalim Seif Hamad akubali* uchaguzi urudiwe.Siku chache zilizopita, Jaji Boman alinukuliwa na vyombo vya habari akimtaka Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi* Zanzibar kukubali kurudia uchaguzi huo kama ilivyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kuwa utarudiwa ndani ya siku 90
Jecha alifuta matokeo ya urais na uwakilishi wa Zanzibar, akisema kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni na kwamba ndani ya tume yake wajumbe walitofautiana hadi kukunjana.Jaji Bomani alisema kama Maalim Seif alishinda, atashinda uchaguzi ukirudiwa kwani wananchi watampigia kura.
*Hata hivyo, Duni alisema: “Anajua kabisa nchi yoyote inaporudia uchaguzi mara nyingi amani huwa inapotea, kwa mfano Burundi leo hii bado wanauana na hakuna anayezungumza lolote kwa sababu ni chama tawala kimeshinda.“CUF inasisitiza Katiba ya Zanzibar ilindwe au kwa sababu upande wa Bara wamepata Rais (John Magufuli), sasa hawajali usalama wa Wazanzibari?”Duni alihamia Chadema chini ya mpango maalumu wa Ukawa wa kuwezesha vyama hivyo kuchukua urais Bara na Visiwani, mpango ambao haukuweza kuzaa matunda.[/SIZE][/FONT]

picha za mazishi ya dada yake Kikwete

Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiweka mchanga kaburin

Rais John Pombe Magufuli naye alikuwa mstali wa mbele kuwawakilisha watanzania katika mazishi hayo

Rais wa awamu ya pili Alli hassan mwinyi akiweka mchanga

Friday, December 18, 2015
Kwa ufisadi huu wa Manispaa ya Kinondoni, wanastahili kunyongwa
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ameamuru kusitishwa mara moja malipo yanayofanywa kwa makandarasi waliojenga barabara tano za ndani ya wilaya hiyo.
Amefanya hivyo kwa maelezo kuwa watendaji wa Manispaa hiyo, wameshirikiana na makandarasi hao kuiibia serikali Sh bilioni 5.7. Fedha hizo ni ongezeko ambalo makandarasi hao, wanatakiwa kulipwa baada ya kujenga barabara hizo, ambazo thamani halisi ya ujenzi huo ni Sh bilioni tano.
Lakini, katika hali isiyo ya kawaida, makandarasi hao wanatakiwa kulipwa Sh bilioni 10, ongezeko ambalo ni zaidi ya asilimia 100. Akizungumza jana Dar es Salaam, Makonda alisema taratibu za Serikali zinataka kama barabara haikukamilika ndani ya muda uliowekwa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo mvua na sababu zinginezo, mkandarasi anatakiwa kulipwa fedha zaidi ambazo ni asilimia 15 ya thamani ya fedha za mradi.
“Lakini kinachostaajabisha katika miradi hii ya barabara, fedha ambazo zimeongezeka ni zaidi ya asilimia 15, kiasi hiki ni zaidi pia ya asilimia 100, wametumia utaratibu gani kulipa fedha hizi za ziada kwa makandarasi hawa?” Alihoji Makonda.
Alizitaja barabara ambazo watendaji wamezitumia kufisadi fedha za umma kuwa ni ujenzi wa barabara ya Lion kwa kiwango cha lami yenye thamani ya Sh milioni 592.1, lakini nyongeza ya fedha zilizoongezeka ni Sh milioni 860.1 na hivyo kufanya mradi huo kugharimu Sh bilioni 1.4.
Barabara ya kutoka Biafra hadi Embassy, matengenezo yalikuwa ni Sh milioni 507.9 na fedha zilizoongezeka ni Sh milioni 487.5 jumla ya malipo kwa mkandarasi ni Sh milioni 994, barabara ya Mabatini thamani ya mradi ilikuwa Sh milioni 655.5 na fedha zilizoongezeka ni Sh milioni 777.8 na jumla ya mradi kugharimu Sh bilioni 1.4.
Makonda alitaja barabara nyingine zilizojengwa kwa kiwango cha lami zenye ufisadi ni ya Journalism, ambayo ujenzi wake ulikuwa ugharimu Sh bilioni mbili, nyongeza ya fedha katika mradi huo ni Sh bilioni 1.8 na hiyo kufanya mradi huo hugharimu Sh bilioni 3.8, Barabara ya Maandazi ambayo thamani ya mradi ni Sh milioni 799 imeongezwa kiasi cha fedha Sh bilioni 1.2 na hivyo kufanya mradi wote kugharimu Sh bilioni 2.

Dkt. Kigwangalla atumbua MAJIPU ya watumishi wachelewaji wa Wizara ya Afya
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi* muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini

Awali Dkt. Kigwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa 1:32 na kwenda kusimama getini na kisha kuwaamrisha askari wa geti la kuingia katika wizara hiyo kulifunga geti hilo na wasiruhusu mtu yeyote kuingia ndani.
“Fungeni geti na kila atakayefika msimruhusu kuingia ndani ninataka kuona wote ambao wanakuja wamechelewa,” alisikika Dkt. Kingwangalla akiwambia askari wa getini.
Baada ya kutoa amri hiyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Michael John kumpa vitabu vya kusaini kwa vitengo vyote ili aweke mstari wa kuonyesha kuwa muda wa kuingia ofisini umekwisha na akafanya hivyo kwa kuweka mstari kwenye vitabu vya mahudhurio kuwa muda wa kusaini kuingia umeisha.
Baada ya kukamilisha zoezi hilo Naibu Waziri alizungumza na wanahabari kuwa ameamua kufanya zoezi hilo katika ofisi za wizara kwa kutaka kuona ni jinsi gani watumishi wa ofisi hiyo wamekuwa na mwitikio wa kufanya kazi kwa kasi anayoitaka rais, Dkt. John Pombe
Magufuli.

Alisema watumishi hao wameajiriwa na serikali ili kufanya kazi lakini wamekuwa wakichelewa kuingia ofisini na yeye kama Naibu Waziri ana wajibu wa kuwasimamia watumishi hao ili wafanye kazi ambayo serikali imewaagiza kufanya.
“Nina wiki moja tangu nimeingia hapa ofisini kuna mambo ambayo nimeyaona hayapo vizuri na sasa naanza na hili ili tujue kuwa* ni kina nani huwa wanachelewa na zoezi hili litakuwa ni endelevu, kama mimi sitasimamia watumishi wa serikali basi sitakuwa na kazi wizarani tunataka watumishi ambao wanakuwa wanafanya kazi kwa kujitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa,” alisema Dkt. Kigwangalla.
Aidha Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kuhakikisha watumishi wote waliochelewa kufika ofisini wanaandika barua ya kutoa maelezo kwanini wanachelewa kufika ofisini na baada ya hapo Mkurugenzi na yeye atoe maelezo kwanini muda wa kutoka watumishi wanakuwa hawasaini kuwa wametoka.

Pia alishauri uongozi wa wizara ufanye mabadiliko ya mfumo wa watumishi kuingia ofisini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kadi au kidole “Biometric” ili kuwa na taarifa katika mifumo ya mawasiliano kujua wanaochelewa ofisini na wanaowahi kutoka na baada ya hapo uongozi utajadili adhabu za kuwapa watumishi wote ambao wamekuwa wakichelewa kufika na kuwahi kutoka ofisini.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipitia mahudhurio ya watumishi wa wizara kwa siku zilizopita[/SIZE][/FONT]

Wednesday, December 16, 2015
Lowassa kuzunguka nchi kuanzia kesho
Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ataanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura uchaguzi mkuu wa oktoba 25 ambapo yeye alikuwa wapili kwa kupata asilimia 39.9 za kura akitanguliwa na mshindi wa uchaguzi huo ambaye ni Mh rais John Pombe Magufuli aliye shinda kwa asilimia 58.4

hapo kesho ata kuwa Tanga ambapo ata ambatana na Viongozi waandamizi wa ukawa kuwashukuru wananchi kwa namna ambavyo wameunga mkono upinzania na ajenda ya Mabadiliko kwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Breking Newz MELI YA ROYAL YAPATA AJALI YA MOTO
Meli ya Royal iliyokuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba inaungua moto baharini muda huu.
Kwa bahati meli ya Serengeti iliyokuwa inatokea pemba kwenda unguja imeikuta njiani meli hiyo na inatoa msaada wa uokoaji wa abiria na mali.

Powered by Blogger.