Thursday, November 26, 2015

Drogba anataka kuwa kocha wa Chelsea

Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesema kuwa atarejea Stamford Bridge kuwa kocha.Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesema kuwa atarejea Stamford Bridge kuwa kocha.
Drogba, ambaye kwa sasa anasakata soka ya kulipwa huko Canada, aliifungia the Blues mabao 164 katika enzi yake huko Stamford Bridge.
"Ningependa kuihudumia klabu hiyo hata baada ya kukamilika kwa kipindi changu cha uchezaji''
''Tayari nimekubaliana na wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa ninaweza kurejea kuwa mkufunzi kwa sababu klabu hiyo ilinifaa sana nilipoanza'',alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 37.
''Kwani siwezi kuwa meneja ? kwani siwezi kuwa mkurugenzi wa kiufundi,mkufunzi wa chuo cha mafunzo ya wachezaji ama hata mshauri wa washambuliaji ?
Drogba ndiye aliyeifungia Chelsea bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012.
Vilevile aliisaidia Chelsea kunyakwa mataji 4 ya ligi kuu ya Uingereza kabla ya kuhamia Canada kujiunga na Montreal Impact.
Chelsea haijakuwa na mwanzo mzuri katika msimu huu baada ya kushindwa katika mechi 7 kati ya 12 za kwanza msimu huu.
Mabingwa hao watetezi wanashikilia nafasi ya 15 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.
Kumhusu kocha Jose Mourinho, Drogba anasema kuwa mreno huyo angali ana makali ya kuwa kocha wa mabingw hao watetezi.



Drogba ndiye aliyeifungia Chelsea bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012.

''Kama halmashauri inayosimamia klabu inaimani naye inamaanisha kuwa mmiliki wa klabu Roman Abramovich ana imani naye.''
''Ninafikiri kuwa wachezaji wanaimani naye na kuwa anajitolea kwa kila hali ikizingatiwa hali ngumu iliyoko kwa sasa.''
''klabu inawachezaji wenye hadhi ya juu na wanauwezo wa kujifurukuta na kufufua kampeini yao.''Alisema Drogba

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.