Hii ndio zawadi ya Floyd Mayweather kwa mtoto wake aliyetimiza miaka 16…
Bondia maarufu zaidi duniani Floyd Mayweather haishiwi headlines kila wakati na mara nyingi zimekuwa zikihusisha utajiri wake.
Kingine kutoka kwa staa huyo katika ukurasa wake wa @Instagram amepost picha akiwa na mtoto wake wa kiume Koraun pamoja zawadi ya gari mpya aina ya Mercedes Benz C class yenye thamani ya dola 30,000 sawa na zaidi ya fedha za kitanzania milioni 60 aliyomnunulia mwanaye huyo baada ya kutimiza miaka 16.
Hii ndio zawadi inayodhaniwa kuwa ya gharama zaidi kwa staa huyo kuweza kumpa mtoto wake tangu alipotengana na mama wa mtoto huyo.
Wanawake weusi wanaoingiza pesa nyingi zaidi duniani kwa mwaka 2015 !
Katika list ya jarida la Forbes ambalo mara nyingi hutoa list ya watu na pesa zao, Mtangazaji wa TV Mmarekani Oprah Winfrey alishikilia nafasi ya kuwa mwanamke mwenye kipato kikubwa zaidi kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo vinamwingizia fedha.
Mwaka 2014 mtoto wa Rais wa Angola aitwaye Isabel Dos Santos alimpita Oprah na kukamata nafasi ya kwanza mpaka sasa ambapo list kamili ya hao Wanawake weusi watatu ndio hii imekamilika hapa chini.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos
BY, Prince Kibiki
0 comments:
Post a Comment