Saturday, November 28, 2015

MAN CITY YAJIPOZA KWA SOUTHAMPTON

Man CityManchester City leo wamejipoza kwa ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Southampton mchezo ulipigwa kwenye dimba la Etihad, kabla ya mchezo huo Man City ilikuwa na kumbukumbu ya vipigo kutoka kwa Liverpool kwenye mchezo wa ligi ya England kabla ya kuchapwa na Juventus kwenye michuano ya Ulaya.
Kelvin de Bruyne alianza kuifungia City bao la kwanza dakika ya tisa huku Fabian Delph akipachika bao la pili dakika ya 21 kipindi wakati Kolarov akipachika bao la tatu dakika ya 70 na kuihakikishia ushindi timu yake.
Bao pekee la kufutia machozi la Southampton limefungwa na Shane Long 50 na kufanya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa City kutwaa pointi zote tatu na kufikisha jumla ya pointi 26 baada ya kucheza mechi 13.
  Imechapishwa na Shaibu Kibiki - Hapa kazi tu Blog.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.