Monday, November 30, 2015

RC KILIMANJARO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA

MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika masoko manne ya Manispaa ya Moshi pamoja na dampo za kukusanyia uchafu, ili kujionea hali ya usafi na utendaji kazi katika mkoa huo. Katika ziara hiyo, RC Makalla alitumia muda huo kuwaagiza watendaji wake, hususan katika mchakato mzima wa kuifanya Moshi iwe kwenye usafi.




Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla mwenye miwani, akikagua soko lililopo kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumzia ziara yake hiyo, Makalla alitoa siku tatu kwa watendaji wa Manispaa ya Moshi kuhakikisha kwamba lundo la takataka katika soko la Kwasadala linaondoshwa haraka iwezekanavyo. Alisema hawezi kukubali kuona Manispaa hiyo inashuka kiwango chake cha kuifanya Moshi inaendelea kuheshimika katika suala zima la usafi.


Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla aliyesimama mlangoni, akiendelea na ziara yake ya kushtukiza kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

“Pamoja na kuagiza kuondoshwa kwa uchafu huo, pia nataka kuona Mkoa wetu wote unakuwa kwenye hali ya usafi, magari ya usafi yazoe taka kwa wakati, uongozi wa masoko uthamini usafi bila kusahau uongozi wa Hospitali ya Hai unakamilisha haraka ukarabati wa vyoo,” alisema Makalla. Kwa mujibu wa RC Makalla, kitendo cha kuiweka Moshi katika mazingira ya uchafu si tu inaondosha kwa kasi ile heshima yake, bali pia itazalisha ugonjwa wa mripuko, ukiwamo ule wa Kipindupindu unaosikika kuweka katika kambi katika baadhi ya wilaya nchini Tanzania. 


Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla akipata maelekezo kutoka kwa watendaji na watumishi katika Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika sehemu mbalimbali kwenye manispaa hiyo.

 Na, Prince Kibiki

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.