Thursday, November 26, 2015

Man United yatoshana nguvu na PSV - UEFA

Mechi za makundi za michuano hiyo ziliendelea tena usiku wa jana kwa michezo kadhaa katika hatua ya makundi.
Klabu ya Malmo imeambulia kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya Paris Saint Germain ya ufaransa, Shakhtar Donetsk ikichapwa bao 4-3 na Real Madridi.
CSKA Moscow imeambulia kipigo cha mabao 2-0 na Wolf-Sburg, Manchester United ikitoshana nguvu na PSV Eindhoven bila ya kufungana.
Kwingineko FC Astana imetoka sare ya bao 2-2 na Benfica, Atletico Madrid imeifunga Galatasaray bao 2-0.
Borussia Moenche-ngladbach imeibamiza sevilla bao 4-2 , huku Vijukuu vya turini Juventus waikiicha Manchester City bao 1-0.
Mechi hizo za Uefa hatua ya makundi zinatarajia kuendelea tena hapo December 08 mwaka huu kwa michezo miwili ambapo Paris St Germain itaikabili Shakhtar Donetsk.
Na Real Madrid itakuwa ikimenyana na Malmö zikiwa ni mechi za kundi A.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.