Mama wa staa wa muziki Bongo, Sanura Kassim ‘Sandra’.
SINEMA limeanza! Sanura Kassim ‘Sandra’ ni mama mzazi wa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni anadaiwa kuingia katika figisufigisu na mwanaye huyo kwa kumuhoji kama kweli Latiffah ‘Tiffah’ ni damu yake kwa kumzaa na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Amani limenyetishiwa.
Akizungumza na mwandishi wetu Jumatatu ya wiki hii, mmoja wa wanandugu wa Diamond alisema ishu hiyo ilijiri hivi karibuni nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar ambapo mama na mwana hao walikuwa katika mazungumzo ya kawaida.
Ndipo, mama Diamond alipojikuta akiponyokwa na sentensi hiyo ya kuhoji uhalali wa Tiffah kuwa mtoto wa Diamond kauli ambayo awali ilichukuliwa kama utani wa bibi na mjukuu!
‘Kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
‘Yuda’ huyo wa Diamond, alizidi kusema kuwa, mama huyo alijikuta akimtaka Diamond aachane na wazo la kumhesabu Tiffah kama mwanaye kwani hafanani naye hata kidogo na kwamba ameuziwa mbuzi kwenye gunia kama si mfuko wa chumvi!
“Diamond alibadilika sura na kumtaka mama yake aachane na utani wa namna hiyo. Lakini mama alisisitiza kuwa si utani bali ni ukweli ambao amekuwa akivizia autoe kwa njia gani, hivyo siku hiyo aliona ndiyo muda mwafaka wa kutoa la moyoni.
“Kaka (mwandishi), ilibidi Diamond aondoke pale maana anampenda sana mama yake na huwa hapendi kumuudhi. Hivyo ili kuepusha mambo mengine, aliamua kwenda chumbani kwake. Lakini mama haikuishia hapo, alimfuata na kugonga mlango huku akisisitiza juu ya suala hilo.
“Sasa ninavyoongea na wewe, Diamond ana kama siku mbili au tatu hajaonekana nyumbani, anamkwepa mama yake maana naye amekomaa akimtaka mwanaye amuweke wazi anachofahamu kuhusu uhalali wa Tiffah kuwa damu yake,” alisema mtoa habari huyo ambaye ombi lake kubwa kwa mwandishi wetu ni hifadhi ya jina lake ili kuepuka kuonekana ni ‘kikulacho’ cha familia hiyo.
Kama kawaida ya gazeti hili, ambalo ni mashine bab’kubwa kwa habari za ndani za mastaa wa Bongo, kujiridhisha na kila habari kabla ya kuichapisha na kuipeleka kwa msomaji, ‘kiranja mkuu’ wa dawati alimtafuta mama huyo kupitia simu yake ya mkononi ambapo aliposomewa madai hayo mpaka mwisho, aliishia kusema:
“Jamani, kwanza mimi naumwa! Sitaki kabisa maswali magumu kiasi hicho cha kuumiza kichwa, niacheni na familia yangu,” (akakata simu na kuizima).
Amani lilimsaka Diamond mwenyewe kwa njia ya simu kwa kumtumia meseji na ilimfikia (deliva) lakini hakujibu kitu.
Agosti mwaka huu, Zari alimzalia Diamond mtoto huyo na kuibua hisia tofauti kutoka kwa wadau, hasa wa nchini Uganda ambako Zari ana asili nako, wakidai mtoto huyo si wa Diamond.
Hata hivyo, Diamod amekuwa akisema Tiffah ni mtoto wake na ana uhakika na hilo