Home »
KITAIFA
» Jokate Adai Alimpenda Sana Hasheem Thabeet, Ataja Sababu za Kuachana Naye
Hasheem Thabeet kwa mujibu wa Jokate Mwegelo, alikuwa ni ‘first love’ na huenda kuachana naye kilikuwa ni kitu kibaya zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake.Mrembo huyo alikuwa akijibu swali la PapiChulo_Chuly kwenye Twitter aliyeuliza, “Ni tukio gani baya huwezi sahau maishani?”“Kumwacha mtu ambaye nilikuwa nishapanga vitu vingi sana nae kichwani. Very very disappointing but it’s life,” alijibu Jokate.October 2013, kwenye jarida la Vibetz, alifunguka kuwa japo uhusiano wake na Hasheem ulidumu kwa miaka mitatu, walifanikiwa kuufanya usijulikane sana kwa wengi na walikuwa wakipendana sana.“With Hasheem, I think it was more than love. He was my first real love,” aliliambia jarida hilo.“Siku zote nilidhani he was my soulmate. Kiukweli nilimpenda sana. He is like the only guy I would drop anything at anytime for. Nilikuwa tayari kufanya lolote kwaajili yake, that’s how deep I loved that guy,” aliongeza.“Nilimpenda kiukweli Hasheem, and yes kama mwanamke mwenye kutaka kufanikiwa I’m drawn to ambitious/successful men, you know the go getters but my family haikunilea katika maadili ya kujenga mahusiano yoyote katika mhimili wa fedha,” Jokate alieleza kujibu swali kama aliamua kuwa na Hasheem kwasababu ya fedha zake. “I had never wanted to use Hasheem, all I wanted was to love him.”Jokate alidai kuishi mbali na Hasheem ni moja ya sababu iliyochangia kuvunjika kwa uhusiano wao.“Yes kuishi mbalimbali pia inaweza kuwa sababu japo ndogo iliyochangia kuvunjika mahusiano yetu cause sometimes I would hear a lot of stuff and that would upset me. Nilikuwa naogopa sana kumpoteza, I ended up doing vitu vya kijinga kama dating Diamond. I had issues with Hasheem na Diamond came in picture. It was a very frustrating time for me. I was super confused. I cried for a whole year. Like every night I would just cry like crazy.”Kwa sasa Jokate ana uhusiano na Alikiba
0 comments:
Post a Comment