Wednesday, November 16, 2016

Mgonjwa ashindikana kutibiwa Muhimbili kwa kuwa mrefu kuliko binadamu wa



Kijana Baraka Elias Mashauri mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Musoma mkoani Mara ameshindwa kupata matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na urefu wake usio wa kawaida.

Baraka anayesumbuliwa na tatizo ya nyonga ana kimo kirefu cha zaidi ya  futi 7 na hii kufanya kushindwa kupatiwa matibabu kufuatia vifaa katika taasisi hiyo ikiwemo mashine za X- ray vitanda vya kufanyia upasuaji kuwa vifupi ukilinganisha na urefu wake.

Tatizo hilo la nyonga linalomsumbua Baraka limemfanya ashindwe kutembea na kulazimika kutumia magongo ambayo anasema yanamtesa kutokana na urefu alionao.

Akizingumzia jinsi watu wanavyomshangaa kutokana na urefu wake alisema kuwa kwake anaona fahari kwani ni maisha ambayo ameyazoea kila anapokwenda. Amesema kuwa hiyo haimpi shinda kwani anajua wanamshangaa kutokana na urefu wake kitu ambacho si kibaya.

Kuhusu ugonjwa unaomsumbua na baada ya kushindikana kupatiwa matibabu nchini, Baraka ameomba wasamaria wema waweze kumsaida ili apatiwe matibabu nje ya nchi ili arudie  kwenye hali  yake ya kawaida kwani magongo anayotumia kutembelea yanamtesa.

Hapa chini ni video yake alipokuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mifupa. TAZAMA VIDEO: 

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.