Tuesday, November 22, 2016

Chemical: Kwanini Watu Wanashindwa Kuamini Kuwa Mimi ni Bikira?



Rapper wa kike mwenye swaga za hatari Chemical amesema anashangazwa kwa kitendo cha baadhi ya watu wanaompinga kuwa hajawahi kufanya mapenzi.

Hitmaker huyo wa ‘Am Sorry Mama’ amekiambia kipindi cha Kubamba cha Times FM, kuwa aliwahi kuwa na mpenzi lakini waliachana kwa kuwa alikuwa na haraka ya kufanya mapenzi.

“Sijawahi kufanya mapenzi hata siku moja. nimeachana na mpenzi wangu kwa sababu hataki kusubiri, nipo single sasa hivi. Sijui watu kwanini hawaamini wanahisi ni kitu ambacho hakiwezekani aisee,” amesema Chemical.

Kwa sasa rapper huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Mary Mary’ aliouachia siku chache zilizopita


0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.