Monday, November 14, 2016

Nchi Kumi Zinazoongoza Kwa Kuwa na Wasichana Warembo Barani Afrika



Afrika ni miongoni mwa Bara lililobarikiwa tamaduni, lugha na watu tofauti wenye tabia zinazoshabihiana ikiwamo ukarimu.

Miongoni mwa watu wa Bara hili wapo wasichana warembo wa kuvutia tofauti na wengine, katika hili kuna mjadala mpana huku baadhi wakikubali kuwa kuna watu wanaovutia kuliko wengine huku baadhi yao wakidai kuwa uzuri, urembo wa mtu unatafsiriwa kulingana na anayemtizama.

Lakini katika hili tukubali tukatae miongoni mwa wanawake wa Afrika bila kujali wanatizamwa na nani ni wazuri na warembo na wanavutia kuliko wengine.

Ifuatayo ni orodha ya nchi 10 zenye wanawake wenye mvuto barani Afrika, mwaka jana Tanzania ilishika nafasi ya 10 mwaka huu imepanda nafasi moja na inashika nafasi ya tisa.

10: Ghana

Nchi ya Ghana inashika namba 10 kwa kuwa na wanawake wazuri Barani Afrika kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Machi mwaka huu na tovuti mbalimbali za masuala ya urembo ikiwamo Afrojuju, Urbanviralmedia.

Jambo wanalolingana wanawake wa Ghana kuwa wana mvuto wa asili ambao huuongezea kwa kujiremba.

Mwaka jana Ghana ilishika namba nane, mwaka huu imeshuka nafasi mbili na kushika nafasi ya 10.

9: Tanzania

Nafasi ya tisa mwaka huu imeshikiliwa na Tanzania iliyokuwa inashikilia nafasi ya 10 mwaka jana hivyo imepanda nafasi moja.

Miongoni mwa sifa za wanawake wa Tanzania ukiachilia mbali uzuri wa asil ni ni pamoja na kutunza nyumba, ujuzi wa kukisafisha chumba na kukipamba. Katika orodha hii wametajwa kuwa wanawake bora wachapa kazi na wanaojali familia.

8: Kenya

Imepanda nafasi moja kwa kuwa mwaka jana ilishika nafasi ya tisa.

Sifa za wanawake wa nchi hiyo ni pamoja na kuwa wajuzi katika mapenzi, wachapa kazi na watuamiaji wa pombe, jambo linalowatofautisha na watu wengine ni rangi yao ya kuvutia.

7: Nigeria

Kwa miaka miwili mfululizo warembo wa Nigeria wanashikilia nafasi ya saba.

Wanawake wa Nigeria licha ya kuwa na rangi za kuvutia, pia wana maumbo ya yaliyojazia na wamejaaliwa kuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi, kati ya 1970 na 2011 Nigeria iliongezeka idadi ya watu mara tatu na kuifanya kuwa nchi yenye wakazi wengi barani Afrika. Kama unataka mwanamke mzuri na atakayekuzaliwa watoto wengi Nigeria inakuhusu.

Kwa wale wanaotaka mwanamke mwenye sifa za kuwa mke, wa nchi hiyo wanafaa. Sifa ya kipekee wanajua kupika na kutunza familia.

6: Ivory Coast

Mwaka huu namba sita imeshikiliwa na Ivory Coast ambayo mwaka jana haikuwepo kabisa, hivyo imeingia kwenye 10 bora kwa mara ya kwanza, nafasi hiyo mwaka jana ilishikwa na nchi ya Afrika Kusini.

5: Afrika Kusini

Nchi hii imewapa jina warembo wake “Upinde wa Mvua wa Taifa”. mwaka huu imepanda nafasi moja kutoka nafasi ya sita iliyoshika mwaka jana.

Ni miongoni mwa nchi zenye wasichana warembo wa kuvutia katika Bara la Afrika. Miji ya Cape Town, Johannesburg, Pretoria na Durban ndiyo yenye wanawake wenye mvuto. Wanawake wa Afrika Kusini wanang’aa na kuvutia kutokana na ngozi zao nyororor.

Unapofika nchini humo hasa katika Jiji la Pretoria kuwa makini kwa sababu unaweza kugongwa na gari kutokana na kuwashangaa warembo hao ambao kwa kawaida huvaa tofauti kidogo, nguo zao huwa fupi.

4: Rwanda

Wanaume wao hujivunia kwa kuwaita “Tufaa Lililojificha”, mwaka jana nchi hiyo ilishika nafasi ya kwanza kwa kuwa na wanawake warembo, mwaka huu imekamata nafasi ya nne.

Wanawake wa nchi hii sifa ya kipekee ikiwamo urefu unaopendeza, shepu ya Kiafrika kabisa, wasomi na wanaotaka kufahamu kila jambo.

Kitu kinachowafanya wawe juu licha ya kuwa warembo, ni wachapa kazi wanaojali muda na kupigania wanachokitaka bila kujali wanapambana na nani na ana nafasi gani ikiwamo kutoogopa mashindano na wanaume katika nyanja mbalimbali ikiwamo za kisiasa, kielimu au kiutendaji.

3: Somalia

Sifa yao maarufu na wanayopendwa kuitwa na wanaume wa nchi yao ni “Vita Aiharibu Urembo”, mwaka jana walishika nafasi ya pili. Licha ya urembo na kuwa karibu maeneo mengi katika Bara la Afrika bado wana utamaduni wa kuoana wao kwa wao. Wanatajwa pia kuwa miongoni mwa wanawake wanaoamini katika ndoa na kuitendea haki.

2: Eritrea

Ni miongoni mwa nchi zenye wanawake wenye mvuto barani Afrika, licha ya asilimia kubwa ya wanawake wake kujihifadhi kwa kuvaa ushungi na mavazi marefu bado asili ya urembo wao ipo pale pale.

1: Ethiopia

Wanawake wa nchi hii huitwa “Asili ya Ubinadamu”. Huo ni utambulisho wao mbele ya macho ya dunia.

Inaelezwa kuwa ustaarabu kwa wanawake ulianzia katika Ethiopia, hivyo inatajwa kuwa ni nchi yenye wanawake wenye mvuto zaidi barani Afrika.

Wengine wanasema matokeo ya mvuto wao yanatokana na mchanganyiko wa watu wa kale wa Yemen na Ethiopia. Wakati mwingine inakuwa ngumu kuwatofautisha kutokana na baadhi yao kufanana sana, maumbile, sura na uzungumzaji.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.