Tuesday, November 22, 2016

Diamond Aelezea Sababu ya Kujiita Jina la Diamond Platnumz



Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii wakubwa barani Afrika kwa sasa. Siku za hivi karibuni alipata nafasi ya kushiriki tamasha la muziki la Coke Studio Afrika kusini ambapo alitengeneza wimbo uliowavutia wengi kwa kushirikiana na Cassper Nyovest, wimbo unaitwa My Heart.

Akiwa katika tamasha hilo alifanya mahojiano na waandaaji na moja ya yaliyowavutia wengie ni alipoeleza jinsi alipopata jina lake la sanaa ‘Diamond Platnumz.’

Akielezea chanzo cha jina hilo, Naseeb Abdul Juma alisema kuwa jina hilo lilianza kitambo alipokuwa akiimba ambapo rafiki zake mtaani walikuwa wakimwambia kuwa yeye ana kipaji kizuri cha kuimba na siku akipata mtu wa kukiendeleza, ataweza kuwa mwenye thamani kama Diamond.

Alieleza kuwa katika kipindi hicho walianza kumuita jina hilo la Diamond na kwavile hapakuwepo na msanii yeyote anayetumia jina hilo, akawaza kwanini asilitumie. Ndipo na yeye akaaza kujiita Diamond.

Akifafanua lilipotekea jina Platnumz, Naseeb alisema kuwa neno hilo lina maanisha mtu mtanashati mwenye swaga, mwenye muonekano wa kuvutia na mtu wakupendeza kila mara. Hivyo akajiita Diamond Platnumz na ukawa ndio mwanzo wa jina lake hilo.

Msikilize Naseeb Abdul Juma akielezea hapa chini. Vipande vingine vya mahojiano aliyofanya ameviweka kwenye ukurasa wake wa Instagram.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.