Tuesday, November 29, 2016

Daktari Feki Afanya Upasuaji Wagonjwa 9 na Kufariki Mmoja, Apewa Ofa ya Kujiendeleza Kielimu



KENYA: Kamati ya maswala ya afya nchini Kenya imependekeza daktari feki aliyekamatwa nchini humo aruhusiwa kujiendeleza na masomo ya udaktari badala ya kutumikia kifungo gerezani.

Kauli hiyo imetolewa baada ya kubainika kuwa daktari huyo feki alifanikiwa kufanya upasuaji kwa wagojwa tisa ambao kati ya yao wanane walipona na mmoja ambae alikuwa mjamzito ndiye aliyepoteza maisha huku akifanikiwa kumuokoa mtoto aliyekuwemo tumboni mwa mjamzito huyo.

Watu 76 Wamethibitika Kufariki Dunia na 5 Kunusurika Katika Ajali ya Ndege



Watu 76 wamethibitika kufariki dunia na 5 kunusurika baada ya ndege ya wachezaji kutoka Brazil kuanguka asubuhi ya leo. Kati ya waliofariki 22 ni Waandishi wa Habari.

Timu Atlético Nacional ambayo ilipaswa kucheza wa kwanza wa fainali dhidi ya timu ya Chapeonense yaomba Shirikisho la Soka barani Amerika Kusini(CONMEBOL) kukabidhi kombe kwa timu hiyo.

Msemaji wa Uwanja wa Ndege wa Medellin Bwana Jose Maria Cordova amesema kuwa ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya hewa katika ukanda huo, kwani kupitia Sattelite radi na mawingu mazito yalionekana katika anga

Alikiba Asherehekea Siku ya Kuzaliwa Kwa Kutembelea Mbugani



Leo ni siku ya kuzaliwa ya Alikiba. Na kusherehekea siku hiyo muhimu kwake, muimbaji huyo mahiri alitumia private jet kwenda na timu yake ya Rockstar4000 akiwemo Barakah Da Prince kwenda mbugani. Chini ni picha alizoweka kwenye Instagram


Friday, November 25, 2016

Chemical: Kwanini Watu Wanashindwa Kuamini Kuwa Mimi ni Bikira?



Rapper wa kike mwenye swaga za hatari Chemical amesema anashangazwa kwa kitendo cha baadhi ya watu wanaompinga kuwa hajawahi kufanya mapenzi.

Hitmaker huyo wa ‘Am Sorry Mama’ amekiambia kipindi cha Kubamba cha Times FM, kuwa aliwahi kuwa na mpenzi lakini waliachana kwa kuwa alikuwa na haraka ya kufanya mapenzi.

“Sijawahi kufanya mapenzi hata siku moja. nimeachana na mpenzi wangu kwa sababu hataki kusubiri, nipo single sasa hivi. Sijui watu kwanini hawaamini wanahisi ni kitu ambacho hakiwezekani aisee,” amesema Chemical.

Kwa sasa rapper huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Mary Mary’ aliouachia siku chache zilizopita.

Paul Makonda Alivyoamuru Mwenyekiti Mwingine Akamatwe Katikati ya Mkutano



November 24 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salam, Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku 10 ambayo lengo ni kukutana na wanannchi kwa ajili ya kusikiliza kero zao. Ilikuwa ni zamu ya Ilala na hapa ulikuwa ni mkutano wa hadhara Chanika, katika mkutano huo ulitawaliwa na kero kubwa moja ambayo ni suala la ardhi.

Moja ya kero iliyowasilishwa ni kuhusu mwenyekiti wa mtaa wa Zavala ambaye anatuhumiwa kuuza ardhi kinyume cha sherialikiwemo eneo lililotengwa kwa ajili ya kuhamishia wananchi wa kata ya Kipawa ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege.

RC Makonda baada ya kuwasikiliza baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa waliotoa ushuhuda kuhusu tuhuma hizo aliamuru mwenyekiti kukamamtwa katikati ya mkutano. Unaweza kuangalia ilivyokuwa kwenye hii video hapa chini.

Kampeni ya Kumng’oa Trump Yashika Kasi


Ndoto za Donald Trump aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa 45 wa Marekani huenda zikayeyuka baada ya wajumbe sita wa Democratic watakaopiga kura za majimbo kuanzisha kampeni maalumu ya kuwashawishi wajumbe wengine kutomwidhinisha Rais huyo mteule.

Wajumbe hao ambao majina yao yalitangazwa jana wanaamini kuwa iwapo watafanikiwa kuwashawishi wenzao wengine 37 kutoka Chama cha Republican basi watakuwa wamefanikiwa kumzuia bilionea huyo kuingia ikulu.

Desemba 19 wajumbe 538 kutoka majimboni watakutana kupiga kura ya kisheria kumthibitisha Rais mteule anayetarajiwa kuapishwa Januari 20. Kura hizo zitahesabiwa mbele ya Bunge la Congress Januari 6.

Hatua ya wajumbe hao wa Democratic kuanzisha kampeni hiyo imekuja siku chache baada ya makundi ya kiharakati kuanza kukusanya saini nchi nzima ili kuwashinikiza wajumbe hao kutompitisha rais huyo ambaye tayari ameanza kutangaza vipaumbe vyake.

Mmoja wa wajumbe hao aliyetambulika kwa jina la Michael Baca anayewakilisha Colorado amekuwa akizunguka huku na kule kuwashawishi wajumbe wenzake kuepuka kumuunga mkono Trump wakati wa upigaji wa kura.

Mjumbe mwingine ambaye hakupenda jina lake kutajwa alisema kutokana na mvutano unaoendelea kujitokeza sasa kunaweza kuzusha hoja zitakazolazimisha kuangaliwa upya kwa mfumo unaotumika sasa kupitia kura za majimbo kumchagua rais.

Ingawa bado haijajulikana ni wajumbe wangapi wanaendelea kuwa waaminifu kwa kambi ya Trump lakini mchambuzi wa masuala ya siasa, Profesa George Edwards III amesema kama kutatokea wajumbe nane au 10 wakaamua kutomuunga mkono rais huyo mtarajiwa basi kunaweza kubadilisha ndoto za kiongozi huyo kuingia ikulu Januari 20 mwakani.

Tayari wafuasi hao wameitisha kampeni ya kuomba Wamarekani kuwaunga mkono mtandaoni kupitia tovuti ya www.change.org wa kuwashawishi wachaguaji hao kumchagua Clinton badala ya kumthibitisha Trump kwa kuwa hafai kuwa rais wa taifa hilo.

Ujumbe huo unaeleza kuwa iwapo watachagua kama ambavyo majimbo yamepiga kura katika uchaguzi huu, Trump atashinda.

“Hata hivyo, wanaweza kumpigia Hillary Clinton wakiamua,” inasomeka sehemu ya kampeni hiyo yenye kichwa cha habari; “Kura ya uamuzi: Mfanye Hillary Clinton kuwa rais Desemba 19”.

“Hata katika majimbo ambayo wajumbe hawatakiwi kufanya hivyo, wakiamua kura zao zitahesabika, wanaweza wakafanya uamuzi kidogo ambao tutaamini wafuasi wa Clinton watavutiwa nao.”

Mtandao huo unaeleza kuwa Clinton alishinda kura ya wengi hivyo anafaa kuwa rais kwa kuwa Trump alishinda majimbo yenye kura nyingi za majimbo basi mwenendo ukaonyesha bayana kuwa atashinda kura za uamuzi.

Katika uchaguzi uliofanyika Novemba 8 mwaka huu, Wamarekani waliwachagua wagombea wa urais kwa kura ya wengi na kuchagua wapigakura watakaomchagua rais mteule mwezi mmoja ujao.

Clinton aliongoza kura za wengi kwa zaidi ya kura 200,000 lakini Trump aliibuka mshindi kutokana na kushinda majimbo yenye kura nyingi za majimbo.

Ili Rais ashinde kinyang’anyiro hicho, anatakiwa kushinda kura 270 kati ya kura 538 zilizopo kutoka majimboni.

Kwa kutumia mfumo wa mshindi wa jimbo anashinda pia kura za uamuzi. Hadi sasa Trump ana kura 306 wakati mpinzani wake, Clinton akiondoka na kura 232. Ni mara chache kwa Marekani mshindi wa urais kuzidiwa katika kura za wengi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Fordham, Christina Greer alisema kati ya wajumbe 538 watakaopiga kura mwaka huu, 100 ni maseneta ambao ni wawili kila jimbo, wajumbe watatu kutoka makao makuu ya nchi, Washington D.C, na wabunge 435.

“Majimbo yote kasoro mawili ya Maine na Nebraska mgombea mwenye kura nyingi kwenye jimbo basi ndiye mshindi pia wa kura za wajumbe.

“Hii ina maana matokeo yakitoka tu mwenye kura nyingi huwa ni mshindi licha ya kura kusubiri kura za uamuzi Desemba 19,” Dk Dreer.

Hata hivyo, matumaini ya wafuasi hao wa Clinton huenda yasizae matunda kwa kuwa sheria za majimbo mengi likiwamo la Minnesota Marekani zinakataza uwepo wa “wajumbe wasiowaaminifu” na baadhi yanatoza faini kati ya Dola 500 (Sh1 milioni) za Marekani hadi 1,000 (zaidi ya Sh2 milioni).

Faini hiyo ni matokeo ya uamuzi wa Mahakama juu ya nchi hiyo iliamua mwaka 1952 wapigakura hao wawe wanakula viapo mapema wakati wa mkutano mkuu wa chama juu ya nani watamchagua, mtandao wa Factcheck.org unaochapisha habari za siasa, umeeleza.

Timu Lipumba, Maalim Seif zatwangana Mahakamani


KATIKA hali isiyo ya kawaida, wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), jana waligeuza Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, kuwa ukumbi wa masumbwi baada ya kutwangana baadhi yao walipojaribu kumzuia Profesa Ibrahim Lipumba kuingia kusikiliza kesi inayomhusu.


Watu hao ambao walikuwa wamevaa sare za chama hicho, walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili, moja likiwa kwa Profesa Lipumba, ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Upande mwingine ulikuwa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama hicho, Abdallah Khatau, wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ambao wamefungua kesi ya kupinga uenyekiti wa kutambuliwa na Msajili.

Jana saa 2:45 asubuhi, wafuasi wa pande zote mbili katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, zilikuwa zimetanda kwenye korido za mahakama hiyo wakisubiri kuingia chumba cha korti kusikiliza shauri hilo.

Hata hivyo, baada ya mawakili kuingia katika ofisi ya Jaji Sekiet Kihio kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo, baadhi ya wafuasi hao walisimama mlangoni kumzuia Profesa Lipumba na watu wake wasiingie kwenye chumba hicho.

“Huwezi kuingia ndani hadi mawakili waingie", "kaja kufanya nini wakati kesi haimuhusu," "ondoka Lipumba…,” walisikika wakisema baadhi ya wafuasi hao.

Hatua hiyo ilisababisha wafuasi wa Prof. Lipumba kuanza kupiga kelele huku wakitaka wenzao wanaomzuia kutoka mlangoni ili aweze kuingia kusikiliza kesi hiyo.

Tukio hilo lilikuwa kama sinema baada ya timu ya Prof. Lipumba kumnyanyua juu juu mtu aliyesimama mlangoni kumzuia mlalamikiwa huyo kuingia mahakamani na baadaye walimshushia kipigo huku moja wao akisikika akisema “mnataka kuharibu kesi, toka hapa mlangoni na usirudi tena."

Wakati 'sinema' hiyo ikiendelea hakukuwa na askari eneo hilo hivyo kufanya fujo hizo zidumu kwa zaidi ya nusu saa mpaka askari polisi na magereza walipofika na kufanikiwa kuwatuliza wafuasi hao na Prof. Lipumba kuingia kusikiliza kesi yake.

Ndani ya chumba cha mahakama, Jaji Kihio aliwalaumu mawakili wa pande zote mbili kwa kuonyesha utovu wa nidhamu mahakamani hapo na kwamba hawakustahili kufanya hivyo.

“Nasikitika sana kwamba ninyi wote ni watu wazima inakuwaje mnaanzisha vurugu wakati kesi yenu imepangwa kwa ajili ya kutajwa?

“Kesi yenu inatajwa kwa dakika tano, nashangaa mnaamua kupigana, mawakili siku nyingine mnatakiwa kutoa taarifa kuwa mmekuja na wafuasi wengi ili twende mahakama ya wazi,” alisema Jaji Kihio.

Wakili wa Mlalamikaji, Juma Nassoro, aliomba Jaji Kihio ajitoe kusikiliza kesi hiyo.

Alidai kwamba wamewasilisha pingamizi dhidi ya majibu ya walalamikiwa kwa madai kwamba yana upungufu wa kisheria.

Alidai kuwa viapo vya walalamikiwa vina upungufu wa kisheria na kwamba vilitoa maelezo ya uongo pamoja na muapaji kuweka maelezo ya kuambiwa.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata, aliwasilisha pingamizi la awali kwamba mahakama hiyo haijatoa kibali cha kufungua kesi dhidi ya walalamikiwa.

Jaji alisema kuhusu suala la kuombwa ajitoe bado hajapokea barua kutoka upande wa mlalamikaji na kwamba akipokea barua hiyo atatoa uamuzi siku ya kusikiliza pingamizi Desemba 6.

Mbali na Msajili, walalamikiwa wengine katika kesi hiyo ya madai namba 23/2016 ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Prof. Lipumba na wanachama wengine 11 wa CUF

Rais Magufuli Aongea na Makonda Live Akiwa Kwenye Mkutano wa Wananchi



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amempigia simu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuongea naye ‘live’ akiwa katika mkutano wa ziara yake ya wilaya ya Ubungo ya kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuzitatua.

Makonda alimpigia simu mkuu huyo wa nchi ili kuomba ufafanuzi juu ya changamoto za wananchi wa Ubungo hasahasa kwa wale ambao wanabomolewa nyumba kutoka na utanuzi wa barabara. Sikiliza Hapa:

Shirikisho la Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Tahliso) Watoa Tamko Kali Kwa Bodi ya Mikopo



Dar es Salaam. Shirikisho la Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Tahliso) imevikumbusha vyuo vikuu nchini mambo wanayotakiwa kufanya ikiwamo kuelewa mikataba na nafasi ya wanafunzi katika masuala ya malipo ya ada vyuoni mwao.

Katika waraka wake uliotolewa kwa vyombo vya habari, Tahliso walilaani vikali kitendo cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino kutangaza kuwazuia wanafunzi kufanya mahafali kwa kisingizio cha ada.

“Tahliso tumepokea malalamiko yenye kusikitisha kutoka kwa wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) - MWANZA ambao wamehitimu katika mwaka wa masomo 2015/2016” amesema  Stanslaus Kadugalize, Mwenyekiti wa Tahliso

Waraka huo umesema Mkataba wa malipo ya ada ni kati ya vyuo hivyo na HESLB na kuwa zipo taratibu zinazotumika kulipana ada hizo kati ya vyuo na Serikali kupitia HESLB;

“Wanafunzi hawajawahi kushiriki katika kupanga ada hizo, kufuatilia malipo ya ada hizo wala kutafuta fedha za kulipa ada hizo.” umesema waraka huo na kuongeza:

“Kwa sababu hizo, TAHLISO tunapinga vikali hatua hiyo iliyochukuliwa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino na kuwataka wakuu wa taasisi za elimu ya juu nchini kutozuia wanafunzi kuhitimu masomo yao.”


Katika waraka huo Tahliso ilizitaka taasisi za elimu ya juu ambazo zinadai ada kutoka HESLB, kufuata utaratibu uliopo ambao umezoeleka wa kuidai HESLB na sio kuwaadhibu wanafunzi wahitimu

Ushindi wa KRC Genk ya Mbwana Samatta Unaowafanya Watinge hatua Inayofuata Europa League



Usiku wa leo November 24 2016 timu ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ilicheza mchezo wake wa tano wa hatua ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya timu ya Rapid Wien ya Austria.

KRC Genk katika mchezo huo wa tano walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Luminus, Genk wakiwa nyumbani walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 55 dhidi ya wageni wao Rapid Wien, kitu ambacho kimewasaidia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 11.

Kwa matokeo hayo Genk na Atletico Bilbao wanafuzu hatua inayofuata kutokana na wote kuwa na point 9 wakati Rapid Wien na Sassuolo ya Italia watakuwa wanasubiri mchezo wa mwisho wa kukamilisa ratiba, maana hata wakishinda watakuwa na point nane kila mmoja, point ambazo hazitoshi kuipiku Genk wala Atletico Bilbao.

Mwanaume Aliyekuwa Akijifanya Mwanamke na Kutapeli Wanaume Akamatwa



Mwanaume mmoja nchini Uganda aliyefahamika kwa jina la Ivan Bebeto amekamatwa na Polisi akidaiwa kuwa amekuwa akijifanya yeye ni mwanamke na kuwatapeli wanaume.

Mwanaume huyo anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Katwe jijini Kampala akidaiwa kuwa hujifanya mwanamke ambapo huvalia mavazi ya kike na kujiweka kama mwanamke kisha kuwatapeli wanaume. Taarifa kutoka nchini humo zimeeleza kuwa mtuhuiwa huyo amekuwa akifanya ujanja huo kwa muda mrefu sasa hasa katika miji ya Nairobi, Kampala na Bujumbura.

Akiwa katika muonekano wa kike, mtuhumiwa huyo hujiita Queen.

Aidha, siku ya tukio hilo alikamatwa baada ya mwanamume mmoja aliyekuwa tayari amekubaliana nae kuanza kumtilia mashaka baada ya Bebeto kukataa kwenda nyumba ya kulala wageni kama walivyokuwa wamekubaliana kabla ya kupewa malipo.


Baada ya hali hiyo, mwanaume huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja alipiga simu Polisi na ndio Bebeto akakamatwa.

Rais Magufuli: Niliivunja Bodi ya TRA Baada ya Kuidhinisha Mabilioni ya Pesa Kwenda Benki Binafsi Kama Fixed Deposit



Novemba 20 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu na kuivunja hiyo bila kueleza sababu zozote.

Rais John Magufuli ameeleza sababu za kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuwa ilitokana na bodi hiyo kuidhinisha mamlaka hiyo kuweka mabilioni ya fedha kwenye benki binafsi

Novemba 20 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu na kuivunja hiyo bila kueleza sababu zozote.

Akizungumza leo wakati wa sherehe za mahafali ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani, Rais Magufuli amesema kuwa TRA walichukuwa fedha mabilioni na kuweka fixed account benki 8 binafsi na bodi ikaidhinisha.

Tuesday, November 22, 2016

Mwenyekiti Aomba Kupigwa Risasi Mbele ya Makonda Baada ya Kubanwa na Wananchi



Mwenyekiti soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mokiwa Hassani ameomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo.
mokio-hassan
Mwenyekiti akijitetea mbele ya Wananchi

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika manispaa ya Temeke.

Unaweza ukadhani ni masihara lakini ndivyo hali halisi ilivyokuwa baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kutoa nafasi kwa wakazi wa Mbande hususan wafanyabiashara wa soko hilo kutoa kero zao.

Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti wa soko hilo Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo na kufafanua kuwa bei hiyo ya shilingi laki nne kwa kizimba ni makubaliano kati yao na wananchi hao, pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuendesha soko hilo, ambalo bado halijakabidhiwa kwa Halmashauri.

Kufuatia utetezi huo ikamlazimu Mkuu wa Mkoa kutumia busara ambapo ameuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kusimamia uundwaji wa uongozi wa soko hilo haraka mpaka kufikia mwezi Desemba kero zinazolikabili soko hilo ziwe zimetatuliwa

Ndoa Ina Mwaka Sasa Inanishinda, Sina Hamu ya Kufanya Tendo la Ndoa na Mke Wangu



Naombeni ushauri jamani,

Nimeoa na ndoa yangu ina mwaka sasa. Mke wangu ana tabia nzuri sana kiasi kwamba kila mtu ananisifia kuwa nimepata mke bora.Tatizo linakuja kitandani, yaani si enjoy chochote kile kutoka kwake najikuta sina hamu naye kabisa hali inayopelekea niwe nasingizia naumwa ili asiombe mechi.

Na nilimuoa kwa sababu ya tabia yake na hatukusex mpaka ndoa! Nashindwa kutoka nje kwa sababu ya heshima niliyonayo ndani ya jamii na pia kuheshimu ndoa yangu na isitoshe kwa sasa tuna mtoto mchanga. Ana maumbile makubwa na pia maji mengi nimefikia hatua hata abaki uchi mbele yangu sisimki kabisa.

Nimecreate account fake ili nipate ushauri please

Jamani nifanyeje kwani si enjoy kabisa maumbile yake?

: ‘Nikikuta Mgambo Kituo cha Polisi Nitakula Sahani Moja


November 21 2016 ziara ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda iliendelea katika jiji la Dar es salaam, katika ziara hiyo RC Makonda amekutana na wananchi wa Yombo Temeke ambao walitoa kero zao mbalimbali ikiwemo suala la usalama, migogoro ya ardhi, rushwa kwenye vituo vya polisi pamoja na kero za daladala kukatisha vituo.

Wakati akitoa ufafanuzi wa moja ya majibu ya kero, RC Makonda amesema jeshi la polisi limekuwa likichafuliwa na baadhi ya mgambo ambao wamekuwa wakiruhusiwa kufanya kazi kwenye vituo vya polisi hivyo amepiga marufuku mgambo hao kufanya kazi kwenye vituo vya polisi badala yake wawe kwenye ngazi ya mtaa.

’Ni marufuku kituo cha polisi kuwa na mgambo na mimi nitafanya operesheni zangu, nikikuta mkuu wa kituo ameacha mgambo kwenye kituo chake nitakula sahani moja na Kamishna Sirro, wakati mwingine Jeshi la polisi linapakwa matope kumbe ni matope ya mgambo’-RC Makonda

Diamond Aelezea Sababu ya Kujiita Jina la Diamond Platnumz



Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii wakubwa barani Afrika kwa sasa. Siku za hivi karibuni alipata nafasi ya kushiriki tamasha la muziki la Coke Studio Afrika kusini ambapo alitengeneza wimbo uliowavutia wengi kwa kushirikiana na Cassper Nyovest, wimbo unaitwa My Heart.

Akiwa katika tamasha hilo alifanya mahojiano na waandaaji na moja ya yaliyowavutia wengie ni alipoeleza jinsi alipopata jina lake la sanaa ‘Diamond Platnumz.’

Akielezea chanzo cha jina hilo, Naseeb Abdul Juma alisema kuwa jina hilo lilianza kitambo alipokuwa akiimba ambapo rafiki zake mtaani walikuwa wakimwambia kuwa yeye ana kipaji kizuri cha kuimba na siku akipata mtu wa kukiendeleza, ataweza kuwa mwenye thamani kama Diamond.

Alieleza kuwa katika kipindi hicho walianza kumuita jina hilo la Diamond na kwavile hapakuwepo na msanii yeyote anayetumia jina hilo, akawaza kwanini asilitumie. Ndipo na yeye akaaza kujiita Diamond.

Akifafanua lilipotekea jina Platnumz, Naseeb alisema kuwa neno hilo lina maanisha mtu mtanashati mwenye swaga, mwenye muonekano wa kuvutia na mtu wakupendeza kila mara. Hivyo akajiita Diamond Platnumz na ukawa ndio mwanzo wa jina lake hilo.

Msikilize Naseeb Abdul Juma akielezea hapa chini. Vipande vingine vya mahojiano aliyofanya ameviweka kwenye ukurasa wake wa Instagram.

GHARAMA za Kumlinda Rais Mteule wa Marekeni Donald Trump Kwa Siku Moja Hizi Hapa



Tarehe 9, Novemba 2016 siku moja baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Marekani, aliyekuwa mgombea wa Chama cha Republican Donald John Trump alitangazwa kuwa mshindi baada ya kumgaragaza mpinzani wake wa karibu na mgombea wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton.

Baada ya kutangazwa kuwa Rais Mteule wa Marekani, vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo vinawajibu wa kuhakikisha yeye (Donald Trump) na familia yake wanakuwa salama wakati wote.

Kwa mijibu wa taarifa iliyotolewa na  Ofisi ya Meya wa New York, Marekani gharama za kumlinda Trump na familia yake kwa siku moja ni zaidi ya dola milioni 1 (TZS bilioni 2.2).

Mke wa Donald Trump, Melania Trump pamoja na mtoto wao wa miaka 10, wao muda mwingi huwa nyumbani sababu ya shule kufungwa hivyo hutakiwa kulindwa muda wote huku Trump akiendelea na shughuli nyingine za serikali.

Mbali na hao bado kuna watoto wengine wa Trump na wajukuu zake ambapo wote hao wanatakiwa kulindwa na maafisa wa usalama wa Marekani.

Afisa wa Polisi katika Jimbo la New York aliwaeleza waandishi wa habari siku ya Ijumaa kuwa ulinzi wa Rais Mteule na familia yake ni suala namba moja wanalotakiwa kulishughulikia. Kazi kubwa polisi wanayotakiwa kufanya ni kutoa usaidizi kwa Maafisa Usalama wa Taifa ambao hasa ndio wana jukumu la kumlinda Rais Mteule

Erick Shigongo Aamua Kufunguka Mahusiano yake na CCM, Adai Wanataka Kumdhulumu Haki yake



Mwandishi nguli hapa nchini, Eric Shigongo amesimulia masaibu anayoyapitia baada ya kuwa amefanya kazi ya Chama cha Mpainduzi (CCM) lakini hajalipwa fedha zake. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Shigongo ameandika waraka huu;

Nawaomba radhi sana wananchi wa Singida,  sikuweza kuwepo Namfua baada ya waandaaji kuahirisha tamasha, ipo siku tutakutana.

Nimekwishasema mara nyingi kwamba, hata mimi, kama ilivyo binadamu wengine huwa nina siku mbaya na nzuri katika maisha yangu, kwa sababu kwa watu wengi tafsiri ya maisha bora ni kuwa na gari, nyumba, kazi, fedha nk. Ni rahisi kudhani kwamba ninaishi maisha ya furaha kila siku, si kweli, kuna siku natokwa na machozi kama binadamu mwingine, naomba nikushirikishe sasa siku yangu ya Novemba 19, 2016, siku ya Jumamosi iliyopita, ili upate uhalisia wa maisha.

Usingizi ulikata saa tisa na nusu usiku, nikaanza kuyapitia maisha yangu na changamoto ninazokutana nazo, mambo ninayoyafanya lakini pia kufanyiwa na watu. Mawazo yangu haya yananifikisha kwenye uhusiano wangu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kwa muda mrefu sana nimekuwa kada wake, mara kadhaa nikijitoa mhanga mimi mwenyewe kukitetea na kukipigania nikiamini ndiyo chama pekee kinachoweza kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli.

Naipenda CCM, nakiamini chama hiki hata kama kuna baadhi ya watendaji ndani yake natofautiana na jinsi wanavyofanya mambo kiasi cha kuathiri hatma ya chama hiki kama taasisi, wapenzi, mashabiki na wanachama wake.

Pamoja na kuwa mfanyabiashara nimewahi kuacha kazi zangu na kuzunguka karibu nusu ya nchi yetu nikipiga kampeni na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, lakini kwa sababu mtu yeyote anayeonesha mapenzi kwa CCM hasa akiwa mfanyabiashara hutafsiriwa anajipendekeza au mwoga, pengine hivyo ndivyo ninavyoitwa, lakini kwangu mimi ambacho hunisukuma kufanya mambo haya ni mapenzi na imani niliyonayo kwa CCM kama taasisi na zilivyo sera zake.

Kama nilivyosema hapo awali, tatizo langu kubwa huwa ni watendaji wa CCM, ambao wakati mwingine hufanya mambo ambayo huathiri  mapenzi yangu kwa taasisi yenyewe, hali hii imewavunja moyo watu wengi sana waliokuwa na mapenzi pamoja na imani kubwa kwa CCM.

Yesu ni mwokozi wangu, daima nitazungumza ukweli, hata kama utanigharimu! Nakumbuka huko nyuma nimewahi kuzungumza ukweli kuhusu CCM kwenye ukurasa huu, baadhi ya viongozi wa juu hawakufurahishwa na nilichokiandika, Katibu Mkuu Kinana nikiongea naye ofisi kwake aliniambia “Eric wewe ni kijana wa hapa, siku nyingine ukiwa na suala la kuzungumza tueleze sisi moja kwa moja, usilipeleke barabarani!”

Nilikubaliana naye na sikuwa tayari kabisa kusema maneno yaliyotokana na mawazo yangu ya usiku gazetini tena, kwani nilimuahidi nisingefanya hivyo, lakini nifanye nini, nisemee wapi? Kama katibu mkuu wangu nampigia simu kila siku hapokei? Namuandikia ujumbe kwa njia ya WhatsApp na unaonekana umesomwa lakini hanijibu, tafsiri yangu ni ya haraka ni kwamba ananidharau ingawa mimi namuheshimu kama baba  na kiongozi wangu, angalau angekuwa anapokea simu hata kunipa tu matumaini, nisingefikia hatua ya kuzungumza hapa.

Kuanzia usingizi ulipokata saa tisa na nusu usiku, nilifikiria mambo mengi sana juu ya namna ambavyo baadhi ya watendaji wa CCM wamekuwa wakinifanyia pamoja na kujitoa kwangu kote kwa chama hicho, moyo unaniuma mno kwani sistahili hata kidogo kufanyiwa mambo ambayo leo natendewa na chama ambacho mimi binafsi naamini nimejitoa kiasi kikubwa mno kukitumikia kwa akili, muda na mwili wangu.

Inahitaji usiwe mtu mwenye hofu au uliyekata tamaa kufungua mdomo na kuzungumza nitakayoyasema leo, ndugu zangu, Watanzania wenzangu, moyoni mwangu pamejaa uchungu mwingi mno, acha niseme labda nitakuwa mwepesi! Sijui kitakachonipata, Mungu anajua, mimi ni msema kweli, nionavyo mimi ni bora kuzungumza ukweli ukapata matatizo kuliko ubaki hai ukiendeleza unafiki, NASHINDWA.

 Mawazo haya juu ya CCM yananitoa machozi  mke wangu akiwa usingizini kando yangu, sitaki kumuamsha, sitaki kumshirikisha kinachoendelea, mimi ni mtoto wa kiume mambo mengine natakiwa kukabiliana nayo mwenyewe, kwa muda mrefu naendelea kuwaza nikiwapitia viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia mwenyekiti mstaafu, mwenyekiti aliyeko madarakani, katibu mkuu na mweka hazina.

 “Mama!” saa kumi na mbili na dakika kumi namuamsha mke wangu.

“Bee!”

“Tulikubaliana kwenda hospitali Muhimbili kusalimia mgonjwa.”

“Kweli.”

“Mzima lakini?”

“Naendelea vizuri, wewe?”

“Mimi mzima, nina mafua tu kidogo!” nilimjibu hivyo kwa sababu sikutaka agundue kilichokuwa kimetokea.

Kawaida ya wanawake ni kujiandaa taratibu sana, mpaka tunaondoka kwenda Muhimbili tayari ilikuwa ni saa moja asubuhi, tumechelewa muda wa kuona wagonjwa. Mbele ya Jengo la Mwaisela, alipolazwa mgonjwa ambaye ni mkamwana wa mama mmoja aitwaye Mama Swai, ambaye tulikuwa tukiabudu naye Kanisa la Word Alive kabla hatujahamia Victory Christian Center, tunakutana na mlinzi mkali kama pilipili.

“Muda wa kuona wagonjwa umekwisha.”

“Tusaidie kaka” nambembeleza kwa muda, hatimaye akionekana kunionea huruma, anasema “basi aende mmoja tu, tena mwanamke, maana hii wodi ni ya wanawake.”

“Mama nenda basi wewe!”

Mke wangu anaondoka na kuniacha nimesimama peke yangu nje ya wodi, mawazo yananirejesha tena kwa CCM baada ya kubaki peke yangu, najiuliza ni kitu gani nimekikosea chama hicho mpaka kunitendea mambo wanayonitendea! Roho inaniuma, nasikia huzuni kubwa moyoni mwangu, niko chini kabisa kiroho leo, sina furaha hata kidogo, mawazo ya CCM na mambo wanayonitendea, wakati mimi nilishafanya mema mengi kwao yamenivuruga.

Dakika ishirini baadaye mke wangu anatokeza kutoka wodini, alikuwa amepewa muda mfupi sana, pamoja tunaongozana mpaka kwenye gari, namfungulia mlango, anaketi nami nakaa kwenye usukani na kuanza kuendesha kuelekea ofisini, anawahi kazini kwake kwa sababu leo ana sherehe ya watu waliokodisha hoteli.

Njiani nasikia wimbo wa vijana kutoka Kenya waitwao Sauti Sol, uitwao ‘Kuliko Jana’ nilishawahi kuusikia wimbo huo kabla, lakini leo unaonekana kuwa wimbo mpya kabisa kwangu, maneno yake yananigusa sana moyo, namshikirisha Vene kwenye wimbo huo, anaonekana kama hanielewi au ninachokiongea hakimgusi, bila shaka anawaza sherehe inayofanyika hotelini kwake.

“Hawa vijana wanaimba sana, natamani siku moja niwaalike hapa Dar es Salaam, nifanye tamasha kubwa la vijana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu, bure! Nifundishe vijana wa taifa hili uzalendo na kupenda nchi yao.” Natamka maneno hayo ingawa moyoni mwangu kuna uchungu mwingi;

Bwana ni mwokozi wangu,

 Tena ni kiongozi wangu,

Ananipenda leo kuliko jana!

Baraka zake hazikwishi si kama binadamu habadiliki,

Ananipenda leo kuliko jana,

Kuliko jana, kuliko jana,

Yesu nipende leo kuliko jana,

 Kuliko jana, kuliko jana,

Yesu nipende leo kuliko jana,

Nakuomba Mungu uwasamehe

Wangalijua jinsi unavyonipenda

Mimi wasingenisema

Na maadui wangu nawaombea

Maisha marefu wazidi kuniona ukinibariki

Ujue binadamu ni watu wa ajabu sana

Walimkana Yesu mara tatu kabla jogoo kuwika…

Safari inaendelea, wimbo uliokuwa ukipigwa redioni umefika mwisho, kwa kutumia simu yangu nilitafuta ‘You tube’ kisha kuuchagua wimbo huo ambao unaendelea kupiga mpaka namfikisha mke wangu ofisini kwake, kila unapokwisha naurudia tena, unanizidishia uchungu moyoni, namshusha mke wangu na kuendesha tena kuelekea ofisini kwangu.

Mawazo ni mengi, kichwa kimevurugika, Mariam, msaidizi wangu anaingia na kunitayarishia chai, nakunywa lakini haipandi. Baadaye anaondoa vyombo na kuniacha peke yangu, muda mfupi baadaye aliingia mzee Mbizo, sijui kama alinielewa kwa hali aliyonikuta nayo, nilikuwa kwenye siku yangu mbaya, niko chini sakafuni nawaza, baada ya salamu tu tofauti na siku nyingine zote ambazo mimi na yeye huongea mambo machache, anaaga na kuondoka.

Nabaki peke yangu nikiendelea kufikiria, naikumbuka siku ya mwisho nilipofika ofisi ndogo ya CCM pale Lumumba, ambako nilikwenda nikitarajia kulipwa fedha zangu ninazodai kwa kazi niliyoifanya (kwa leo sitataja ni kiasi gani) kama nilivyokuwa nimeahidiwa baada ya kuwa nimesubiri mwaka mmoja na miezi sita, hapo katikati nikiwa nimelipwa fedha kidogokidogo sana.

Tofauti na matarajio kwamba siku hiyo ningelipwa fedha zote, nikalipwa kiduchu tena! Nikiwa ndani ya ofisi ya mweka hazina wa chama, mama Zakia Meghji, yeye ni shahidi, kama nasema uongo au ukweli anajua, machozi yalinitoka! Hali yangu kibiashara ni mbaya, fedha nyingi ziko mikononi mwa CCM na nina madeni makubwa ninayodaiwa, baadhi ya wadai wanataka kupiga mnada mali zangu! Chama Cha Mapinduzi kimeniingiza kwenye matatizo makubwa.

Nakumbuka alichokifanya mama huyu ni kunipa  chupa ndogo ya maji ya Kilimanjaro na kuniambia “Kunywa maji mwanangu, upunguze uchungu!” nikayapokea na kuyanywa, niliondoka ofisini hapo nikiahidiwa kwamba ningelipwa muda si mrefu, lakini haikuwa hivyo, siku zinazidi kusonga na hali inazidi kuwa mbaya na hakuna anayeonekana kujali.

Kwenye saa 5: 00  asubuhi hivi, naamua kuachana na mawazo hayo kwani maisha bado yanaendelea  na kuamua  kwenda kuungana na wenzangu kwenye kikao cha asubuhi kujadili maendeleo ya Gazeti la Ijumaa Wikienda ili nifute kilichokuwa kikiendelea kichwani,  nafanikiwa kufanya kikao hicho bila mtu yeyote kugundua kilichokuwa kikiendelea akilini mwangu na baadaye narejea ofisini ambako naendelea kuusikiliza Wimbo wa Sauti Sol huku nikizidi kuhuzunika.

Muda mfupi baadaye anaingia Davina Lema, msimamizi wa kampuni yetu ya Blue Mark Real Estate ambayo inajishughulisha na upangishaji wa nyumba, tunaongea naye kuhusu biashara na namna ya kufanya biashara katika kipindi hiki kigumu, nampenda Davina, alianza kazi hii akiwa hajui chochote lakini sasa amemudu kazi, baada ya mazungumzo hayo ndiyo naanza kumweleza kidogo kuhusu maisha na namna ambavyo mtu unaweza ukatenda wema lakini ukalipwa ubaya.

Sikuweza kuzungumza hadi mwisho, machozi yananitoka mbele ya mfanyakazi wangu, si jambo jema lakini sikuwa na jinsi, siandiki haya ili nionewe huruma la hasha! Nawaeleza muone baadhi ya siku zangu ambavyo huwa zinakuwa, mtu asinione napita barabarani akadhani maisha yangu ni keki kila siku, kuna mateso na maumivu makubwa nyuma yake!

Alichofanya Davina ni kunitafutia tishu za kufutia machozi kisha kuondoka baada ya meneja wetu mkuu, Abdallah Mrisho kuingia na kunikuta katika hali mbaya niliyokuwa nayo, akaketi chini na kuanza kunidadisi ni kwa nini nilikuwa nalia! Kwikwi ilikuwa imenishika sikuweza kuongea, kuna jitu lilikuwa kooni ambalo nahisi ni hasira.

“Braza inaniuma sana, nimejitahidi maishani mwangu kuwa mtu mwema, nikikusanya senti tanotano kwa njia halali mpaka kufika hapa nilipo, mimi ni tofauti sana na wanasiasa ambao wanaweza kutia saini mkataba mmoja tu wa kifisadi wakaingiza bilioni ishirini au watoto wa viongozi wanaoweza kutumia majina ya wazazi wao kujipatia mikataba minono ya kuwatajirisha, kaka unajua mimi nadunduliza kila siku nikijinyima na kuishi maisha ya kawaida ili niwaachie watoto wangu urithi, leo hii nahisi kabisa nataka kunyang’anywa haki yangu niliyoitesekea kwa muda mrefu, inaniuma!

Kwa mwili huu nilikuwa na uwezo wa kushika bunduki na kuingia benki kuchukua fedha au kwenda Brazil kupakia mzigo mkubwa wa heroin au Cocaine na kuleta hapa nyumbani kuja kuharibu watoto wa watu akili, sikutaka kufanya hayo yote kwa sababu sitaki kufanya dhambi au kupata fedha ambazo baadaye nitajilaumu, nimechagua kufanya biashara halali kuanzia gazeti la shilingi mia moja mpaka leo shilingi elfu moja, kwa nini sasa kikundi fulani cha watu kininyime haki yangu? Sitakubali, ni bora nife kuliko kubaki hai wakati haki yangu inataka kuchukuliwa na wanaoona kwamba wana nguvu na hawawezi kufanywa chochote.”

Wakati nayasema maneno hayo yote nilikuwa nikilia kwa uchungu mno, meneja mkuu alijaribu kunituliza lakini alishindwa, roho ilikuwa ikiniuma sana, mimi mtoto wa maskini, niliyetoka chini kimaisha nikapambana mpaka hapa nilipo, unidhulumu kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo? (nitakitaja hivi karibuni). Hapana, ni bora kufa au kupigania haki mpaka tone la mwisho, huko ndiko kunaitwa kuwa mwanaume.

Baadaye nilitulia, tukazungumza na braza Mrisho kwa muda mrefu akinisihi nitulie wala nisichukue hatua yeyote, yeye akiamini haikuwa rahisi kudhulumiwa wakati tulikuwa na mikataba! Jambo moja ambalo hakulifahamu ni kwamba dhamana tulizoweka kwa waliotukopesha fedha zingeweza kuuzwa, hata kama baadaye tungelipwa na CCM ingekuwa haina maana kubwa, wazungu wana msemo usemao “Justice delayed is justice denied” yaani haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki ambayo haikutolewa, wakati wa kulipwa na CCM ni sasa ili tuepuke kuuziwa dhamana zetu.

Alipoondoka meneja mkuu ofisini kwangu, aliingia Nyemo Chilongani, mmoja wa vijana wachapakazi ofisini kwangu ambaye husimamia ukurasa wangu wa Facebook, aliongozana na wasichana wawili ambao aliwatambulisha kwangu kama mashabiki wa ukurasa wangu ambao walikuja ofisini kununua vitabu na walitaka niwasainie vitabu vyao na pia tupige picha pamoja.

Wasichana hawa walikuwa ni Zainabu na Dina kutokea Kigamboni, mara moja nilibadilisha muonekano wangu kama vile kilikuwa hakijatokea kitu, tukaanza kuongea mambo mbalimbali kuhusu maisha, nikiwaeleza umuhimu wa kuthamini vipaji maishani, ambavyo kila mmoja wetu anavyo, “Mtu anaweza kufeli darasani kama nilivyokuwa nikifeli mimi, lakini kipaji kikamuinua na kumfanya awe mtu mwenye mafanikio!”

Mwisho wa mazungumzo yetu nilipiga nao picha na kwa kweli walifurahi kukutana nami ambaye ujio wao na mazungumzo tuliyoyafanya ulisaidia sana  kubadilisha akili yangu na kunipa uwezo wa kuketi chini na kuandika haya unayoyasoma leo.

Hivyo ndivyo siku yangu ya Novemba 19, 2016, ilivyoanza, nifuatilie wiki ijayo nipate kukueleza kwa undani kilichotokea mpaka nikajikuta katika haya niliyoyaandika leo.

MTV Base south Africa, Imetaja List ya Marapa 10 wakali Kutoka Bongo Waliotisha zaidi Kwa Mwaka 2016



Sasa Luninga ya MTV Base south Africa, imetaja list ya marapa 10 wakali waliotisha zaidi kwa mwaka 2016.

Namba moja wamempatia rapa Fareed ‘Fid q’ Kubanda kutokea Mkoani Mwanza, Itazame list nzima hapo chini then tuachie maoni yako,

#BongoHipHop |Tanzania| #TZHottestMCs 2016

1.Fid Q
2.John Makini 
3.AY 
4.Mwana FA
 5.ROMA
6.Mr. Blue 
7.Nikki Wa Pili 
8.G Nako 
9.Prof Jay 
10.Chindo Man

Hawa Wadada Wenye Majina Makubwa Wanatoa Wapi Pesa za Matanuzi?



Nikimuona Diamond na kina Kiba na wanamuziki wengine wakila bata najua ni mziki wao unawalipa. Ila kuna hawa watu maarufu huko Instagram kama kidada fulani Tunda na wengine, picha zao zimekaa kibatabataaa lakini niulize huwa wanafanya kazi gani maana hata kama ni kuimba kama hata wamewahi jaribu bado hawana majina makubwa, hawaonyeshi kumiliki labda hata mabiashara.

Hebu jamani kama wapo humu watuambie kazi zao maana hata kulalama njaa kama wengine wanaolialia hawasikiki.

Tafakuri tu japo ni maisha ya watu hayanihusu

Mchungaji Atumia Dawa ya Mbu ya Doom Kuwaponesha Watu Kwa Miujiza




Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amelaaniwa vikali.

Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, pmchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.

Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko.

Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.


Nchi hiyo imekuwa na wimbila visa ambapo wajumbe wa kanisawamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili kupata tiba.

Katika picha zilizosambazwa kwenye kurasa za Facebook na Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mountzion General Assembly katika jimbo la Limpopo ,anaeonekana akimpulizia dawa ya kuuwawadudu moja kwa moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya mwili mbele ya waumini wa kanisa lake.

Amemueleza mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa mmoja wa wanawake kwasababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa "yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu".

Pia alidai kuwa dawa hiyo ya Doom inaweza kuponesha saratani na virusi vya HIV vinavyosababisha.

Kampuni inayotengeneza dawa ya Doom kwa nembo ya Tiger inasema kuwa inamsihi s mchungaji aliyejitangazia kuwa ''nabii'' huko Limpopo - Lethebo Rabalogo kuacha kuwapuliza dawa ya wadudu kwenye nyuso za binadamu kama sehemu ya imani ya kuabudu:

''Tunaona tendo hili kuwa kutia hofu kubwa , na tungependa kubainisha wazi kwamba ni hatari kupulizia Doom ama dawa nyingine yoyote ile ya wadudu kwenye macho ya watu''.

''Doom ilitengenezwa kwa ajili ya kuwauwa wadudu wa aina fulani ambao wameonyeshwa kwenye kopo , na maelezo yaliyoandikwa bayana kwenye kopo la Doom yameonya juu hatari na yanapaswa kufuatwa.''

''Kampuni ya Tiger iko katika mchakato wa kuwasiliana na Nabii kumtaka aache kufanya tendo hilo'' imesema kampuni ya Tiger

Mbunge Godbless Lema Aendelea Kusota Gerezani...Akosa Dhamana



ARUSHA: Mahakama Kuu yamnyima Mbunge Lema dhamana arudishwa gerezani. Yawataka Mawakili wake warudishe kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Lema amesota rumande tangu alipokamatwa Novemba 3, 2016 akiwa mkoani Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha ambapo anashtakiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya Rais Magufuli.

Mawakili wake wakiongozwa na Peter Kibatala wamesema wanakata rufaa ndani ya muda wa masaa mawili.

Soudy Brown Afanyiwa Interview, Kumbe Alikuwa Anafanya Kazi TBC



Mzee wa Ubuyu Soudy Brownkafanyiwa interview na TBC amabapo ana dai ndio sehemu iliyomlea
amefungukia aanvyotukanwa instagram na anavyochulia
Pia amesema anapenda kuvaa mask kama swag tu, na akiivua anakuwa sio Soudy Brown tena 

Wakili wa Serikali Amuomba Radhi Hakimu kwa Kushindwa Kumkamata Tundu


Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemuomba radhi Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumkamata mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio.

Wakili Mwita alifanya hivyo jana baada ya hakimu huyo, Thomas Simba kumuhoji sababu za kushindwa kutekeleza amri hiyo wakati hati ya kumkamata ilitolewa Novemba 3, 2016 na wakili huyo kuisaini. “Kwa nini hamkumkamata” Si mlikuwa na wajibu wa kumkamata? Mnamuogopa?” alihoji hakimu huyo.

Hata hivyo, pamoja na kuomba radhi hiyo mahakama imechukua hati ya kusafiria ya Lissu ili kudhibiti safari zake nje ya nchi kwa kuwa amekuwa akisafiri bila kuitaarifu mahakama.

Katika kesi hiyo, Lissu na watu wengine watatu wameshtakiwa kwa makosa matano ya uchocheza kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti la Mawio kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 28, 2016 na washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Kabla ya uamuzi huo, Wakili Mwita alisema jana ilikuwa siku ya kesi hiyo kutajwa na kwamba upelelezi unakaribia kukamilika.

Kuhusu madai ya kudharau mahakama Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lissu aliiambia mahakama kuwa mteja wake yupo mahakamani, hivyo ametii amri ya mahakama na kwamba jukumu la dhamana ni kuhakikisha mshtakiwa anakuwapo mahakamani wakati wa kesi yake na kwamba uwepo wake ni kutii masharti ya dhamana.

Hata hivyo, Wakili Mwita alidai kuwa kitendo cha Lissu kutofika mahakamani mara mbili mfululizo ni kama kuonyesha dharau kwa mahakama hiyo.

Mwita alidai kuwa Lissu ni mwanataaluma wa sheria na anafahamu taratibu za kufuatwa kama hafiki mahakamani na kwamba mdhamini si mbadala wa mshtakiwa mahakamani.

“Alipaswa kuandika barua kuitaarifu mahakama hii kama wakili kuwa ana kesi ya uchaguzi anayoiendesha Bunda na kuambatanisha na samansi ama orodha ya kesi. Tunaomba mahakama iheshimiwe na jukumu la kumfutia dhamana ama kutokumfutia dhamana Lissu bado lipo mikononi mwako mheshimiwa,” alieleza wakili huyo wa Serikali.

Akizungumzia hoja hizo, Hakimu Simba alisema Lissu ni wakili maarufu, msomi na anajua taratibu zote za mahakama, lakini wadhamini wake wanababaika, hivyo alimtaka aeleze sababu za kwenda Ujerumani bila kutoa taarifa mahakamani.

Lissu alijibu kuwa hakuwa na nia ya kuidharau mahakama, wala kuikimbia kesi inayomkabili bali alikwenda Ujerumani katika mazingira ya dharura.

Hakimu Simba alimwambia mahakama inafahamu kesi za uchaguzi na maelekezo yake, hivyo ikamuuliza sababu za kutotoa taarifa wakati alipokwenda kushughulikia kesi ya Bunda

“Nilipopata taarifa ya kwenda kuiendesha kesi hiyo ilikuwa ni siku moja baada ya kutoka nchini Ujerumani na kwamba niliandika barua ya kuitaarifu mahakama na nilituma iletwe mahakamani kupitia wasaidizi wangu,”alisema Lissu.

Lakini Hakimu Simba alisema: “Hakuna barua iliyotufikia. Usituingize katika migogoro kutokana na nafasi yako katika jamii ya mwanasheria. Hatukuogopi labda upande wa mashtaka ndio wamekuogopa.

“Tunataka kufuata mfumo, hatutakuogopa na wala hatutakuonea. Hapa naona upande wa mashtaka wanapiga blaa blaa, tuelewane tunaichukua hati yako ya kusafiria ili ukitaka kusafiri tujue.”

Rais Mugabe Asema Anarogwa



Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa mika 92, anazungumzia kuhusu kustaafu , lakini swali ambalo bado watu wanahoji ni ikiwa kweli anamaanisha hilo.

Mwishoni mwa juma Bwana Mugabe aliuambia mkutano wa watu wapatao 400- walio piagania uhuru kwamba ikiwa atastaafu anapaswa kupewa fursa "inayofaa" kufanya hivyo.

Pia aliwakosoa baadhi ya viongozi wa chama chake cha Zanu-PF kwa kumuombea afe na kujaribu kumroga ili wachukue nafasi yake.

Malumbano ya ndani kwa ndani miongoni mwa wafuasi wa chama tawala ya kutaka kumrithi Bwana Mugabe yameongezeka huku kiongozi huyo akionekana kuendelea kudhoofika zaidi.

Lakini si mara ya kwanza Kwa Bwana Mugabe kuongelea kuhusu kuachia madaraka it's
Mwaka 2006 alitangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008.

Licha ya hayo aligombea na kushinda katika uchaguzi uliokuwa na ghasia ambao matokeo yake yalibishaniwa.

Kwa hivyo haijawa wazi ni lini , kama kweli Rais Mugabe ataondoka madarakani.
Mnamo mwioshoni mwa juma kamati za kikanda za chama tawala cha, Zanu-PF provincial zilimuidhinisha kama mgombea wake katika uchaguzi wa 2018 , ambapo atakuwa na umri wa miaka 94.

Chama hicho kitaidhinisha uamuzi huo katika mkutano mkuu wa chama utakaofanyika mwezi ujao.
Kwa hiyo kwa sasa haionekani kama kweli anaangalia uwezekano wa kustaafu.
Powered by Blogger.