Saturday, December 10, 2016

ALIKIBA Afunika Tuzo za EATV Awards



Mkali wa ‘Aje’, Ali Kiba jana aling’ara zaidi katika tuzo za EATV 2016 zinazoandaliwa na kituo cha runinga cha East Africa zilizotolewa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye huku msema chochote akiwa mtangazaji wa zamani wa kituo hicho, Salama Jabir.

Kiba aliongoza orodha kwa kunyakua tuzo tatu katika vipengele vyote vitatu alivyokuwa akiwania. Tuzo ya kwanza ni Msanii Bora wa Kiume, Wimbo Bora wa Mwaka (Aje), na Video Bora ya Mwaka (Aje).

Akitoa neno la shukurani mara tatu, Mfalme Kiba alisitiza kuwa tuzo hizo ni za mashabiki wake waliomuwezesha na kwamba yeye anachukua tu kwa niaba yao.

Tuzo nyingine nzito ya heshima ilienda kwa DJ Bony Love, aliyekuwa mmiliki wa studio za Mawingu na mmoja kati ya waasisi wa muziki wa Bongo Flava.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.