Wednesday, December 7, 2016

PAUL Makonda Kuwashindanisha Christian Bella na Banana Zoro Kuimba Live....Bella Ajigamba Kuchukua Mil 50 za Zawadi


Mkali wa masauti Christian Bella amejinadi kuwa atamshinda muimbaji mkongwe Banana Zorro katika pambano la kuimba live lililoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.


RC Makonda wiki moja iliyopita aliwataka wasanii hao wawili kuandaa show ya pamoja ili washindane kuimba live na mshindi atampatia tsh milioni 50.

Akiongea na Bongo5 wiki hii Christian Bella, amedai hana shaka na pesa hizo kwani anajua atamshinda Banana na kuondoka na kitita kicho kikubwa cha pesa.

“Tunamshukuru Mh Paul Makonda ni wazo zuri sana kwa kutujali vijana, kwa kujali vipaji na kuvithamini,” alisema Bella. “Kwahiyo sisi tunaiandalia mazingira ili kuangalia itakuwaje kwa sababu tunatakiwa kuwa serious sana lakini tumeshapanga itakuwa mwezi wa pili au wiki ya mwisho ya mwezi Januari,”

Aliongeza, “Kwa upande wangu mimi sasa najiandaa, mimi sitaruka sarakasi bali nitaperform vizuri ngoma zangu zote kali, niimbe zaidi, nitafanya performance ya hasira ili nipate hiyo hela. Lakini mimi naamini hiyo hela niyakwangu hata kama Banana Zorro ni mkali na anaimba vizuri, mkongwe, kipaji lakini naamini mimi nitachukua hiyo hela,”

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.