Home »
KIMATAIFA
» WAFANYABIASHARA wa Viungo vya Binadamu Wakamatwa
Utawala nchini Misri umewakamata madaktari, wauguzi na maprofesa wanaoshukiwa kuwa kwenye mtandao wa kimataifa wa biashara ya viungo vya binadamu.Kukamatwa kwa takriban watu 25 siku ya Jumananne pia kuliwahusisha wale wanaonunua viungo hivyo.Utawala pia ulipata mamilioni ya dola na dhahabu.Ni kinyume cha sheria kununua viungo vya binadamu nchini Misri lakini umaskini husababisha watu wengi kuuza viungo vyao.Shirika la kupambana na ufisadi lenye nguvu, linadai kuwa mtandao uliolengwa uliwajumuisha wamasri na waarabu na ulitumia fursa hali ngumu ya kuichumi ya watu kununua viungo vya watu na kisha kuviuza kwa faida kubwa.
0 comments:
Post a Comment