Wednesday, December 7, 2016

MAREHEMU Wanaodaiwa Mikopo HESLB, Kusamehewa



Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pamoja na na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imejikuta ikitoa taarifa zinazokinzana kuhusu wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu ambao tayari wamekwisha poteza maisha.

Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya amesema wanafunzi ambao wamefariki huku wakiwa na deni la Bodi ya Mikopo wanasamehewa madeni yao kwa kuwa hawawezi kupatikana tena.
Manyanya alitoa ufafanuzi huo hivi karibuni wakati akiwa katika kipindi cha Kikaangoni kinachoruka kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, ambapo alisema suala la kufariki ni mipango ya Mungu, na hakuna mtu anayeweza kujiua makusudi ili kukwepa kulipa deni lake.

Akifafanua zaidi wakati akijibu swali la mmoja kati ya wananchi waliouliza maswali, Manyanya alisema serikali ina uwezo wa kujiridhisha kuwa mdaiwa fulani amefariki kwa kufuatilia nyaraka muhimu, na kuwataka wadaiwa wasitumie msamaha huo kujisingizia vifo

"Mimi ndiyo serikali, unapaswa kuchukua taarifa yangu kwamba waliofariki wakati wanadaiwa, watasamehewa madeni yao, naamini hakuna mtu atajiua makusudi ili kukwepa, tukibaini kama kuna kughushi vifo, basi hatua za kisheria zitachukuliwa" Alisema Manyanya.

Hivi karibuni mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo akizungumza na East Africa Radio alisema kuwa madeni ya wadaiwa waliofariki yatalipwa na wanafamilia, wadhamini pamoja na ndugu walio hai.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.