Kwenye interview niliyofanya na Diamond hivi karibuni, nilimuuliza kuhusu kuandamwa na tetesi za kumsaliti mchumba wake Zari na jinsi anavyozichukulia. Katika moja ya majibu yake, staa huyo alisema, “There is no way simba akapita katika zizi la swala akaondoka watu wakasema hakula swala hata mmoja, watasema tu alikula hata kama hakula.”
Na sasa maneno yake huenda yakawa yametimia. Ni kwasababu, Simba anasingiziwa kula swala mzuuuuri wa Zimbabwe, jina lake wa kuitwa Jackie Ngarande.
Ilianza kama utani baada ya Diamond kuita msichana wa kujumuika naye wakati akiimba wimbo wake Kamwambie kwenye ukumbi wa HICC wa Harare mbele ya mashabiki zaidi ya 7,000 waliokuwa wakitazama show hiyo.
Kwa mujibu wa mshiriki wa shindano la Big Brother Afrika, Pokello Nare aliyeipost video hiyo juu kwenye akaunti yake ya Instagram, walimchagua Jackie kwenda kumpa kampani fupi Diamond juu ya steji hiyo kwakuwa waliamini kuwa ni chumaa haswaaa!
“When @diamondplatnumz asked if Zim had sexy women.We sent in a representativeπππ @jackiengarandeofficial on shift for #TeamSexyZimWomen,” aliandika Pokello.
Muda mfupi baadaye, zikazuka tetesi kwenye blog mbalimbali za Zimbabwe kuwa Diamond na mrembo huyo walionana kabla. Page ya Instagram ya TZShaderoom, ilikuza zaidi tetesi hizo kiasi cha kumfanya mrembo huyo kuzungumza yake na kukanusha yanayosemwa.
“I am not sure were you got this information ,but well .I think as a gossip blogger sometimes its good to do your own research before you attach people’s name’s on lies and stories that can cause malicious damage’s and bad reputation on one’s name,” aliandika Jackie.
“The problem is that i don’t understand Swahili so it took me time to look for a translater so i could reply you. My main worry is that you are more interested in lies than the truth. Nothing is permanent in this wicked world not even your gossip or lies will not last forever. Im sure the person who feeding you all this is up for my downfall but Guess what ,I serve a bigger GOD. I had to leave my throne to address a peasant like you ..because you know what I usually do not leave the throne ..ππππππ,” aliongeza.
“Divert this energy you waste writing gossips into things that are productive and beneficial to you and your future .Unless you are a gettting paid to write lies i will say Madam /Sir @tzshaderoom
Continue doing your work for your salary is going to deposited into your bank account.Other than that Sorry for you π’π’π’π’.”
TAFSIRI:
Sina uhakika ni wapi umepata hizi taarifa, lakini sawa. Nadhani kama blogger wa udaku wakati mwingine ni vizuri ukafanya utafiti wako mwenyewe kabla ya kuambatanisha majina ya watu kwenye habari za uongo ambazo zinaweza kusababisha madhara na sifa mbaya kwa jina la mtu. Tatizo ni kwamba, sielewi Kiswahili hivyo ilinichukua muda kutafuta mtu wa kutafsiri ili niweze kukujibu. Hofu yangu kubwa ni kwamba unavutiwa zaidi na uongo kuliko ukweli. Hakuna kitu cha muda wote kwenye ulimwengu huu katili; hata umbea wako au uongo utaweza kukaa milele. Ninaamini mtu anayekulisha yote haya anataka nianguke lakini, ninamhudumia Mungu mkubwa. Imebidi niache kitI changu cha enzi ili nikujibu mkulima kama wewe sababu siku zote huwa sikiachi. Peleka nguvu hii unayopoteza kuandika udaku kwa vitu vingine vyenye maana na faida kwako na siku zako za usoni. Labda kama unalipwa kwa kuandika uongo nitasema endelea kufanya kazi yako kwakuwa mshahara wako unaenda kuweka kwenye akaunti yako ya benki. Tofauti na hayo, pole kwako
Pamoja na tetesi hizo, show ya Diamond inadaiwa kuwa ya kihistoria na ameacha heshima kubwa kwenye nchi hiyo inayotawaliwa na Robert Mugabe.
0 comments:
Post a Comment