Sunday, December 25, 2016

UKWELI Kuhusu Lulu Diva Kutoka Kimapenzi na Barnaba Classic



Mwanadada ambaye ameingia kwa kasi ya aina yake kwenye game ya bongo fleva, Lulu Diva, amevunja ukimya na kufunguka kuhusu skendo za yeye kulala chumba kimoja na msanii Barnaba Classic, walipokuwa wamekwenda kufanya video nchini Afrika Kusini.


Akifunguka kwa watanzania kupitia kipindi cha FNL cha EATV, Lulu amesema taarifa hizo siyo za kweli na kwamba anamchukulia Barnaba kama kaka yake, hivyo hawezi kumvunjia heshima kwa kuwa na mahusiano naye, wakati akijua kuwa Barnaba anaye mke wake wa ndoa.

"Barnaba na mimi tunaheshimiana sana, tulipokwenda Sauzi hatukufanya chochote, yule ni kaka yangu hata tukiwa chumba kimoja hatuwezi kabisa kufanya chochote, yule ni kaka yangu, kwahiyo taarifa hizo siyo za kweli" Alisema

Kuhusiana na mahusiano yake na mke wa Barnaba amesema wanafahamiana na wanaishi kama marafiki "Mimi na mke wake tunafahamiana na ni marafiki wa karibu sana na mambo mengine tunashauriana"

Amesema kila kitu walichokifanya kule kilikuwa ni sehemu ya kazi iliyowapeleka kule na si vinginevyo
Mbali na Barnaba, Lulu alipangua pia skendo nyingine zinazomkabili za kutoka kimapenzi na wasanii wa kiume Bongo, na wote alisema ni kaka zake.

Lulu amefanya kolabo na Barnaba na tayari ameachia video ya ngoma hiyo inayokwenda kwa jina la Milele ambayo ndani ya wiki mbili ilikuwa imefikisha views zaidi ya laki 2.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.