Sunday, December 11, 2016

MZEE Aliyeweka Tangazo la Kutafuta Mke Afunguka Sababu ya Kufanya Hivyo


Mzee Athumani Bakari Mchambwa (76) aliyeweka tangazo la kutafuta mke maeneo ya Mtoni Mtongani, Dar es Salaam amefunguka sababi ya kufanya hivyo.


Mzee Mchambwa ameiambia Global TV kuwa ameamua kufanya hivyo ili mwanamke yeyote atakayekuwa tayari kuolewa naye atambue mapema vigezo na masharti anayotakiwa kufanya na atakuwa anayatambua majukumu yake mapema kwani hata siku akibadilika hataweza kumsumbua sana.

Akitaja sababu ya kutafuta mke mwingine wakati tayari ameshaoa, Mzee huyo amesema, “Mimi nina kawaida ya kuwa na wake wawili, hayo ndio maisha yangu kutoka miaka yote lazima niwe na wake wawili. Sasa huyu mke mkubwa ndio alikuwa hapa Dae rs Salaam, kuangalia watoto wajukuu, nyumba na mambo mengine kadhalika.”

“Mara nyingine anapokuwa na wasaa anakuja shamba pia kucheki taratibu za shamba lakini la zaidi mimi na yule wa shamba tunakuwa shamba. Sasa nilichokuwa nakikusudia baada ya huyu kufariki lazima nipate mtu mwingine ambaye anisaidia mawazo ya kufikia pale ninapopataka mimi.”

Mzee huyo ameongeza kuwa mke wake huyo alifariki Agosti 6 ya mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.