Home »
KIMATAIFA
» ALIYEKIMBIA Mgomo wa Madaktari Kenya Ajifungua Watoto 5 Tanzania,
Moshi. Raia wa Kenya, Bahati Tabu (37) amejifungua watoto watano mjini hapa Mkoa wa Kilimanjaro alikokimbilia kupata msaada kutokana na mgomo wa madaktari na wauguzi unaoendelea nchini humo.Mgomo huo unaohusisha madaktari na wauguzi zaidi ya 5,000 wa hospitali za Serikali, ulianza Desemba 6, mwaka huu na kudaiwa kusababisha zaidi ya wagonjwa 40 kupoteza maisha.Hata hivyo, watoto wanne kati ya hao walifariki dunia kwa kufuatana kila walipozaliwa katika Kituo cha Afya cha Faraja Himo.Akizungumza na gazeti hili kituoni hapo jana, mzazi huyo alisema huo ulikuwa ni uzao wake wa 11 na tayari ana watoto 10, miongoni mwa hao kuna mapacha.Aeleza alivyokimbilia TanzaniaBahati alisema alishindwa kwenda hospitalini nchini kwao kutokana na mgomo wa madaktari na wauguzi unaoendelea kushinikiza nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi.“Baada ya kuanza kuumwa uchungu, majirani walinichukua na kunileta Tanzania kujifungua na nilipofika hapa (Himo) nilikuwa tayari nakaribia kujifungua,” alisema Bahati.Alisema alijifungua kwa njia ya kawaida watoto hao, wanne wakiwa wa kiume, lakini bahati mbaya walifariki dunia na kubakia na wa kike mwenye uzito wa gramu 600.“Imeniuma sana, sina jinsi namuachia Mungu kwani ndiye anajua kwa nini ameamua kunipa na baadaye kuwachukua tena,” alisema huku akibubujikwa machozi.Alisema alipokuwa mjamzito, alikwenda kliniki na kuambiwa ana watoto wanne na siyo watano, majibu ambayo yalimpa woga na hofu ya namna ambavyo angewalea. “Nilijawa na hofu baada ya majibu hayo kwa sababu nimekuwa nikilea watoto wangu mwenyewe na huu uzao wa jana (juzi) wa mapacha ni wa 11, awali nilishazaa tena mapacha,” alisema Bahati.Alisema anaishi kwenye nyumba ya kupanga na kujishughulisha na kazi ya kufua nguo za majirani ili aweze kuwatunza watoto wake 10 na baada ya uzao wa juzi watakuwa 11.“Hapa nilipo sijui nitatokaje hospitali kwa sababu hata mwanamume aliyenipa mimba hatuna mawasiliano mazuri. Majirani ndiyo wameenda kuchangisha fedha ili nilipe bili,” alisema.Daktari aeleza watoto walivyokufaDaktari kiongozi wa kituo hicho, Dk Samwel Minja aliliambia gazeti hili kuwa walimpokea Bahati juzi akitokea Taveta Kenya baada ya kukosa huduma.“Wakati anakuja chupa ya uzazi ilikuwa imepasuka na alituambia kuwa mimba yake ilikuwa na miezi sita, lakini anajisikia uchungu. Tulivyompima tuligundua kweli ni mimba ya miezi sita, lakini tumbo lilikuwa kubwa kuliko umri wa mimba. Kabla hatujamfanyia uchunguzi zaidi, akaanza kujifungua mtoto wa kwanza ambaye ni wa kike akiwa na gramu 600 baada ya muda mfupi alijifungua mtoto mwingine akakaa kama dakika tano akafariki.“Baada ya dakika 15 tena akajifungua mtoto wa tatu ambaye naye alikaa dakika tano akafariki. Baada ya robo saa akajifungua mtoto wa nne ambaye naye alikaa dakika tano akafariki. Baadaye tumbo la mama likawa linaonyesha bado lina watoto. Akaa baada ya nusu saa hivi alijifungua mtoto wa tano ambaye naye alifariki baada muda mfupi,” alisema daktari huyo.Kwa mujibu wa Dk Minja, Bahati alijifungua salama watoto wake wote na hali yake inaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment